Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Juzi juzi nilienda kumlipa Binti yangu ada kwenye shule fulani ya watoto wa kike kufika office ya Mhasibu nikamkuta mama flani namslimia akanishusha tu akaendelea na mambo yake. Nikamsalimia mara ya pili ndo akanijibu "nimeshakusikia" nikaamua kusubiri alipomaliza mambo yake ndo akaniita "haya unasemaje?" Nikamwambia nimekuja kumlipia ada ya Binti yangu anayesoma hapa
Akashtuka "ooh kumbe sikujua"
Nikatoa bank slip ya 3.5m ambayo ni ada ya mwaka mzima Pamoja na slip ya pili yenye laki 5 ya michango
Alipoona hivyo akaanza kujichekesha mpk akawaagiza wanafunzi wamwite Binti yangu amsalimie .
Aahh.. wanadamu tuna shida sana [emoji38][emoji38][emoji38]wanapima Kwa macho

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Miaka fulani nilikuwa na likizo ndefu ya chuo basi nikaona nisikae bure nikafungua kamgahawa katikati ya mji. Nilikuwa nauza bites zote, juice fresh na matunda fresh.

Nilikuwa karibu na ofisi nyingi na banks. Basi nikawa napata oda ya kupeleka bites na maziwa asubuhi pamoja na matunda.

Dada mmoja staff wa pale CRBD aliweka oda ya matunda kila ikifika saa 6 mchana, ikawa siku nyingine ukipeleka anakwambia umechelewa nishakula kwingine, au leo sili basi narudi nayo. Au ukienda siku nyingine anakuangalia tuu hapokei matunda unabaki umesimama kama sanamu na matunda yako.

Siku moja nikaenda nikiwa na shida ya kufungua joint acc, kufika kwake hata sijamsalimia kanijibu leo sitaki matunda. Nikamwambia nina shida nyingine kabla sijaeleza akajibu tena "hapa tunasikiliza za kiofisi tuu hivyo ondoka". Sijui alijua nataka msaada wa hela au vipi.

Ikabidi niwe mpole maana alikuwa peke yake kwa muda ule customer service pale. Nikamweleza nahitaji fomu kufungua joint acc na mama yangu. Akachukua fomu akanipa akaniuliza "utaweza kusoma na kuzijaza kweli na mama yako??" Nikamjibu ndio. Akaniambia viambatanisho vinavyohitajika nikaondoka kesho nirudishe fomu.

Kesho yake nimeenda na mama, kufika pale akamkaribisha akakae kwenye kiti mimi akaniambia kasubiri pale yaani pembeni, ndio mama akamwambia nimekuja na binti yangu tunafungua joint acc, kwanza alistuka akamuuliza ni mwanao kumbe mama sikujua. Akaishiwa pozi.

Basi katika kupiga stori na bimkubwa akamwambia sikujua kama una binti mkubwa, bimkubwa akamwambia mara nyingi hayupo nyumbani kwasasa yupo likizo anasoma masters huko mkoa X. Alishangaa kwa nguvu Masters?? Aliniangalia sana. Miaka hiyo bimkubwa na mzee walikuwa wafanyabiashara wakubwa sana mkoani na chapaa zipo za kutosha wanajulikana kila kona. Bank pale walikuwa wanajulikana sana.

Dada alikosa raha sana hadi muda anatoa copies akaniambia dada kakae kwenye kiti [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] toka siku hiyo alianza na kunisalimia na kunichangamkia. Mimi wala sikumwonyesha tofauti nikaendelea kumpelekea matunda.
Daahh...aseehhh[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka siku nareport shule kuanza 4m 5, sasa kufika pale ofisin kwa makamu wa shule kufanya usajiri,
Ile alivoniona akakaa kimya km dakika 10 anantazama tu, baadae akaniuliza full details zangu nkatoa kumpa (result slip na leaving) plus resit za michango mbalimbali.

Then akaangalia kweny file la selection alipoliona jina langu alishtuka na kuhamaki mno, akasema "ulivyo hufanani na kusoma tahasusi hii, tena kwa shule km hii, na matokeo yako ya 4m 4 na shule uliyotoka hufanani nayo" kiukweli nilijskia vibaya sanam

Ila still maisha yaliendelea hadi nikahitimu, siku nimeenda pale kuchukua results slip na leaving, ndo akanambia kuwa alivyokua anadhani sivyo na alivotegemea wala kuwepo.

Mie huyo nikasepa zangu.
🤯🤯🤯

Mchezea akili za watu 🤣
 
It was a suprise kwangu.

Jirani yangu aliekuwa anajifanya ni boss wa Ikulu mtaani muda wote kanuna na miwani yake mieusi alikuja kunihudumia Chai Ofisini kwa Mama Salma Kikwete wakati wa WAMA, kumbe Alikuwa Office attendant pale tena wale wa oya oya na mie na wenzangu tulienda kupeleka project paper ya ki NGO chetu ambacho ni Hayati kwa sasa kuanzia 2015.
Hicho ki NGO mzilankende myao alikipiga pini Nini!!?maana jamaa alizika Hadi vyuo vikuu uchwara!!
 
