Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Tuna tofauti kijinsia
Ila katika eneo la kazi ama elimu haimaanishi mwanamke ana uwezo wa chini

Mh Rais ni Mama Yetu Mpendwa SASHA🥰
Mbona huwa siwaoni kwenye kazi ngumu Kama za zege,kuchimba hata mashimo ya vyoo,makondakta hawazidi labda 50 hapa mjini,madereva ni wa kuhesabu, hata wabunge ukiangalia wanawake wanabebwa viti maalumu tu ni kwa Nini hawapambani wao Kama wao. Wao wanasubiria kuwa empowered tu.
Katika majeshi yetu ke ni wa kutafuta na torch,
Pia kozi za Engineering,Md, architecture huko pia ni wa kutafuta kwa torch.
Sijapondea jinsia uelewe Ila mie navyojua mwanamke yupo chini ya mwanaume regardless what.
Why katika maandiko mwanaume ndiye anayepewa maagizo na Mwenyezi Mungu na si ke.
Bodaboda siwaoni ke,vibarua shambani ama kuzibua vyoo siwaoni pia huko Bali wao huwa nawaona wakitegemea nguvu ya k kuishi hapa sio wote.
NB: hayo maeneo niliyotaja wapo ke wenye uwezo kuliko me Ila ni %age ndogo Sana.
Chuoni kozi ya engineering Kuna wadada walikuwa na uwezo mpaka kwa department yetu best student ni ke akapewa scholarship amemaliza PhD yake USA.
 
Hahahaha mkuu umenikumbusha mbali Sana
Mimi nilivokua chuo wale washikaji waliokua wananifata kupiga misele kalibia wote walidisko ilifika hatua mtu akidisco wanauliza kwani ulikua na urafiki na buzitata?

Ila walichokua hawajui Mimi nasoma sehem zenye makelele na sio sehem iliyotulia so nlikua nikitaka kupiga msuli ni lazima nianzishe zogo darasan hapo ndo mambo yanapanda Ila wenzangu walikua hawajui kwamba hapo mm ndo mambo yanapanda kinoma.
Yaani wewe Ni Kama Mimi tu nilikiwa siwezi soma sehemu yenye utulivu [emoji1]

Yaani lazima nianzishe kelele huku naibia kwenye daftari ndio naelewa vizuri.

Kusoma sehemu iliyo kimya nakuwa naboreka
 
Mbona huwa siwaoni kwenye kazi ngumu Kama za zege,kuchimba hata mashimo ya vyoo,makondakta hawazidi labda 50 hapa mjini,madereva ni wa kuhesabu, hata wabunge ukiangalia wanawake wanabebwa viti maalumu tu ni kwa Nini hawapambani wao Kama wao. Wao wanasubiria kuwa empowered tu.
Katika majeshi yetu ke ni wa kutafuta na torch,
Pia kozi za Engineering,Md, architecture huko pia ni wa kutafuta kwa torch.
Sijapondea jinsia uelewe Ila mie navyojua mwanamke yupo chini ya mwanaume regardless what.
Why katika maandiko mwanaume ndiye anayepewa maagizo na Mwenyezi Mungu na si ke.
Bodaboda siwaoni ke,vibarua shambani ama kuzibua vyoo siwaoni pia huko Bali wao huwa nawaona wakitegemea nguvu ya k kuishi hapa sio wote.
NB: hayo maeneo niliyotaja wapo ke wenye uwezo kuliko me Ila ni %age ndogo Sana.
Chuoni kozi ya engineering Kuna wadada walikuwa na uwezo mpaka kwa department yetu best student ni ke akapewa scholarship amemaliza PhD yake USA.
Linapokuja suala la ndoa na kazi ngumu kweli Mwanaume yuko juu ama zaidi ya Mwanamke

ila kazi zisizohitaji nguvu usijidanganye
Chunga mtizamo wako...

ama unatuaminisha pia wenye hela wote ni wanaume😅
 
Linapokuja suala la ndoa na kazi ngumu kweli Mwanaume yuko juu ama zaidi ya Mwanamke

ila kazi zisizohitaji nguvu usijidanganye
Chunga mtizamo wako...

