Simbamteme
JF-Expert Member
- Sep 10, 2011
- 804
- 2,131
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.
Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nilipigilia kipensi changu na ka t-shirt flan hivi local nikachagua sehem nikakaa, kutizama vizuri nikaona kuna meza amekaa mdada mmoja hivi and of coz she is gud looking nikaamua kujitosa angalau kumpa hata hi 'coz tulikuwa wateja 2 tu, nikamfata nikamsalimu.
Yule dada kwanza alinishusha kuanzia juu mpaka chini then akaitikia salamu yangu ki-design kama namsumbua flani hivi. Nikaomba kujumuika nae kama asipojali. Jibu lake ndo lilinitoa confidence kabsa, alinambia: "Kwahiyo kaka unadhani kila msichana akikaa peke yake anahitaji kampani? Hapana sihitaji" Dah, mwanamme nikajizoazoa pale nikarudi nilipokaa. Nilikaa kama masaa ma3 hivi nikaamsha zangu. Sasa kilichotokea jana ndo kimenifanya niandike huu uzi.
Nilipokea maagizo kuanzia J3 ya wiki hii kuwa leo watakuja watu wa Taasisi flani ya kifedha kutoa semina kwa sisi wafanyakazi kwa ajili ya kutushawishi kujiunga na huduma za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.
Asubuhi mida kama ya saa 3 hv ugeni ukafika, walikuwa watu kama 7 hivi, kati yao alikuwepo yule dada nilieonana naye weekend.
Wakaingia ofisini nikawakaribisha, wakati mkubwa wao anatoa introduction macho nikayakaza kwa yule dada, bahati nzuri tukagonganisha macho, akashtuka flani, nikajua kashanikumbuka.
Baada ya semina kuisha ikafika kipindi cha watu kujiunga sasa kwa walioshawishika. Nikamfata yule dada nikamuomba aje anielekeze namna ya ujazaji fomu. Alivyofika tu, nikamuuliza "Unanikumbuka?" Akachekaaa, akaniambia "Yani wewe, sikutarajia kama unaweza kuwa unafanya kazi huku", nikamuuliza ulitarajia niwe nafanya kazi wapi? Akaishia kucheka tu. Mawasiliano yake kanipa; fresh bila shida kabisa.
Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?