Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

16 twende
 
S3 epi 16



Tukazuga pale tukaaga tukaondoka, hapo kumbuka mama mkwe tangia tufike zaidi ya salamu hajatia neno, basi pale nikaona hapa kazi ipo, ba mdogo nae analalamika Hawa wazee mbona siwaelei nikamwambia Mzee hii ishu tushaianza wote usijifanye kama haikuhusu, ingekua kazi rahisi ungedhani nilishindwa nini kuimaliza mpaka nikakuita wewe uje huku



Nikampigia Simu G tukakutana mahali hapo tupo na ba mdogo tumekaa mahali tu, nikamuelezea yaliojiri akawa ananiambia naomba Sana haya mambo yaishe salama Nije tu kukaa kwangu..... Hapo Sasa ndo akili yangu inakuja kwamba kumbe baada ya Hili sakata Kuna kupewa huyu Binti tena, hapo namuuliza na kazini Sasa vipi huendi, akaniambia hapana mi siwezi tena akili haipo sawa mpaka nijue mwisho wa hili jambo ni nini, sawa tukakaa pale badae G akaaga akaondoka, ba mdogo nae hua hayupo serious kabisa, hapo tuna majanga ye akaanza matani " Mzee hapa upo sawa kabisa, huyu mtoto hata pesa zetu tutatoa Kwa halali kabisa"


Nikawa nashukuru tu at least nipo na mtu anajua nayopitia tunaweza hata kushauriana, ba mdogo hapo tushatiana kiburi kua Hawa wazee tuachane nao kwanza maana tushaambiwa kule wao hawana Mamlaka yoyote, na kama Hilo tambiko sijui Hela tulishawapa ni kama wanatafuta namna ya kufanya hili jambo liwe fursa kwao



Basi zinapita siku, wazee wanapiga Simu sisi tupo kimya tu hapo nawaza Hawa watakua na plan gani mbona walishatupa vitisho vingi, Rachel nae alisharudi geita nilifanya kuambiwa mtoto akawa kamucha pale kwao, G Bado yupo Kwa shangazi huko..... Kuna siku nikapigiwa namba mpya kumbe ni yule mama Sasa wa Ile siku mwenye nyumba akawa ananiambia mkipata wakati mnijulishe ni lini mje nyumbani tuongee.... Nikamwambia sawa ntakujulisha...... Hio siku nimekaa pale mara napigiwa Simu na mkuu wangu kazini, Sasa nikawa nawaza huyu anataka nini ila sikushangaa Sana maana Kuna kipindi unakuta upo likizo unapigiwa tu Simu unakuta mtu uliyemuachia nafasi Kuna maelezo anataka kutoka kwako..... Sasa napokea tumepena salamu pale na nini, anaanza kuniuliza " hivi policy za kazi si mnazijua wote, mambo yenu private ni marufuku kufika kazini"



Namuambia Hilo nalielewa, maana kweli kazini kulikua na policy za kijinga kweli mambo Yako ya nyumbani ukileta kazini wanakua na zogo kweli, Kuna kipindi Kuna mfanyakazi Ali apply zile emergency Loan akaandika anahitaji ada Kwa ajili ya watoto wake, yaani alichambwa ofisi nzima mpaka ikawa aibu, Hawa wajinga shida za nyumbani ukiondoa maradhi au kifo walikua hawataki kuskia



Sasa kumbe wale wazee wameenda pale ofisini napofanya kazi, aliyewaelekeza huko hata sielewi ni nani, nikashangaa kwanza nikaona mpaka Sasa Hawa wamefika mbali, uzuri tu pale ofisini mkuu akawasikiliza akawaambia mbona hapa naona ni mambo private sielewi sisi tunahusika vipi, mtafuteni muongee kifamilia, Sasa hapa nao washanitia dosari kazini, na ukizingatia hii ishu sikuwahi kumuambia mtu



Ba mdogo Sasa namuuliza Hawa wazee tunadeal nao vipi maana naona Sasa tunatiana aibu tu Sasa na ukizingatia swala la kuongea nao tena tushaliweka pembeni, ba mdogo ananiambia waache kwanza hao tutajua namna ya ku deal nao



Ikafika siku tukaja kwenda Kwa mama mkwe kule, same routine... Tukafikia Kwa yule mama hio siku yupo tu yule mama na mama mkwe hapo nipo na ba mdogo, mama mkwe kama kawaida baada ya salamu yeye yupo kimya tu, yule mama Sasa ndo muongeaji, akaniambia "mwanangu hapa sitaki mambo yawe mengi Wala nini ndo maana hata unaona tupo wenyewe tu hatukutaka watu wengi maana haya mambo yashakua ya aibu, huyu ashakua mama Yako inabidi ifike mahali tu msameheane maisha yaendelee, hapa sisi Wala hatuwezi hata kuanza kukaa vikao vya kupigana faini Wala nini, wewe ni mtu mzima Wala sio mtoto nendeni tu mjipange mje na chochote sisi tutapokea Kwa mikono miwili, Ili huyu(G) awe amepata baraka za mzazi Sasa, hapo ba mdogo nae akadakia akajifany anaongea maneno yake ya busara pale mimi hapo nipo kimya tu naitikia tu..... Tukaongea pale tukawa tumemaliza





Sasa Mila za huku Kanda ya ziwa Kuna muda hua sizielewi, kuna kitu kinaitwa nzengo, Hawa ni majirani wote ambao mnakua mnaishi mtaa Mmoja, omba Sana kugombana na mtu yoyote ila sio Hawa watu, nilishazoea tu kuhudhuria matukio mbalimbali ya mtaani pamoja na kutoa michango pale panapohitajika, sasa hio siku napigiwa Simu nifike Kwa Mzee mmoja ni karibu ninapoishi, tukatoka hapo nipo na ba mdogo, Sasa Ile kufika hio nyumba nashangaa tena nakutana na lile jopo la wazee...... Nikabaki nashangaa Hawa wananitafuta nini
 
B
Ba mdogo analeta udaresalam mikoani
 
Wazee wa fursa wamekuganda sana utakoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…