ama unatuaminisha pia wenye hela wote ni wanaume😅
Kama wenye hela hebu tuanze kuangalia matajiri Billionaires in terms of usd Kama alfu 10 afu ratio Kati ya ke/me ni ngapi. Ama tuanzie Mia moja najua hii itapatikana hata Kama tukigugo.
Tuachane waliyopewa talaka na utajiri wakaupata kwa wanawake.Tuone waliohaso from zero kabisa na sio kurithi ni wangapi
 
Billionaires mbali sana
Maisha ya kawaida tu wenye hela wote ni Wanaume?
Wenye magari wote ni wanaume?.
Viongozi wote ni wanaume?

sikatai tofauti za kijinsia ila haimaanishi mara zote mwanaume yuko juu ya mwanamke kama ulivyosema
Hasa katika muktadha nje ya mambo ya ndoa
 
Namie sijakukatalia naelewa hata vitani Kuna wanawake wana uwezo mkubwa Sana wa kuongoza mapambano kuliko wanaume. Ila inatokea tu Kama accident my dia ama bado sijaeleweka.
Pia wanawake wanaohaso kabisa from zero wakasimama ni wachache ilo tuelewane bila ya mkono wa mwanaume.
Kama hajatoa k ili apewe nafasi Fulani kikazi.
Pia sikatai kuwa wanawake hawana uwezo.
Mfano mzuri kwetu home mama alikuwa na nguvu za kulima shambani kuliko baba.
Yaani mama Ana nguvu from Ile akiwa mdogo ndo Bibi alimpendea akadai kuwa anafaa kuwa mkamwana wake.
Ila inabidi ukubali ukweli basi.
 
Nafikiri tuishie hapa mana tuna mtizamo tofauti
 
Kweli kabisa usimdharau mtu usiye mjua.

Hata mm imenitokea hiyo kuna Mkaka mmoja mtaan kwetu ukweli sikuwahi kumuelewa kabisa. Kwanza nilikuwa namuona kama hajatimia kuitwa wa kiume kwa njisi tu alivyo alivyo. Hata salamu tulikuwa hatuna.

Kuna siku moja nilikuwa nimekaa nje kwetu na shoga angu akapita huyu kaka. Nikajikuta namwambia best yng "yaani katika watu nisiowaelewa hapa duniani huyu kaka wa kwanza. " akaniuliza kwa nini, nikamwambia basi tu simuelewi katika kila kitu.

Zikapita siku za kutosha. Siku moja nimetoka zangu mishe najiandaa kuingia bafuni mara shoga angu huyoo ananiita. Nikamwambia nisubiri ndani nakuja. Niliporudi ile naingia tu kuniona akaanza kucheka hatari. namuuliza wacheka nini wewe. akajibu yule kaka usiyemuelewa hapa duniani kanipa zawadi hii nikuletee. Anaomba kukutana na ww. Looh nikamwambia muongo ww naanzaje kwenda kumsikiliza na kwa nn umepokea zawadi hii ikiwa unajua kila kitu. akasema ndio hivyo nenda ukamsikilize uku anacheka hatari.

Kweli sikwenda siku hiyo. Ilipita kama wiki mbili hivi akuacha kunitumia zawadi. Ile kitu ikanifanya niwe namfikiria sana. Nikampa nafasi nikaenda kumsikiliza. Akamwaga sera zake pale nikazipokea taratibu nikaanza nikazifanyia kazi. Nakumbuka kauli yake ya kwanza alisema "Nakupenda, sitaki kujua kuhusu mahusiano yako uliyonayo ingawa ninchojua mm hujaolewa, so nipe nafasi alafu utachagua ww yupi anakufaa." Hakuwa na mengi

Looh mpaka leo siamini nimezama mwenzenu. Alivyo kwa nje na ndani tofauti kabisa. Na sasa ndoa imetangazwa.
Kweli usimdharau mtu usiye mjua
😄😄😄
 
Hii siledi nayo ni miongoni mwa siledi duu[emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my cupboard using mug
 
Ndevu na nywele zangu hazinaga ushirikianao, hivyo nywele huwa nanyoa kila wiki zikae size ya chini kabisa, ndevu naziacha lakini ziko kidevuni tu nazo hata niziache miezi hazizidi kimo flani.

