BoManganese
JF-Expert Member
- Jun 10, 2017
- 980
- 2,679
Habari zenu wanaJF. Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, katika harakati za hapa na pale katika maisha inaweza kutokea situation fulani tuu ukajikuta unajua kitu na kukifanya mbele za watu hatimae unaumbuka hapo ndo unakuja ule msemo usemao "utajua ujui".
Mimi binafsi miaka ya nyuma kidogo nilienda water park fulani hivi kurefresh kuogelea kwenye swimming pools kufika pale nikakuta kuna swimming pools za wakubwa zenye kina kirefu na za wadogo zenye kina kifupi. Sasa sikutaka hata kujiuliza kwanini kule kwenye kina kifupi ndio kuna watu wengi kuliko ile pool nyingine yenye kina kirefu nikaona potelea pote washamba tuu. Kwakweli sikuwa nimewahi kwenda before ndo ilikuwa ni mara ya kwanza ndipo kidume nikajikuta mjuaji kwamba ndio best diver sikutaka kwenda kwenye kina kifupi nikajichanganya kwenye swimming pool yenye kina kirefu na kulikuwa na alert kabisa pale ila mimi nikajiona much know. Basi nikaingia kwenye swimming pool taratibu nikiwa nimejiegemeza pembezoni kabisa huku ukutani nikicheki watu wawili watatu mule wakicheza michezo yao.
Sasa sijui ni kitu gani kikanitekenya nikaona ngoja nisogee pale katikati nikajipush kutoka pale pembezoni yaani kama nilitumia nguvu ya ule ukuta kuswim hata pale kati sikufika vizuri nikaanza kuhisi kama navutwa ndani ya maji nikaanza kuvuta picha kwa wale wataalam wanavyo ogelea huwa kuna namna wana piga miguu ndani ya maji wanaelea basi na mimi nikaanza kufanya vile nikawa narudi juu kidogo nikiacha kupiga miguu nazama tena pale kwenye angle ya swimming napaona ila kupafikia ndio ilikuwa shughuli kwangu nilipiga sana miguu nikatumia utaalamu wote niliouona kwenye TV vile wanaogeleaga lakini wapi kupiga kelele za kuomba msaada napo nilikuwa naona aibu.
Mwisho wa siku baada ya kutapatapa sana na ukizingatia kwenye angle palikuwa sio mbali basi nikachoka nikajiachia tuu nikawa nazama ndo kama nilikuwa naiona dunia inazunguka nikiwa ndani ya maji huku nikiwa nakunywa vikombe heavy vya maji taratibu kabisa. Wakati naelekea kufumba macho kuiaga dunia kwa mbali nikaona malaika ananipa mkono na mimi nikaona nimpe mkono japo kwa kujikongoja sana huku nikijisemea moyoni Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, nikampa mkono. Mara ghafla nikaona nimeibuliwa kwa nguvu kutoka ndani ya maji kumbe alikuwa ni jamaa tuu nahisi alikuwa ananichora tuu tangu mda ule natapatapa.
Basi akanivuta akanishikisha ile angle aisee niliing'ang'ania kwa nguvu zangu zote huku nikiwa nakohoa nikapanda hadi juu nje ya swimming pool kwa speed ya mwanga nikakaa pembeni nikiwa siamini yaliyo nitokea pale dakika chache zilizo pita huku kwa mbali nikisikia vicheko vya watu ni dhahiri kabisa mimi ndiye niliyekuwa nachekwa maana kwa wakati huo akili haikuwepo kabisa pale.
Nikanyanyuka nikatafuta nguo zangu zilipo nikavaa nikapiga msosi pale fasta nikaondoka zangu home bila hata kugeuka nyuma. Yaani hapo ndio nilijua sijui.
Vipi na nyinyi wadau ni kitu gani ulijifanya mjuaji ukaumbuka hebu tiririkeni hapo hata kama sio wewe lakini ulimshuhudia mtu mwingine,
Karibuni.