Mie ni tofauti kidogo , tulikuwa safari ya mkoa basi likaharibika njiani , wakati wanatatua tatizo abiria mmoja akashauri kitu Fulani akward dizaini za kuwa harrass wenye basi .nikampinga kibabe na kupata support kutoka kwa abiria wenzangu
Kesho yake nimefika kwa ajili ya mishe kumbe jamaa niliyejibishana naye Jana yake safarin ndio top wa ofisi niliyoifungia safari ., Ila hakuwa na kinyongo alifanikisha mission yangu
[emoji1787][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi uzuri nina adabu simdharau mtu kwakweli ila kuna Mtu aliwahi kuvuka matarajio yangu yani sikutegemea.

Maana jamaa alitaka nikamfanyie kazi fulani akanambia niandike namba atanicheki anatumia Tecno S series[emoji23] nikadharau nikajisemea huyu nae nani[emoji1787], siku ya kazi kaja kunichukua Offisini na Range rover sport anaishi Cliffside resiidence toure dr hakuna kazi nililipwa kama hio mtu unafanya kazi huku unakunywa Moet Chandon Shampaigne.
[emoji1787][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huwezi nilazimisha nikusalimie wakati wa kupokea huduma. Sio lazima kabisa wala haiongezi au kupunguza chochote.
Nikija customer care nahitaji huduma, salamu naweza enda shule ya msingi wakanisalimia watu zaidi ya 1000 na shida yangu isitatuliwe.
[emoji1][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]daahh watu mna majibu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Miaka fulani nilikuwa na likizo ndefu ya chuo basi nikaona nisikae bure nikafungua kamgahawa katikati ya mji. Nilikuwa nauza bites zote, juice fresh na matunda fresh.

Nilikuwa karibu na ofisi nyingi na banks. Basi nikawa napata oda ya kupeleka bites na maziwa asubuhi pamoja na matunda.

Dada mmoja staff wa pale CRBD aliweka oda ya matunda kila ikifika saa 6 mchana, ikawa siku nyingine ukipeleka anakwambia umechelewa nishakula kwingine, au leo sili basi narudi nayo. Au ukienda siku nyingine anakuangalia tuu hapokei matunda unabaki umesimama kama sanamu na matunda yako.

Siku moja nikaenda nikiwa na shida ya kufungua joint acc, kufika kwake hata sijamsalimia kanijibu leo sitaki matunda. Nikamwambia nina shida nyingine kabla sijaeleza akajibu tena "hapa tunasikiliza za kiofisi tuu hivyo ondoka". Sijui alijua nataka msaada wa hela au vipi.

Ikabidi niwe mpole maana alikuwa peke yake kwa muda ule customer service pale. Nikamweleza nahitaji fomu kufungua joint acc na mama yangu. Akachukua fomu akanipa akaniuliza "utaweza kusoma na kuzijaza kweli na mama yako??" Nikamjibu ndio. Akaniambia viambatanisho vinavyohitajika nikaondoka kesho nirudishe fomu.

Kesho yake nimeenda na mama, kufika pale akamkaribisha akakae kwenye kiti mimi akaniambia kasubiri pale yaani pembeni, ndio mama akamwambia nimekuja na binti yangu tunafungua joint acc, kwanza alistuka akamuuliza ni mwanao kumbe mama sikujua. Akaishiwa pozi.

Basi katika kupiga stori na bimkubwa akamwambia sikujua kama una binti mkubwa, bimkubwa akamwambia mara nyingi hayupo nyumbani kwasasa yupo likizo anasoma masters huko mkoa X. Alishangaa kwa nguvu Masters?? Aliniangalia sana. Miaka hiyo bimkubwa na mzee walikuwa wafanyabiashara wakubwa sana mkoani na chapaa zipo za kutosha wanajulikana kila kona. Bank pale walikuwa wanajulikana sana.

Dada alikosa raha sana hadi muda anatoa copies akaniambia dada kakae kwenye kiti [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] toka siku hiyo alianza na kunisalimia na kunichangamkia. Mimi wala sikumwonyesha tofauti nikaendelea kumpelekea matunda.
Hilo tunda ningelila kimasihara [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] umenichekesha sana

Eti nilikuwa nampelekea matunda [emoji527]
 
