Ushawahi kukuta nyumba kama danguro……….!?

Ushawahi kukuta nyumba kama danguro……….!?

Mirathi hii nimejichagulia na sitaki kupangiwa! Ila nashukuru kwa strict upbringing, imenisaidia sana na hii gun ya urithi ndo usiseme!
Sasa dingi hapo kwenye kuficha mambo kwa Ngina ndo tunapokosana! Talk to the lil gal! Tell her kumvulia nguo mwanaume kabla hajakuoa ni kujishushia heshima yako! Build that kichwani kwake! Wata-pollute mind yake afu tubadili kilio sasa hivi, usiniite ujue!
Mie visa vyangu huwa wanarithi watoto wa kiume tu, sasa sijui wewe hiyo mirathi umeipataje.............!? LOL
Naomba nikupongeze kwa namna ulivyoweza kukopi na kupesti tabia zangu, si unajua wakati nawalea nilikuwa nawashikisha adabu na henzirani pale mnapotoka nje ya mstari. nilikuwa sina mchezo na ndio maana mmekuwa na adabu na hishma mpaka ukubwani.

Kuna jirani yangu watoto wake wa kike hawa adabu kabisa, unaweza kukuta usiku wazazi wamelala wao wako nje kibarazani eti wanapiga stori na washkaji zao, kumbe wanafanya Malabuku viambazani mwa uzio wetu, tukiamka asubuhi tunakuta vifanyio kila kona. kuna siku huyu mdogo wako Ngina aliniuliza ni nani anatupa vile vifanyio pale nje kwetu nikamwambia ni watoto wa majirani wasio na staha na miili yao. lakini alipotaka kujua zaidi, maana Ngina haishi udadisi nikamkata kalma na kumtaka akajifungie chumbani kwake afanye home work.
 
Terms and conditions ndo zinapoapply sasa. Lazma kila anaechelewa kurudi home aseme anachelewa wapi na kwa nini. Unless ni shuleni. Kurudi saa kumi alfajiri once in a while sio mbaya na itolewe taarifa pia. Ila ungehitaji matron,lol! Anytime u need my service holla me, nadhani wasiofit wataondoka wenyeewe!
Self discipline ni muhimu kwenye maisha bana!
mimi kiukweli kingasti sipendi kelele kabisa.so kukaa nyumba watu 7 kwanza nisingeweza makelele na pia displine ingekuwa ngumu kuimonitor.besides mimi sio mzazi wao atii niliwatimuaje mimi huwa sina unafiki cause hata wazazi wao hawajawai kunisaidia
hawa ndugu wa kukujua wakati wa mafanikio huwa siwafagilii kabisa
khaaaa
 
Pole mamito!
Ila huo ndio ukweli wenyewe!
Wajitahidi na wao wawe na kwao ebo!
 
Heshima yako baba,hizi nyumba zawezekana zikawepo kbs,
Dah!hii habari imenikumbusha nyumba moja niliishuhudia maisha yake hata sijui ndio ndanguro au nn?

Kuna shost wangu alikuja huku kikazi ili kubana hela akafikia kwa shangazi yake baada ya siku 2 akapata homa akawa ameshinda nyumban kumbe pale kuna wadada 3,wawili wana watoto 2 kila mmoja na huyo shangazi na ndugu wengine 2 wadada,nikawa nimeenda kumjulia hali kwa mda wa nusu saa niliokuwa pale nikagundua haya;

Ile nyumba haipikwi kila mtu anajitegemea au anajipikia,mwingine akinunu sukari mwingine vitafunwa akizuba kidogo mwenzie keshaviiba,huku mama analalamika sabun yake kuna mtu kachukua,yani hapo wanaishikm cjui km nn ni vurugu kuibiana,mpaka viatu mwingine anatoka navo,watoto wanapigana mama zao wanagombana wanatukanana matusi ya ajabu,yani nilihis kuchanganyikiwa,