Nilimsikia F.a anasema alianza kuwa na mwili alipoanza kwenda ym ili awe anakula sana, namimi nina mpango huo maana mwili hauna shukrani huu.
Fanya hivyo mkuu!! Ukifika gym ,train kama vile unataka kuwa bodybuilder yani ile serious usiafanye mazoezi dk15 na dk15 nyingine selfi na kuchat kama washua wenzako wanavyofanya... achana na aerobics, miezi mitatu tu tunakusahau!!!
 
Mm miaka hii nimeanzisha michezo ya kizungu. Nikiwa na mihadi na mtu nionane nae namuelekeza aje sehemu ya kulia chakula hotel kubwa kubwa nikifika kule naagiza kisosi kidogo cha mboga za majani au kikombe cha maziwa na yai moja la kuchemsha hapo najua hata 10K haifiki. Mda huo chai inachemka nachukua sim naanza kuchambua timu za kubet huku namsubiri best yangu aje. Basi wahudumu wanajuaga huyu jamaa mnyamwezi au kaishi sana mbele, kumbe nawaangalia wazungu Instagram alafu naigiza.
You never know mkuu siku unaweza ukaokota dodo huko maisha yakabadilika ghafla😃😃😃
 
Tuna tofauti kijinsia
Ila katika eneo la kazi ama elimu haimaanishi mwanamke an saa uwezo wa chini

Mh Rais ni Mama Yetu Mpendwa SASHA🥰
Mama samia i really love that mama,,
Leo namuona anaingia zeke ikulu na msafara wake anaperuz peruz jamii forum nyuma gari,
Hana habari so relaxed,.
Mbele waheshmiwa ma rto na zto wanaongoza msafara,
MUNGU AMPE MAISHA MAREFU SANA MAMA ETU,
Nikimuonaga moyo wangu unapata amani sana nasahau shida zangu zote kwa muda..
 
Mhhh umetia chumvi hapo kwenye kuperuzi JF
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.

Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nilipigilia kipensi changu na ka t-shirt flan hivi local nikachagua sehem nikakaa, kutizama vizuri nikaona kuna meza amekaa mdada mmoja hivi and of coz she is gud looking nikaamua kujitosa angalau kumpa hata hi 'coz tulikuwa wateja 2 tu, nikamfata nikamsalimu.

Yule dada kwanza alinishusha kuanzia juu mpaka chini then akaitikia salamu yangu ki-design kama namsumbua flani hivi. Nikaomba kujumuika nae kama asipojali. Jibu lake ndo lilinitoa confidence kabsa, alinambia: "Kwahiyo kaka unadhani kila msichana akikaa peke yake anahitaji kampani? Hapana sihitaji" Dah, mwanamme nikajizoazoa pale nikarudi nilipokaa. Nilikaa kama masaa ma3 hivi nikaamsha zangu. Sasa kilichotokea jana ndo kimenifanya niandike huu uzi.

Nilipokea maagizo kuanzia J3 ya wiki hii kuwa leo watakuja watu wa Taasisi flani ya kifedha kutoa semina kwa sisi wafanyakazi kwa ajili ya kutushawishi kujiunga na huduma za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.

Asubuhi mida kama ya saa 3 hv ugeni ukafika, walikuwa watu kama 7 hivi, kati yao alikuwepo yule dada nilieonana naye weekend.

Wakaingia ofisini nikawakaribisha, wakati mkubwa wao anatoa introduction macho nikayakaza kwa yule dada, bahati nzuri tukagonganisha macho, akashtuka flani, nikajua kashanikumbuka.

Baada ya semina kuisha ikafika kipindi cha watu kujiunga sasa kwa walioshawishika. Nikamfata yule dada nikamuomba aje anielekeze namna ya ujazaji fomu. Alivyofika tu, nikamuuliza "Unanikumbuka?" Akachekaaa, akaniambia "Yani wewe, sikutarajia kama unaweza kuwa unafanya kazi huku", nikamuuliza ulitarajia niwe nafanya kazi wapi? Akaishia kucheka tu. Mawasiliano yake kanipa; fresh bila shida kabisa.

Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?
Hao ndo wazuri, ipige iyo sana tu sio mara 2 tu alafu itose
 
Back
Top Bottom