Mimi hizo huwa nakutana nazo sana na imefika kipindi sasa nimezoea na pia nachukulia kama advantages yakuweza kusikia hata watu wanakuongea bila kujua kuwa ni wewe.
Hii imetokana na asset nazomiliki haziendani sana na muonekano wangu kwamaana hiyo Kuna kipindi nanunua viwanja nakuwa nimeshafika site ila bado unakuta muuzaji ananisubiri huku ananisema kuwa boss wenyewe hajali muda bila kujua ndie mimi.
Moja Kali nayokumbuka nilikuwa kwenye ujenz wa nyumba yangu yakuishi sasa kipindi nanunua mtendaji hakuwepo japo muhuli wake ulitumika kwa niaba, sasa nimeanza ujenzi nikawa nimemtoa mwenyekiti kidogo Ili anisimamie mambo ya kibali Cha ujenz kama mnavyojua ujenz wa dar unamambo mengi, basi nipo na mafundi nimejichanganya mara naona jopo la watu limenituzunguka wanataka mwenye nyumba yupo wapi, mafundi wakasema ongeeni na huyo wakanioneshea mm , nikamsogelea dada habari yako akajibu ahaa Mimi sitaki msimamizi nataka mwenye nyumba Yani anayejenga maana huyu atanielewa nn? [emoji23]
Mafundi wakacheka huku wanasubiri kitatokea nn[emoji23]. Nikauliza sasa kama msimamizi maana kwaakuwa kaamua kunichukulia hivyo basi nikavaa huo uhusika, kwani dada Kuna shida gani? Akaanza nyie mnakibali au unakuja kusimamia vitu hujui kitu, kwanza taarifa yenu Sina kbsa asee taarifa ya huu ujenzi naamuru usimame mpigie boss wako, mwambie mtendaji kasimamisha ujenzi mpaka mpate kibali. Bahati yake site for men akatokea akamuita kwa jina we Fulani vipi hapo mbona mnaongea na boss wangu kwa ukali? Akabaki kamtolea macho kwa mshangao, akajikaza akasema namtaka mwenye nyumba. Jamaa akamjibu si huyo hapo ukonae [emoji23]
Nikabaki natabasam tu yy macho yamemtoka maana mjengo si haba ikambidi avunge, haijalishi anakibali sasa kwa sauti ya chini sasa [emoji23], jamaa akamwambia kamuulize mwenyekiti wako huyo kashamaliza Kila kitu. Daaaah akalowa eh basi kaka karibu sana tutasaidia kwenye mambo ya maendeleo mm huwa sipingi maendeleo ni utaratibu tu jamani, nikamuangalia tu akajizoazoa akasepa ikabaki gumzo tu pale aasee.
Likewise
 
Hii ilitokea kuwa nilipata ugeni juu ya ugeni kama ifuatavyo.
Rafiki yangu toka Nairobi alinitembelea na yeye alitegemea kukutana na rafiki yake Mtanzania lkn huyo rafiki yake anaishi Us.

Basi huyu rafiki yangu huyu wa Nairobi akaomba kama sitojali awakaribishe hao wageni wake kwangu na walale siku moja ili wapate wasaa mzuri kuongea usiku.
Nami sikuweka pingamizi kwani nina nafasi ya kutosha nyumbani.

Wale wageni wakati wanakuja walipiga simu na kumwelekeza dereva aliyekuwa anawaleta.
Nilienda kuwapokea kwenye njia panda kuja kwangu.

Nilipowapokea na kuwaleta home, walipokutana na mwenyeji wao na kukumbatiana kwa bashasha..jamaa huyu Mtz mkazi wa Us kwa muda huo walikuja na mkewe..na hapa Tz ni wenyeji wa Kigoma.

Basi niliwakaribisha na kuwapa juisi na wakaendelea kuongea kwa muda kama dakika 30.

Huyu jamaa Mtz mkazi wa Us ilibidi amuulize huyu rafiki yangu kuwa mwenye nyumba yuko wapi tumsalimie?

Rafiki yangu akaniita kwani baada ya kuwapatia juisi mimi niliwapisha sebuleni niliingia kwenye ka ofisi changu kadogo.

Hivyo rafiki yangu akaniita kuwa nije wageni wanatamani kunisalimia, baada ya kufika jamaa huyu Mtz akauliza....una uhakika ndiye mwenye nyumba?
RAfiki yangu akamjibu ndiye...
Jamaa alishangaa sana akasema nilijua labda ni kijana wa mwenye nyumba.
 
S
Hii imekaa kama kilimo cha matikiti tumeona faida tu bila changamoto na hasara.

Ujaeleza chuo ulipata mkopoa ua hukupata, ujaeleza mbilinge za Lecture Sup, Carry nk

Ujaeleza msoto wa ajira na michakato mingine.

Ujaeleza Intiview ulizogonga kutoka kazi moja hadi nyengine.

Vizurungu vya michepuko, muda wa kula tujaona au ulikuwa auli, muda wa kwenda Toilet, muda wa kulala, kucheki Movie nk.

Yaani wewe ujaonesha kuna siku ulipoteza nauri 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Unataka atunge kitabu sasa cha maisha yake,
 
Back
Top Bottom