S3 episode 6
nimjibu kwani nilikua mbaya siku zote? akawa ananiambia hapana bana endelea kua ivo ivo tu kaka, basi hapo na mi nishaanza kupata goosebumps najikuta tu namuwaza G, mapenzi shikamoo
ikaanza phase mpya sasa na G, sio mapenzi wala nini lakini tunajikuta tunachat tu muda mwingi nikiwa sipo nae, ila sio mambo ya mapenzi wala nini, utani wa hapa na pale.... mara kaniambie ujue dada atakuja kuniua patrick, mara kaanze kusema yule mwanamke wako aliyekuja ile siku ile sitaki tena kumuona kwangu.... basi tu utani wa hapa na pale
hapo na mimi nazidi kujenga trust tu, sionyeshi kutaka sana mambo ya mapenzi, kila nikipata nafasi siachi kuwanunulia zawadi hata kama ni vitu vidogo vidogo nae anajikuta tu kama anaanza kunipenda ila sasa anakua muoga kuniambia wazi
upande wa kazini napo Mungu anasaidia hali si mbaya kibanda changu nazidi kukiendeleza, nikipata nafasi siku ntawachukua G, mtoto mama mkwe tutaenda kuangalia basi wanafurahi tu, weakness nyingine ya G niliyokuja kugundua ni jinsi alìvyokua anaona mama yake anavyonipenda na kuniamini, siku hazigandi muda unaenda hapo ni kama G alishaniamini sana tu
sasa kuna siku G ananiambia leo tutakuja kulala huko kwako ongea na mama basi, basi nikiwa kazini nikampigia mama mkwe namwambia leo watume hao waje huku sasa nataka jioni niwapeleke mahali wakale akaniambia sawa hakuna shaka mwanangu
huyu mama nikawa nasema niende nae kwa makini maana ni kama alipata mashaka mara ya kwanza sitakiwi kuondoa trust yake kabisa, basi hio siku nikamuambia G nyie tangulieni mkiweza upike kabisa ntachelewa kurudi leo, badae akanijibu akaniambia sawa ila sitaki uchelewe, nikawaza mmmhh huyu leo ana nini acha tu tutaona
nikatoka kazini narudi home nakuta pako pasafi kabisa tofauti na siku zote , kashapika chakula kipo mezani wanaangalia tv, nafika hapo G ananipokea nikawa nawaza leo hapa shughuli ipo, nikakaa nao kidogo nikaenda nikaoga tukaja kula pale, kaa kaa sebleni badae mtoto akawa anasinzia G akaenda nae akamlaza mi nimebaki zangu sebleni, badae akaja mi npo tu na simu pale akakaa kimya, nikamwambia njoo basi mbona unakaa mbali, anazuga zuga pale ananiambia mbona hapa hata sipo mbali..... hio siku nikasema leo hapana ya nini kujitesa huku, nikamwambia njoo karibu kuna kitu nikuambie... akajivuta vuta pale badae akasogea.... nikamvuta karibu pale tutakiss kama dakika hivi anahema tu, sasa hii ndo ikawa first kiss maana ile siku ilikua vuta vuta hakuna romance wala nini, sasa badae akanisukuma akaanza niuliza hivi kaka una mpango gani na mimi???
weird question!! hakuna kitu sipendi kuulizwa kama hiki, nikamuambia tupo wote leo mbona una haraka sana leo mbona tutaongea mambo yote wala usijali, akaanza kujingata ngata pale ananiuliza hivi unajua mama ataniua mimi akijua na mambo mengine kibao, nikamwambia hebu relax kabisa tutajua tu cha kufanya
badae tukakokotana hao mpaka chumbani ndo ikawa first sex kabisa na yeye akiwa amerelax, basi sex sana pale na kupeana ahadi za uongo na kweli pale vitu ambavyo hata kesho pengine huwezi kumbuka, badae tutaenda mchukua mtoto room ile nyingine tukaenda kulala
kesho ratiba zangu kama kawaida nipo kazini nawaza hivi mwisho wa hii ishu ni nini? nikawaza sana nikawa sielewi, hapo G nae sms za mahaba tu kila saa namjibu fresh tu mapenzi kiutani tani yakaanza
ikaendelea hivo kama the next two weeks hivi kila akipata chance anakuja tunasex na nini, nakumbuka tu kitu nilichofanya ni kuzingatia kujua circle yake ya hedhi nisije chekesha dunia.... mambo yakaenda poa tu mpaka siku ambayo ilikua birthday yangu hapo ndo balaa likaanza sasa
mimi sasa sio mtu wa ma party wala nini, nakumbuka niliwatoa out G na mtoto tukaenda mahali tukala piga piga picha za hapa na pale, badae jioni mama mkwe akaja tukakaa pale mpaka usiku flani ivi nikawapeleka kwao mi nikarudi kulala
mapenzii kikohozi sasa, kumbe usiku ule G kapost picha yangu tukiwa nae na mtoto akaweka caption "family" na hio siku G kuna kofia yangu nilikua naipenda sana alikua amevaa, kumbe jini langu Rachel likaona ile status bana.... japokua haikua mbaya sana ila akawasha moto kuanzia kwa G mpaka kwa mama mkwe.... hapo mi sijui kitu....
asubuhi naamka nakuta sms kama zote kutoka kwa G na rachel, G analalamika kwamba jana dada kanitukana sana na maneno kibao yaani, rachel nae huku kaniandikia sms kibao nyingi tu kuna moja anasema " naona umalaya wako umehamishia kwa mdogo wangu"
hapo rachel namba nilishafuta ila nilijua ni yeye maana namba nilikua najua inaishia na ngapi, basi sikupanic nikarelax tu nikampigia G namuuliza kuna nini kwani ndo ananiambia kuna picha nilipost tu dada kanitukana sana na mama nae kaniuliza maswali mia kidogo, nikamuuliza mama umemwambia nini anasema sijamwambia kitu kwanza mi nimemwambia siwezi kufanya ivo.... nikamwambia sawa badae ntakuchek tutajua tunafanyaje
basi haikupita muda sana nipo kazini napata sms kutoka kwa mama mkwe
"mwanangu ukitoka kazini tuonane nina kikao na wewe"