Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Napenda sana sana kupikapika na nipo vizuri kiasi sekta hiyo. Mama yangu anapika sana so alianza kunifundisha toka nipo mdogo sana.
My dream siku moja niwe na catering service yangu kubwa sana.
Pambania ndoto yako utafanikiwa wateja tupo humu
 
Emotional maturity yako ipo juu sana.
 
W
wewe ni popoma haswa yani hukumla?
 
SASA ruge ana mwili mdogo?
 
SASA ruge ana mwili mdogo?
Yah alikuwa na mwili mdogo. Hata yeye aliwahi kuweka wazi kwenye interview moja kuwa watu wengi ambao hawakuwahi kukutana naye walikuwa wakikutana naye na kujua yeye ndiye ruge walikuwa wanamshangaa kwa sababu ya mwili wake.
By the way sasa hivi nimeongezeka sana hadi natamani kupungua tena. Mwili mdogo kumbe una raha yake aisee. Sasa nachoka hovyo
 
Siku moja tumekaa pale morogoro round about Stendi ya viahice kwà fundi viatu anaitwa shomari. Wamekaa watu wengi kwenye mabenchi tunapiga stori sasa tulikuwa tumekaa na jenerali mstahafu wa jwtz akiwa amepaki gari yake kwenye kituo cha mafuta pale round about sass wakaja watu wa wrong parking wakalitia mnyororo lile gari. Bila kujua ni lanani yule jenerali akamtuma kijana mmoja mchoma mihogo akamwambia akawaambie wale jamaa wa wrong parking wafungue gari yake. Jamaa wakakataa. Jenerali akapiga simu kwà mkuu wa mkoa duuu dakika sifuri ffu hawa hapa tukashangaa jamaa wa wrong parking ndio wako juu ya karandinga wanaenda mahabusu.
 
[emoji23]Hawa jamaa wa wrong parking wanajifanyaga hawaelewagi ,wao Kila gari wanaitia Pini ,Sasa nadhani watajifunza kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hizo huwa nakutana nazo sana na imefika kipindi sasa nimezoea na pia nachukulia kama advantages yakuweza kusikia hata watu wanakuongea bila kujua kuwa ni wewe.

Hii imetokana na asset nazomiliki haziendani sana na muonekano wangu kwamaana hiyo Kuna kipindi nanunua viwanja nakuwa nimeshafika site ila bado unakuta muuzaji ananisubiri huku ananisema kuwa boss wenyewe hajali muda bila kujua ndie mimi.

Moja Kali nayokumbuka nilikuwa kwenye ujenz wa nyumba yangu yakuishi sasa kipindi nanunua mtendaji hakuwepo japo muhuli wake ulitumika kwa niaba, sasa nimeanza ujenzi nikawa nimemtoa mwenyekiti kidogo Ili anisimamie mambo ya kibali Cha ujenz kama mnavyojua ujenz wa dar unamambo mengi, basi nipo na mafundi nimejichanganya mara naona jopo la watu limenituzunguka wanataka mwenye nyumba yupo wapi, mafundi wakasema ongeeni na huyo wakanioneshea mm , nikamsogelea dada habari yako akajibu ahaa Mimi sitaki msimamizi nataka mwenye nyumba Yani anayejenga maana huyu atanielewa nn?

[emoji23]
Mafundi wakacheka huku wanasubiri kitatokea nn[emoji23]. Nikauliza sasa kama msimamizi maana kwaakuwa kaamua kunichukulia hivyo basi nikavaa huo uhusika, kwani dada Kuna shida gani? Akaanza nyie mnakibali au unakuja kusimamia vitu hujui kitu, kwanza taarifa yenu Sina kbsa asee taarifa ya huu ujenzi naamuru usimame mpigie boss wako, mwambie mtendaji kasimamisha ujenzi mpaka mpate kibali. Bahati yake site for men akatokea akamuita kwa jina we Fulani vipi hapo mbona mnaongea na boss wangu kwa ukali? Akabaki kamtolea macho kwa mshangao, akajikaza akasema namtaka mwenye nyumba. Jamaa akamjibu si huyo hapo ukonae [emoji23]

Nikabaki natabasam tu yy macho yamemtoka maana mjengo si haba ikambidi avunge, haijalishi anakibali sasa kwa sauti ya chini sasa [emoji23], jamaa akamwambia kamuulize mwenyekiti wako huyo kashamaliza Kila kitu. Daaaah akalowa eh basi kaka karibu sana tutasaidia kwenye mambo ya maendeleo mm huwa sipingi maendeleo ni utaratibu tu jamani, nikamuangalia tu akajizoazoa akasepa ikabaki gumzo tu pale aasee.
 
Uyo mpige🥒 Kisha tembea
 
Ph.D hapana mkuu bado na sina mpango kwa sasa . Nimeshakuwa na familia sasa hivi hata kusoma sitaweza mambo mengi sana. Labda miaka miiingi mbeleni kama Mungu atatupa uhai.
Hii nchi ina uhitaji wa Ph.D katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma na kitafiti katika taasisi nyingi.
Hivyo angalia uwezekano wa kufanya jambo juu ya hilo pindi upatapo nafasi mkuu.
 
Kila siku tunakutana na makubwa zaidi ya hayo. Tena kwa sisi tunaojua kujifanya punda maji tunawashangaza watu mara nyingi na tunaonbwa msamaha sana na watu. Ni ujinga kujaji mtu kwa mavazi au sura.
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…