Ikabidi nimuulize shost anaishije pale akasema naye anashangaa kwani huwa anatoka asubuhi na kurudi usiku yale hakuwahi kuyaona mie nikamwambia najihic siko sawa narudi zangu kwangu akaingia ndan na kuchukua kibegi chake akaaga tukaondoka naye,yaan nilibaki na mshangao na kutoelewa km kuna familia za maisha ya vile!!!
ujue nini maisha ni magumu cantalisia.unakuta nyumba ina watu kumi ndugu ndugu tu tofauti huo mlo utakuwa sh ngapi? na mambo watu wanakuja mjini wanakaa tu kwa watu naona sio fresh ndo hvo unga robo ukichelewa shauri yako.
inapendeza sana tena sana familia ikikaa pamoja na kula pamoja,so no ya watu nyumbani nadhani ni jambo la kuangalia
ndo maana kuna watu wapo strict sana na wageni wa hme kwao.
kuna bro wangu anakaa masaki kwake jumba kubwa sema ndugu yangu yule ile ni roho mbaya.yaani kwake hulali kabla sijahamia dar ilikuwa nikija kwa interview ananipa hela ya hoteli nakwapia
ndo maana mimi sipendi kukaa kwa watu kama ndugu yangu kaniona mzigo je huko kwa wengine si nitanyanyapaliwa hadi basi?
cha kujitesa?
 
Khaaaa!
Haki ya mungu hii sijawahi kuisikia aisee,
Ila nahisi ni utaratibu wake tu,na ndio maana alikua anakupa hela ya hoteli,
Ila huo ukauzu yataka moyo,

Nikweli maisha ni magumu aisee mambo ya kuleana bila sababu ya msingi ni kupeana majukumu na kutafutiana dhambi za bure,
Nikuwekeana mipaka na taratibu tu mtu akiona hawezi aangalie ustarabu mwingine,
Bora umepanga kwako,kuishi kwa ndugu ishu si mchezo!!
 
Mirathi hii nimejichagulia na sitaki kupangiwa! Ila nashukuru kwa strict upbringing, imenisaidia sana na hii gun ya urithi ndo usiseme!
Sasa dingi hapo kwenye kuficha mambo kwa Ngina ndo tunapokosana! Talk to the lil gal! Tell her kumvulia nguo mwanaume kabla hajakuoa ni kujishushia heshima yako! Build that kichwani kwake! Wata-pollute mind yake afu tubadili kilio sasa hivi, usiniite ujue!
Naona aibu mie, haya mambo ni ya mama yako mama Ngina, lakini yeye mwenyewe anadai eti Ngina anamchosha na maswali......... Itabidi nimlete kwako akae na wewe kipindi ukiwa likizo ili uone jaramba lake................LOL
 
Khaaaa!
Haki ya mungu hii sijawahi kuisikia aisee,
Ila nahisi ni utaratibu wake tu,na ndio maana alikua anakupa hela ya hoteli,
Ila huo ukauzu yataka moyo,

Nikweli maisha ni magumu aisee mambo ya kuleana bila sababu ya msingi ni kupeana majukumu na kutafutiana dhambi za bure,
Nikuwekeana mipaka na taratibu tu mtu akiona hawezi aangalie ustarabu mwingine,
Bora umepanga kwako,kuishi kwa ndugu ishu si mchezo!!
ndivo alivo yule ana madharau balaa balaa sijui ni nini ndugu yetu yule
 
Ndo maana mi nasema kila siku,wale binadamu aliowaumba Mungu na kuwapa zile sifa za kwenye maandiko walishaisha zamani sana!Hawa walioko leo ni makapi tu!
 
Hizi familia zilizopinda ki-maadili zipo sana na yahitaji Mungu ili nasi tusiishie huko...maana matendo yetu tulio wengi kuanzia maongezi,kuchat kwenye mtandao/simu, mahusiano kazini yamejaa tamthilia za matusi na uchafu kama huo.

