Hope urassa
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 4,230
- 10,650
Oh dah
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba utag huo uziKuna ule uzi wa kulinda vitu upitie, kuna point niliipata kule, kwamba kitu kigumu siyo kupata ila kulinda... Yaaani kupata laki siyo tatizo kuilinda ubaki nayo ndo kazi ...
Usiachie kirahisi kitu ambacho umekipata eti kisa kuna kamtu kanaleta zogo, panda naye juu mpaka haki yako ibaki...
Au tu uwe karibu yangu niwe nakufundisha mara kwa mara [emoji23][emoji23]
Eti kuwa na wewe mwanangu utakuja kuyapitia tu[emoji28][emoji28][emoji28]Season finale
Jasiri haachi asili, nipo zangu njiani hapo Nina happy pill Moja kichwani na mzigo nimeubeba kwenye gari, Sina plan yoyote nikifika Sasa nafanyaje huku naondoka tu maana sielewi naona Kila siku Kuna jambo halipo sawa, nikiwa njiani jirani anapiga hapo naanza kudebate kichwani nipokee au nisipokee, badae napokea anauliza uko wapi namwambia nimesafiri mara Moja, basi anaanza kujielezea pale na nini mi namsikiza tu, anasema kwanza huyu mwanaume tume break up siwezi kua na mtu ananifatilia fatilia ivi, kichwani nawaza Sasa huyu nae mtu anakulipia apartment na bills zako hutaki akifatilie, stupid!!! Nikamwambia jirani badae basi tutaongea......
Mungu ni mwema nimefika salama pale napokelewa na mama na familia pale, Kuna vitu niliwachukulia nikavishusha pale basi wakawa na furaha, G nae hapo ndo ukweni mavazi ya heshima kweli anavaa nikawa nacheka tu moyoni nasema kweliii..... Tukaongea ongea tu pale na mama, nikakaa na watoto pale badae nikatoka nikaenda mtaani catch up na washkaji wa mtaani pale muda ukawa ushaenda nikarudi home tu pale, nafika nikala nikaenda kulala, G nae Sasa hapo akaanza kuniomba msamaha kaondoka hajaaga nikamwambia usijali tutayaongea tu haya.... Kesho yake imefika naona dogo wanamuandaa anaenda shule na uniform anazo kabisa nikasema hee huyu tena hawakuniambia hata anasoma shule gani sa ivi, likapita gari la shule akaondoka,nimezuga zuga pale naona pametulia tu mimi huyo nikatoka zangu
Nimekaa kidogo mama huku anapiga vipi uko wapi Sasa Kuna mtu amekuja hapa tuanze kukusaidia na we haupo, Sasa hapo nawaza nikawa sielewi, mama ni mtu flani wa dini kiasi, nawaza Sasa kama ni mganga sijui ndo kaamua kumleta nyumbani? Tangia mimi Nakua sijawahi hata kuskia anaongelea mambo hayo imekuaje tena, anyway nikasema watu wazima Wana Siri zao huwezi Jua acha niende tuone inakuaje......
Mimi huyo mpaka home, nafika kwanza nikawa sielewi, kumbe bana mama Kuna kikundi kanisani Chao Cha maombi, yaani kiufupi kimehamia nyumbani pale, kwaya zinapigwa pale watu wengi kama nini Kila mtu kashika biblia yake, kiufupi kanisa ni kama limehamia pale, nikasema eh Leo Sasa kazi ipo
Wasilimia pale, watu hawataki kupoteza muda, zikaanza nyimbo za kuabudu pale na nini, badae kijana wenu nikawekwa mtu kati pale aisee zilipigwa Sala acha kabisa, kama kuombewa aisee Ile siku niliombewa vibaya mno, badae nikaenda chumba nipo Sasa na huyu mkubwa wao wa maombi akaanza kunielezea Sasa mambo mengi kaonyeshwa sema ilikua general Sana hakua specific maana tu ananiambia Kuna mwanamke ulimuacha hajakubali ndo anapambana vita ya kiroho na wewe..... Nikaombewa tena pale, wakipumzika kidogo narudishwa tena mtu kati ni mwendo wa Sala tu yani....
