Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

S3 epi 17



Tunafika pale tukawasalimia kawaida tu, hapo mi nishapata hasira nawaza Sasa Hawa wazee wanataka nini kutoka kwangu, nikiwaza kama na kazini washafika huku tena wamekuja ni kipi hasa Hawa watu wanataka, nikasema acha tu ngoja tuone



Unajua Toka mwanzo wa hili sakata sio kwamba nilishindwa tu kukaa kimya na kuacha mambo yatavyokua yawe ila kuna mambo kama matatu nilikua nawaza Sana

a) kwanza kuhusu G, hili jambo lisipoliweka sawa ukizingatia na mazingira yenyewe ntamuweka kwenye wakati mgumu Sana hasa upande wa kwao na hata yeye kiujumla.....

b) pili nawaza hata nikisema nikae kimya tu Sasa mwisho wake inakua ni nini, huwezi tu kusema upo ugenini unakaa na mtoto wa mtu kibabe na wao wapo mkoa huo huo, sisi ni binadamu Kuna kuumwa Kuna mengine zaidi ya hapo siku likitokea la kutokea watu wanaweza kukugeuka vibaya Sana

c) katika Hali kama hii, ni Bora kumaliza tu hizi changamoto Ili hata mtoto/ watoto wanakuja kuzaliwa Kwa baraka, sio mtoto anazaliwa kwenye migogoro tayari...


Hivo nikasema acha tu nipambane mpaka nione mwisho wake ni nini hasa



Sasa kufika pale Hawa wazee ni kama walishampanga yule Mzee aliyeniita Sasa wa nzego maana tuliwakuta wanaongea kilugha, kufika pale yule Mzee wa nzengo akaanza kuniuliza " huyu ni nani(ba mdogo) Sasa" nikamwambia huyu ni Mzee wangu, Sasa yule Mzee akaonesha kuchukizwa kabisa.... Akaanza kuniambia " Sasa we nakuita uje hujajua hata nimekuitia nini unaanza kujihami kuja na watu kabisa, kwani mi nilikuambia ulete mtu huku?"


Sasa Ile body language ya yule Mzee yaani ni kama utasema ni mtu anaongea na mtoto wake, ba mdogo nae akaanza "kwani Kuna nini huku mbona hatuelewi?" Sasa kuna Mzee mmoja kati ya wale wazee waliokuja pale akawa anamwambia ba mdogo " wewe hivi vikao havikihusu hapa tunataka kuongea na kijana, wewe nilishakuona hamna kitu ndo maana umeshindwa kumshauri huyu kijana wako mpaka tumefikia huku" Sasa ba mdogo nae kashachukia hapo anajibu " mnakua watu wa ovyo, vitu vidogo mpaka kazini Kwa huyu bwana mshafika,mnahangaika nini mbona haya ni mambo ya familia, na mimi ndo Kila kitu hata kama hamnitaki hakuna mwingine wa kukaa nae zaidi yangu"


Ikawa kelele pale kurushiana maneno, yule Mzee wa nzengo hapo nae kanikata jicho la hasira, mimi mwenyewe nishapata hasira nikasema enough is enough....


NIkatulia kidogo nikamuuliza yule Mzee wa nzengo Sasa " hivi umeniitia nini?" Hapo nami nimeshaweka u serious, yule Mzee akaanza kuniambia " yaani wewe mpaka hapa na wazee wako umewakuta Bado unajifanya hujui nimekuitia nini" nikatulia pale.... Nikamwambia sawa najua basi ulichoniitia Sasa mnasemaje?? Yule mzee ni kama akawa haamini nilichokua namuambia akaanza kufoka " ndo tatizo lenu vijana, mnaharibu huko tunaangalia hata namna za kuwasaidia Bado tena mnajifanya wajuaji, shauri yenu"



Sasa hapo ba mdogo nae wanatupiana maneno na wale wazee wengine ishakua kama vurugu tu pale, ba mdogo akaniambia we twende bana, na mi nikaona yupo sawa hatukuaga Wala nini tukawa tunaondoka...... Yule Mzee wa nzengo Sasa akaniambia " we nenda tu ila mimi ndo Kila kitu hapa lazima utarudi tu"



Tukaondoka hapo nimechukia kweli, Sasa ba mdogo nae ndo ananiambia huyu Mzee wa nzengo nae ni mpumbavu tu kama hao wazee wenzake na kwanza watakuja kutufanya nini hao achana nao....




Tukawa tumeondoka, hapo Sasa siku zikaenda nakaribia kuanza kurudi kazini na Bado huku hata mambo sijamaliza, mama mkwe hapo nae nilishamtoa kwenye blacklist ila hakuwahi tena kunitafuta, G tunawasiliana tu Bado yupo Kwa shangazi kule, siku nikamwambia ba mdogo tuangalie Plan tumalize haya mambo kabla likizo haijaisha, plan ikawa tumtafute yule mama mwenye nyumba kule Kwa mama mkwe kimyakimya tukae nae chini tuone namna hili swala liishe kabisa.... Maana tuliona kama mama mkwe huyu ndo mtu anayemsikiliza



Tukaja Sasa pale kufanya umafia tukapata namba zake kweli siku tukamtafuta tukakutana nae mazingira tofauti kabisa ongea nae Sana, basi akahitimisha tujipange tu Sasa atatuambia lini tuje na pesa ambayo itakua ndani ya uwezo wetu tutoe kama baraka Kwa mama maisha yaendelee, hivo akasema tujipange tu atatuambia...