Si ajabu siku hizi kuongea maneno ya chumbani na office mate wako au kuvizia binti wa fulani anaesoma sekondari..na mzunguko unaendelea kwa sababu maumivu ya kichwa yanaanza polepole ndivyo tabia za aina hii hujengeka polepole.
 
haya mambo ni kutokuwa na heshima tu.sisi tumelelewa na mama tu baada ya mdingi kutangulia mbele ya haki(r.i.p) lakini maza ametudiscipline vizuri sana.ilikuwa ni marufuku ushoga wa kishenzi kishenzi,ile sijui naenda kwao fulani sijui fulani kaja home wiz no gudi bikoz..marufuku.mimi mpaka nafika hapa sina mashoga wa ovyo ovyo,sijawahi kutoka home eti nikalale kwa mtu unles kuna msiba na ni mtu wa karibu sana.
 
Kwakweli!wengine sleepovers tumeona kwenye movies tu hadi tunakua,.sa hivi kunipeleka kulala kwa mtu ni ngumu kwakweli,i wont live but survive...mtambuzi,ni wazazi kutoeka mipaka,watoto kutojitambua..
 
Mimi siwezi kumtongoza mwanamke afu nikubali kupelekwa maskan kwo ku do! Hatakama kantongoza yeye eneo la tukio ntatafuta mimi
 
sidhani kama ipo kwa tz yetu.
Kaka unaishi TZ ipi? haya maisha yapo sana mimi ninayo mifano live mitatu: 1). kwa wale tulioishi Arusha miaka ya mwanzo ya sabini pale kaloleni ukitokea central police kuelekea mnara wa azimio ukivuka mto naura mkono wa kulia kabla hujafika makaburini kulikuwa na nyumba za town concil hizi jamaa yangu zilitia fora. Longanii, Mandepee, Malonga na wengine kama mpo humu jamvini mtanigongea like. 2).kwa wale tulioishi tandika kilimahewa miaka ya mwanzo ya themanini Maeneo ya midizini guest house mtakumbuka tulivyokuwa tunakosa usingizi mabaa yakishafungwa kila mkaazi wa nyumba Yetu akiwa mwanamke anakuja na mwanaume na mwanamme anakuja na mwanamke sasa shughuli ikianza kila mmoja anaugulia kwa starehe kumzingua mwenzie. Mstahiki meya Mrutu kama upo humu UTANGONGEA LIKE. 3).kwa wale tulioishi temeke mikoroshini kona ya mtaa wa ruvuma na maganga kuelekea njaro club miaka ya themanini mwishoni nyumba za dizaini hii zilikuwa siyo kitu cha ajabu. Nimekumegea tuu kidogo kaka MESTOD hayo ndiyo maisha ambayo sisi tumeyaishi tangu utotoni taabu mtindo mmoja na sii ajabu siku ya kiama tukaenda motoni vilevile maana aliye nacho huongezewa na asiye nacho hunyanganywa kabisa hata kile kidogo kama anacho.
 
Kuna nyumba ambazo ukiangalia maisha ya wanaoishi ndani ya nyumba hizo huwezi kuzitofautisha na danguro. Hebu fikiria nyumba ambazo watoto wa kike wanaingiza marafiki zao wa kiume na kufanya nao mapenzi humo, iwe mchana au usiku. Watoto wa kiume nao ni kama hao dada zao nao huja na wanawake zao na kufanya nao mapenzi humohumo ndani ya nyumba.

Lakini hata baba naye akipata mwanamke wa kupitisha naye usiku hujivinjari naye ndani ya nyumba hiyo hiyo. Kama ni mama, akiibua buzi lake huko atokako atakuja nalo na kufanya nalo mapenzi humo humo ndani ya nyumba ya familia huku watoto wakishuhudia. Aibu gani hii!Mara nyingi tabia hizi hujitokeza zaidi katika nyumba za mzazi mmoja. Inawezekana wazazi wameachana au mmoja amefariki, au huyo mzazi anaishi na watoto ambao alizaa kila kona na kuwakusanya hao viumbe wake na kuamua kuishi nao.