Nikajua basi yameisha, aisee mwendo ukawa siku tatu wanakuja pale asubuhi wanaondoka jioni ni mwendo wa Sala tu kijana wenu nishapigishwa Toba kama zote yani, baada ya siku 3 naanza Sasa kuaga niwachukie tu familia yangu turudi Sasa mwanza maana na muda wa kazi unakaribia, ba mdogo ananipigia yupo njiani bi mkubwa alimlazimisha kuja tukae kikao Sasa, ba mdogo Kuja kufika ikabidi tukae kikao Sasa ila sister ye hayupo yupo mkoa mwingine kwake huko
Kikao kinaanza Sasa na G hapo kaitwa bila kumsahau mkubwa wa kile kikundi Cha maombi, mama akaanza kuelezea mambo mengi pale kuanzia alivyotulea na nini mpaka Mzee akapumzika, akaanza Sasa kusema nimemuita na baba Yako mdogo maana najua akili zenu nyie zinafanana hamchelewi kwenda kujazana ujinga wenu, mama akaniasa Sana kuhusu familia yangu pale na kuachana na mambo ya kijinga, nikifika mwanza nitafute kanisa permanent la kusali nimuanganishe sijui na huyo mchungaji na mambo mengi tu tukaongea pale....
Sasa inafika muda wanataka nimuombee G msamaha pale tusameheane mbele Yao nikaona huu Sasa ujinga, kama kawaida ba mdogo pale fasta akaangilia akawa anasema huyu(G) Sasa ndo anatakiwa kuomba msamaha pale aliondokaje bila kunipa taarifa, kama kawaida ba mdogo lazima atanisupport tu, basi yule Mzee pale akaingilia tukaongea yakaisha kawaida tu pale...... Kesho tukashinda pale kesho kutwa yake nikawachukua familia pale safari ikaanza.....
Hapo Sasa nimeacha mavitu yangu? Hapana!!! Ntajificha tu natumia ila nikawa nimejiahidi ntaachana nayo, tumefika mwanza hapo Sina kinyongo na G tumekua tu Sasa kama zamani walifika nyumba yenyewe Iko rough hapo ni kupambana na usafi tu, yule dada jirani nilikuja kumblock lakini nikawa najua G atapata ubuyu tu maana mtaani tena watu hawana dogo.....
Ikafika muda nikaenda kuripoti kazini, nikawa jumapili najitahidi tunaenda kusali na familia, hapo Nina Siri ya addiction yangu hata home ntajifungia kwenye gari ntatumia vitu vyangu basi sitaki mtu ajue, G ugomvi mkubwa Sasa ikawa ni swala la chakula, hapo Sina hamu nikawa kama mtoto Sasa muda wa kula ni vita basi sitaki kumkwaza najitahidi tu ivo ivo
Nimekaa kazini kama mwezi hivi Kuna siku nimeitwa kule Kwa mkurugenzi naenda namkuta yupo na bosi mwingine sehemu kitengo tofauti, kwanza akiniuliza uko sawa sa ivi namuambia tu nipo sawa Kwa Sasa, basi Kuna project Moja akawa anatuelezea pale na yule boss mwingine Sasa, badae akasema hii project nataka iende clean kabisa mpaka iishe, na Ina vishawishi vingi mnaweza kwenda kuhongwa huko mkaharibu hii kazi, akasema anatoa package ya marupurupu tofauti kabisa ya mshahara wala bonus za kazi, tukae tutafakari kama tutaweza ifanya, mtu akiona hawezi ni Bora aje aseme akawa ametupa siku 3
Milango ndo ikawa kama imefunguka Sasa ukiangalia hizo package nikasema huu mwaka wangu, Sasa kutoka ofisini pale yule boss akaanza kuniambia kijana huko ulipoenda ni hatari itabidi unipeleke aisee, namuuliza kwanini akasema hio Dili watu wamepambania Sana watu wametembea Sana Kwa watu wao inakuaje mimi natoka likizo tena ya probation nakuja kulipata kirahisi, basi mi namuambia hakuna kitu jamaa akawa hataki kabisa kuniamini....
Project ilikua kama miezi nane, hapo sisi ofisini tunakuja mara 2 tu Kwa wiki kutoa ripoti tena utawala kule sio hata kwenye department zetu, aisee hicho kipindi nilipata Sana Hela sidhani kama naweza kuja pata project kama Ile tena, maana tulifika kule tu siku ya kwanza wanaosimamia mradi wao yaani walituchana live kabisa kua hapa tukileta ujinga kwenye kuingiliana kimaslahi atakufa mtu, Kwa io kupiga deal hapa na lazima kama hutaki we Fanya kazi ila ukileta u snitch watu wako na wewe
Ofisini kule tunalipwa extra ili tusilete tamaa na huku mnapiga yaani Dili nzito nzito Kuna Hela unapewa mpaka unaogopa aisee, Kwa kifupi nilifanya Sana maendeleo ya kimaisha kipindi icho, nime struggle na addiction zangu Mungu akasaidia badae nikaacha zile pills Kwa shida ivo ivo na hayo ma tambuu, pariki mpaka na Leo mara Moja Moja Sana nikipata natumia....