Hapo wale wazee na sisi tumewakalia kimya, nikaja tena kuambiwa naitwa kule Kwa yule Mzee wa nzengo Wala hata sikuenda, na Simu hapo akawa anapiga mimi kimya sipokei, nikapata wazo hapa Sasa ndo muda muafaka wa kuondoka huku, kumbuka kazini Sasa pesa tulikua tunapata ila inabidi uwe makini kwenye matumizi maana kazi za watu ukijifanya unajua Sana kufanya maendelea Kwa kasi tena kwenye pesa za Dili utajua hujui




Nikapata wazo, niende kazini "nijipige mtama" hii ni mbinu watu wengi wanatumia wakianza kufanya kazi kwenye sehemu ambazo wanapiga deals nyingi, Kwa mfano kipindi hiko kule site kwangu nilihitaji kufanya finishing tu, na mara nyingi kazini nilikua nikipiga deals pesa nyingi hua Nampa sister yangu yeye anaendelea kufanyia biashara, au mama anakua kama kaiweka tu, sio kwamba pesa ya kufanya finishing ningekosa ila kazini wakuda nao wengi Sana, hivyo nikaona Bora niende kuchukua mkopo mkubwa tu japo sikua nauhitaji( ndo kujipiga mtama huko) nifanye mambo yangu Kwa uhuru bila kuwaza ukuda wa kazini


Hilo wazo nilipata maana Kuna madogo pale kazini waliajiriwa japo kitengo tofauti walianza kupiga Hela Kwa kasi Sana, wakawa watu wa show off, Kuna jamaa akawa anawaambia wa lay low kwanza, wapi madogo hawaelewi, wakawa wanatumia resources za kampuni wanafanya kazi zao nje huko wanapiga pesa kweli, hazikupita siku wamekuja wote wamenunua harrier model mpya zinafanana wanakuja nazo kazini, hapo hata mwaka job hawana, sisi kimoyo moyo tunacheka tu, basi ikapita muda waliletewa ma auditor sijui kutoka wapi yaani walikutwa na mahasara vibaya mno mpaka wakawekwa ndani na kazi ikafa.....


Fast forward

Nikaanza ku apply mkopo kimya kimya hapo, nyumba nikaanza kuimalizia hapo Nina uhuru Sasa, ba mdogo nae Bado yupo huku, wale wazee wapo kimya sijui ndo wanapanga sera gani Sasa, nzengo hapo maneno mengi ila siwawazi kwanza nawaza muda wowote hapa nakuja kuhama.....


Basi mpaka ikafika siku twende Sasa kukaa kuyamaliza na wale kina mama kule, kiukweli hii haikua kazi ngumu, maana kumbuka hapo ni mama mkwe tu na yule mama mwenye nyumba na hapo tumepewa uhuru wa kuleta chochote, Sasa katika kitu tulichokua tumejadiliana na ba mdogo Kuna pesa tukawa tumetenga tuitoe, alafu kupitia yule mama mwenye nyumba tumwambia amshauri mama mkwe atumie Kile kiasi kumalizia nyumba yake alikua na ka site nyumba ya kawaida tu mgongo wa tembo haikua imeisha, maana Sasa maisha ya kupanga mpaka lini.....


Sasa kumbe wale wazee sijui walikua wanatumia njia gani Kila mipango tunayopanga wakawa wanaijua



Hio siku tumejiandaa na ba mdogo, na kile kiasi nikawa nipo nacho tumeweka kwenye gari sisi hao mpaka Sasa eneo la tukio, wazee nao Wana slogan Yao "ulipo tupo" .... Kufika tunakuta nje pale jopo Zima la wazee, mashangazi sijui hata wengine kina nani.... Wasukuma/nyamwezi shikamooni aisee
 
Ulipo tupo
 
Kaka patrickk samahi naomba kujua Baba mdogo anafanya kazi gani pia kama anafamilia au laha maana kwa kipindi alicho kaa kwako bila kazi ya kumuingizia kipato aliweza vipi kuhudumia familia yake?
Alafu Hili swala nilitaka kuliongelea tangia mwanzo, ba mdogo yeye alishaachana na mke wake siku nyingi na alikua na watoto wawili wakubwa nadhani kipindi hicho wa kiume form 6 wakike form 3 kama sikosei, alafu huyu mwamba alikua mission town sana Hana kazi Moja specifically, na huku kwangu alikua anapapenda Sana mambo ya mtungi totoz uhakika, alafu huwezi kuamini mpaka Leo tupo karibu Sana akionaga mambo yake hayaelewi anaweza kuja kukaa kwangu hata miezi minne hua inaisha, na mi namkubali sana
 
Aaliyyah Kalpana
 
Wazee wamkataa Bamdogo wetu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… wanaona anawazibia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…