Kwa sababu, kila mtoto amelelewa kivyake huko alikotoka au kwa sababu, baada ya mzazi mmoja kufariki au kuachana, aliyebaki na watoto alishindwa kuwalea vema na sasa wamegeuka nunda halisi.
Sisemi nyumba zote zenye mzazi mmoja zinakuwa hivyo, hapana. Naogopa nitasakamwa. Nazungumzia zile nyumba za mzazi mmoja ambapo mzazi huyo kwa bahati mbaya au kwa hiyari yake bila kujua ameiharibu familia kimaadili.

Bila shaka mtakuwa mnazijua familia za aina hiyo, angalau moja.
Nyumba hizi ni kama nyumba ambazo ni mtaa humohumo ndani ya nyumba. Huyu anaingiza mtu wake chumba hiki na yule anaingiza mtu wake chumba kile. Kama kwamba ni watu majirani tu wanaoishi mtaa mmoja na hakuna mwenye haki ya kuuliza kuhusu maisha ya ndani ya mwingine. Kama baba au mama anafanya hivyo mbele ya watoto, unadhani atathubutu vipi kumkemea mtoto? Tena mtoto mwenyewe ameshaanza kuvuta bangi au kubwia ‘unga,’ thubutu!
Mtambuzi tunasema kua uyaone, nakwambia mjini watu wengi wana maisha ya ajabu, kuweza kudhibiti hali hiyo yahitaji busara ya ziada!!! Kwa sababu inawezekana ukawa forced kuingia kwenye hali kama hiyo, sijui utaua watu nyumbani kwako maana ukifukuza sio jibu huko watakako kwenda watakuwa hivyo tena!!! Kuokoka linaweza kuwa jibu zuri wakati mwingine, the control should be spritualy by the gaidence of the Lord Jesus!!!!!

Kaka unaishi TZ ipi? haya maisha yapo sana mimi ninayo mifano live mitatu: 1). kwa wale tulioishi Arusha miaka ya mwanzo ya sabini pale kaloleni ukitokea central police kuelekea mnara wa azimio ukivuka mto naura mkono wa kulia kabla hujafika makaburini kulikuwa na nyumba za town concil hizi jamaa yangu zilitia fora. Longanii, Mandepee, Malonga na wengine kama mpo humu jamvini mtanigongea like. 2).kwa wale tulioishi tandika kilimahewa miaka ya mwanzo ya themanini Maeneo ya midizini guest house mtakumbuka tulivyokuwa tunakosa usingizi mabaa yakishafungwa kila mkaazi wa nyumba Yetu akiwa mwanamke anakuja na mwanaume na mwanamme anakuja na mwanamke sasa shughuli ikianza kila mmoja anaugulia kwa starehe kumzingua mwenzie. Mstahiki meya Mrutu kama upo humu UTANGONGEA LIKE. 3).kwa wale tulioishi temeke mikoroshini kona ya mtaa wa ruvuma na maganga kuelekea njaro club miaka ya themanini mwishoni nyumba za dizaini hii zilikuwa siyo kitu cha ajabu. Nimekumegea tuu kidogo kaka MESTOD hayo ndiyo maisha ambayo sisi tumeyaishi tangu utotoni taabu mtindo mmoja na sii ajabu siku ya kiama tukaenda motoni vilevile maana aliye nacho huongezewa na asiye nacho hunyanganywa kabisa hata kile kidogo kama anacho.

Bravo Broda..........................., nimeona niwe wa kwanza kukugongea LIKE kwa kunisaidia kumjibu huyo MESTOD, maana alinikata stimu kabisa kwa kukanusha madai yangu.
 
Nyumba za namna hii zipo nyingi tu, nimewahi ishi mojawapo. Ilibidi niache tu kodi yangu ya mwaka baada ya kuishi kwa taabu miezi miwili..
 
Hayo ni madhara ya kizazi cha nyoka cha watoto wasioheshimu wazazi. Na wazazi kwa kutowafunza watoto wao AMRI YA NNE, laana hutembea kizazi hadi kizazi.
 
Back
Top Bottom