Ushawahi faidika na roho mbaya uliyo nayo?

Ushawahi faidika na roho mbaya uliyo nayo?

Sensei Tai

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
168
Reaction score
466
Wewe ni bosi upo kampuni flani au kwenye taasisi ya serikali lakini unatumia mamlaka yako vibaya kwa kuwakandamiza na kuwanyanyasa walio chini yako na kuwadhulumu stahiki zao, nini faida ya yote hayo unayoyafanya?

Zikitangazwa ajira kwenye ofisi yako unaitisha interview kama formality tu lakini tayari una list ya watoto wa ndugu zako au jamaa zako ambao umeshawaandalia hizo nafasi bila kujari kuna watoto wa masikini ambao hata nauli ya daladala wameomba ili waje kushiriki usaili ambao ni geresha tu, unapata faida gani kwa kufanya yote hayo?

Wewe ni nesi upo hospital flani lakini unawafokea wagonjwa na watu wanaokuja kuona ndugu zao kama vile umewazaa wewe, unadhani utadumu kwenye hiyo kazi milele?

Kuna watu wamebarikiwa kuwa na uwezo kiuchumi lakini anaona ni bora vyakula viozee kwenye fridge ,awape mbwa chakula au atupe jalalani kuliko kumsaidia jirani yake ambae analala na njaa.Unadhani unachofanya nini sahihi?

Kuna wale ambao wanachagua misiba ya kuhudhuria, atahudhuria tu misiba ambayo anajua marehemu ni mtu mwenye uwezo au anatokea familia yenye kujiweza kiuchumi, unadhani wewe utaishi milele ?

Kuna watu wanapokea mishahara mikubwa lakini hawavimbi na kuwadharau watu wengine hata kama hawana elimu, unadhani wewe unaepokea 500k per month inatosha kabisa kukufanya uvimbe na kuwadharau wenzako?

Hapa duniani kuna dini nyingi sana lakini siku hizi watu wanatumia dini kuficha maovu yao, akienda kanisani au msikitini atatoa sadaka kubwa sana ili apate sifa lakini kwenye ofisi yake anadhulumu wafanyakazi, kuwalipa vipato vidogo na kuwacheleweshea mishahara, unadhani kwa kuficha maovu yako kwenye kimvuli cha dini unamdanganya nani?

Ndugu zangu maisha haya ni mafupi sana, hata uwe na mali nyingi kiasi gani lazima utaondoka tu na hizo mali hutazikwa nazo

Tunayo mifano hai ya watu wengi mashuhuri ambapo walikua wanajiweza kiuchumi lakini walishaondoka kwenye uso wa dunia na pesa zao hazikusaidia kitu katika kuwafanya waendelee kuwa hai.

Jitahidi kutenda wema mana wema hauozi, lakini kubwa zaidi tukumbuke kuna kifo kinatusubiri na kadri siku zinavyokwenda mbele na ndivyo ambavyo tunazidi kulisogerea kaburi.

Tujitahidi kutenda wema japo kwa kiasi mana dunia sio makazi ya kudumu.
 
Endeleeni kujidanganya hamjakutana na watu wanaokutaka uwe na roho mbaya ndiyo uishi nao kwa heshima na bila kufuatiliana sana .
Mkipata muda watafute watu wanaitwa wamalila kwao na mpenja huko bila roho mbaya utadharaulika na kupandwa kichwani na watoto wadogo
 
Back
Top Bottom