Sasa na mimi kipindi icho Nakua busy na kazi alafu Wanawake nikawa nawaona kama downfall yangu tu najua nikianza mambo hayo tena ntaanguka shimoni, nipo na G wangu tu Raha Sana unaishi na mkeo kama mdogo wako, hua sijui hata maana ya kufokewa Wala kununiwa na mke naskia Kwa watu tu Mungu asaidie yasinikute..... G nae hata mtoto hajakaza kutembea mimba nyingine hio[emoji3], Mungu akaja saidia akajifungua mapacha, hapo Rachel alishaenda dar huko akaolewa nae akajifungua mtoto huko at least mapicha picha yakapungua......
Kazini mambo yakawa yanaenda sawa tu mpaka ma elite wale wanajifanya maboss tukaanza kupatana, maana sisi ndo " boots on the ground" Dili zote za kupiga Hela lazima zitapita kwetu tu ofisini huko zaidi ya kula ac utapiga deal gani Sasa, Kwa Io michongo yote ikawa inapitia kwetu tunakula nao wao wanatubeba kwenye ripoti tu....
G Sasa hivi kamekua kajanja kweli ana duka la accessories zote za watoto, nguo,toys,suppliments,viatu n.k( wateja mkaribie Sasa), mimi namshukuru Mungu kiasi chake kanifanyia mema mengi Sana, pombe Bado tunakula Kwa Kiasi chake, madhara makubwa niliyoyapata hayo mavitu yame suppress appetite yangu sana, sio mtu wa kula kabisa, alafu usingizi Sasa mi nikilala masaa matatu yananitosha kabisa , muda mwingi usiku nikiwa na Simu utanikuta nipo reddit najifunza mambo mapya tu .......nimefanya ku summarize Ili iishe tu hapo katikati hekaheka hazikosekani
Xmas ya juzi hapo, unajua mtoto akishakua mkubwa akili itamjia tu, huyu mwanangu mkubwa ashajua G sio mama yake mzazi japokua anamuita mama na wanapendana kweli, basi sijui ikawaje hio siku akamtamkia G Sasa " niache kwanza nataka Nije niende Kwa mama yangu" nikawaza nimchape pale nikaona na Xmas hii, nikampeleka mahali tumekaa pale Kuna vitu nikamuelezea akawa amenielewa, hapo kichwani nawaza kua na wewe mwanangu utakutana nayo tu.....
Xmas nipo na ba mdogo kubwa la maadui tumechinja na familia tu pale na mama mkwe alikuwepo at least Sasa npo nae sawa, nikawa nawaza Sana mambo mengi niliyopitia Kwa mbali nikawa kama napata huzuni, ila badae nawaangalia wanangu wote wanne, nikasema bila hizi Heka Heka nilizopitia Hawa wasingekuepo, nikawaangalia tena wanangu nikapata roho ya aamani, nikajiambia, this is my family,my clan!!!!
alamsikh..... Mwisho!!!
kaka Patrick mwezi February Narudi likizo Mwanza, kindly nitapenda tuonane unipe ABC fulani ambazo nimeona unaweza kunisaidia(za familia na mahusiano), kindly ni PM
kulipa mahari nusu ya dada mtu na kuoa mdogo mtu, hiyo ni zaidi ya experience, btw sikurudi nilibanana😁Mkuu naona unataka kampani ya gambe coz mtoa mada mambo ya familia na mahusiano hayupo vizuri kabisa.
Kabla hujafika mwanza akutumie namba za bamdogo
🤣🤣🤣🤣
Ni hatariS3 epi 17
Tunafika pale tukawasalimia kawaida tu, hapo mi nishapata hasira nawaza Sasa Hawa wazee wanataka nini kutoka kwangu, nikiwaza kama na kazini washafika huku tena wamekuja ni kipi hasa Hawa watu wanataka, nikasema acha tu ngoja tuone
Unajua Toka mwanzo wa hili sakata sio kwamba nilishindwa tu kukaa kimya na kuacha mambo yatavyokua yawe ila kuna mambo kama matatu nilikua nawaza Sana
a) kwanza kuhusu G, hili jambo lisipoliweka sawa ukizingatia na mazingira yenyewe ntamuweka kwenye wakati mgumu Sana hasa upande wa kwao na hata yeye kiujumla.....
b) pili nawaza hata nikisema nikae kimya tu Sasa mwisho wake inakua ni nini, huwezi tu kusema upo ugenini unakaa na mtoto wa mtu kibabe na wao wapo mkoa huo huo, sisi ni binadamu Kuna kuumwa Kuna mengine zaidi ya hapo siku likitokea la kutokea watu wanaweza kukugeuka vibaya Sana
c) katika Hali kama hii, ni Bora kumaliza tu hizi changamoto Ili hata mtoto/ watoto wanakuja kuzaliwa Kwa baraka, sio mtoto anazaliwa kwenye migogoro tayari...
