Ushawahi kuacha kazi bila kupata kazi?

Ushawahi kuacha kazi bila kupata kazi?

Mr Gratitude

Member
Joined
Aug 8, 2020
Posts
48
Reaction score
66
Mradi uliokuwa unautegemea unakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Unaamka asubuhi hauna ratiba ya kwenda mahali popote, majirani wambeya wanakuuliza maswali ya kipuuzi "vipi Leo mbona hujaenda kazini" siku chache za mwanzo unawajibu kuwa upo off day baada ya muda unawaambia kua upo likizo. Asubuhi unaulamba unabeba begi ukiwa kwenye daladala ndio unawaza uende wapi! Kutafuta mchongo.

Unakosa hela ya kumhonga demu wako hakuelewi, suruali na boxer zinachakaa hauna hela ya kufanya shopping, baadaye Mungu anakufanikisha unapata mchongo mwingine, amani ya moyo inarudi tena unakaa chini unakumbuka ule msemo maarufu "usiache kazi bila kupata kazi"
 
Ni mjinga pekee ndiye anaweza kuacha kazi, huku akiwa hana shughuli nyingine ya kufanya. Maisha mtaani ni mepesi sana ukiwa na shughuli ya uhakika ya kukuingizia kipato.

Muhimu tu ni kujipa muda wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi magumu ya kuondokana na huo utumwa wa kuajiriwa.

Biashara iliyosimama kwa miaka isiyopungua miwili, vyanzo vingine vya mapato mfano kodi ya pango, ufugaji wa kisasa, kilimo cha uhakika, nk humpa mtu ujasiri wa kuacha kazi kirahisi. Na wala siyo hizo Qnet, au kubet. Asilimia kubwa ya watu mtaani hawaja ajiriwa! Na wanaishi. Ni maamuzi tu.
 
Back
Top Bottom