Hivo nikasema acha tu nipambane mpaka nione mwisho wake ni nini hasa
Sasa kufika pale Hawa wazee ni kama walishampanga yule Mzee aliyeniita Sasa wa nzego maana tuliwakuta wanaongea kilugha, kufika pale yule Mzee wa nzengo akaanza kuniuliza " huyu ni nani(ba mdogo) Sasa" nikamwambia huyu ni Mzee wangu, Sasa yule Mzee akaonesha kuchukizwa kabisa.... Akaanza kuniambia " Sasa we nakuita uje hujajua hata nimekuitia nini unaanza kujihami kuja na watu kabisa, kwani mi nilikuambia ulete mtu huku?"
Sasa Ile body language ya yule Mzee yaani ni kama utasema ni mtu anaongea na mtoto wake, ba mdogo nae akaanza "kwani Kuna nini huku mbona hatuelewi?" Sasa kuna Mzee mmoja kati ya wale wazee waliokuja pale akawa anamwambia ba mdogo " wewe hivi vikao havikihusu hapa tunataka kuongea na kijana, wewe nilishakuona hamna kitu ndo maana umeshindwa kumshauri huyu kijana wako mpaka tumefikia huku" Sasa ba mdogo nae kashachukia hapo anajibu " mnakua watu wa ovyo, vitu vidogo mpaka kazini Kwa huyu bwana mshafika,mnahangaika nini mbona haya ni mambo ya familia, na mimi ndo Kila kitu hata kama hamnitaki hakuna mwingine wa kukaa nae zaidi yangu"
Ikawa kelele pale kurushiana maneno, yule Mzee wa nzengo hapo nae kanikata jicho la hasira, mimi mwenyewe nishapata hasira nikasema enough is enough....
NIkatulia kidogo nikamuuliza yule Mzee wa nzengo Sasa " hivi umeniitia nini?" Hapo nami nimeshaweka u serious, yule Mzee akaanza kuniambia " yaani wewe mpaka hapa na wazee wako umewakuta Bado unajifanya hujui nimekuitia nini" nikatulia pale.... Nikamwambia sawa najua basi ulichoniitia Sasa mnasemaje?? Yule mzee ni kama akawa haamini nilichokua namuambia akaanza kufoka " ndo tatizo lenu vijana, mnaharibu huko tunaangalia hata namna za kuwasaidia Bado tena mnajifanya wajuaji, shauri yenu"
Sasa hapo ba mdogo nae wanatupiana maneno na wale wazee wengine ishakua kama vurugu tu pale, ba mdogo akaniambia we twende bana, na mi nikaona yupo sawa hatukuaga Wala nini tukawa tunaondoka...... Yule Mzee wa nzengo Sasa akaniambia " we nenda tu ila mimi ndo Kila kitu hapa lazima utarudi tu"
Tukaondoka hapo nimechukia kweli, Sasa ba mdogo nae ndo ananiambia huyu Mzee wa nzengo nae ni mpumbavu tu kama hao wazee wenzake na kwanza watakuja kutufanya nini hao achana nao....
Tukawa tumeondoka, hapo Sasa siku zikaenda nakaribia kuanza kurudi kazini na Bado huku hata mambo sijamaliza, mama mkwe hapo nae nilishamtoa kwenye blacklist ila hakuwahi tena kunitafuta, G tunawasiliana tu Bado yupo Kwa shangazi kule, siku nikamwambia ba mdogo tuangalie Plan tumalize haya mambo kabla likizo haijaisha, plan ikawa tumtafute yule mama mwenye nyumba kule Kwa mama mkwe kimyakimya tukae nae chini tuone namna hili swala liishe kabisa.... Maana tuliona kama mama mkwe huyu ndo mtu anayemsikiliza
Tukaja Sasa pale kufanya umafia tukapata namba zake kweli siku tukamtafuta tukakutana nae mazingira tofauti kabisa ongea nae Sana, basi akahitimisha tujipange tu Sasa atatuambia lini tuje na pesa ambayo itakua ndani ya uwezo wetu tutoe kama baraka Kwa mama maisha yaendelee, hivo akasema tujipange tu atatuambia...
Hapo wale wazee na sisi tumewakalia kimya, nikaja tena kuambiwa naitwa kule Kwa yule Mzee wa nzengo Wala hata sikuenda, na Simu hapo akawa anapiga mimi kimya sipokei, nikapata wazo hapa Sasa ndo muda muafaka wa kuondoka huku, kumbuka kazini Sasa pesa tulikua tunapata ila inabidi uwe makini kwenye matumizi maana kazi za watu ukijifanya unajua Sana kufanya maendelea Kwa kasi tena kwenye pesa za Dili utajua hujui
Nikapata wazo, niende kazini "nijipige mtama" hii ni mbinu watu wengi wanatumia wakianza kufanya kazi kwenye sehemu ambazo wanapiga deals nyingi, Kwa mfano kipindi hiko kule site kwangu nilihitaji kufanya finishing tu, na mara nyingi kazini nilikua nikipiga deals pesa nyingi hua Nampa sister yangu yeye anaendelea kufanyia biashara, au mama anakua kama kaiweka tu, sio kwamba pesa ya kufanya finishing ningekosa ila kazini wakuda nao wengi Sana, hivyo nikaona Bora niende kuchukua mkopo mkubwa tu japo sikua nauhitaji( ndo kujipiga mtama huko) nifanye mambo yangu Kwa uhuru bila kuwaza ukuda wa kazini
Hilo wazo nilipata maana Kuna madogo pale kazini waliajiriwa japo kitengo tofauti walianza kupiga Hela Kwa kasi Sana, wakawa watu wa show off, Kuna jamaa akawa anawaambia wa lay low kwanza, wapi madogo hawaelewi, wakawa wanatumia resources za kampuni wanafanya kazi zao nje huko wanapiga pesa kweli, hazikupita siku wamekuja wote wamenunua harrier model mpya zinafanana wanakuja nazo kazini, hapo hata mwaka job hawana, sisi kimoyo moyo tunacheka tu, basi ikapita muda waliletewa ma auditor sijui kutoka wapi yaani walikutwa na mahasara vibaya mno mpaka wakawekwa ndani na kazi ikafa.....
Fast forward
Nikaanza ku apply mkopo kimya kimya hapo, nyumba nikaanza kuimalizia hapo Nina uhuru Sasa, ba mdogo nae Bado yupo huku, wale wazee wapo kimya sijui ndo wanapanga sera gani Sasa, nzengo hapo maneno mengi ila siwawazi kwanza nawaza muda wowote hapa nakuja kuhama.....
Basi mpaka ikafika siku twende Sasa kukaa kuyamaliza na wale kina mama kule, kiukweli hii haikua kazi ngumu, maana kumbuka hapo ni mama mkwe tu na yule mama mwenye nyumba na hapo tumepewa uhuru wa kuleta chochote, Sasa katika kitu tulichokua tumejadiliana na ba mdogo Kuna pesa tukawa tumetenga tuitoe, alafu kupitia yule mama mwenye nyumba tumwambia amshauri mama mkwe atumie Kile kiasi kumalizia nyumba yake alikua na ka site nyumba ya kawaida tu mgongo wa tembo haikua imeisha, maana Sasa maisha ya kupanga mpaka lini.....
Sasa kumbe wale wazee sijui walikua wanatumia njia gani Kila mipango tunayopanga wakawa wanaijua
Hio siku tumejiandaa na ba mdogo, na kile kiasi nikawa nipo nacho tumeweka kwenye gari sisi hao mpaka Sasa eneo la tukio, wazee nao Wana slogan Yao "ulipo tupo" .... Kufika tunakuta nje pale jopo Zima la wazee, mashangazi sijui hata wengine kina nani.... Wasukuma/nyamwezi shikamooni aisee
Mfungo ndyo huu weka ratiba ya saa 1 usiku baada ya futari mambo yaende vzuri tena iwe mfungo mzima.Nataka kuanzisha Uzi mwingine nielezee tu majanga yangu ambayo sitayasahau ambayo sikugusia kwenye uzi uliopita
Thanks mkuu hii story nimeisoma yote kwa siku 2 tu non-stop.Jirani kama jirani😀, sema kale kambulu kalikua kazuri ila kalinikuta kipindi nimevurugwa