Ushawahi kukutana na hii kamati ya Nidhamu? Tuambie ilikuaje!

Ushawahi kukutana na hii kamati ya Nidhamu? Tuambie ilikuaje!

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
FB_IMG_1647060155119.jpg

Huyo ni.mdudu hatari sana, anaitwa Nyigu.

kwa maumivu yake hata Nyuki anasubiri

Mara ya kwanza kukutana nae alinipa Komwe la muda mfupi na maumivu ya hatari😅😅

nikimuona naanza safari ya kujihami mapema sana

vipi kwako, tupe stori..
 
Hivi vitu vinauma Bora umtumie Demu nayakutolea asije maumivu unaweza vumilia ila hawa hapana kabisa.
 
Hivi vitu vinauma Bora umtumie Demu nayakutolea asije maumivu unaweza vumilia ila hawa hapana kabisa.
😅😅😅😅😂😂😂
Maumivu yake ni hatari, mapenzi yakasome
 
Hawa jamaa waliwahi kutushughulikia tulikuwa tumeenda kuiba maembe kwenye shamba la mzee mmoja alikuwa analilinda na mishale akitukuta anatutishia.

Nilisikia maumivu mgongoni nikajua leo nimepigwa mshale kume vilikuwa hivi vijamaa, kufika nyumbani bi-mkubwa naye akatushughulikia kwa nini tumeenda kucheza maporini....aisee utoto raha😆
 
Mmoja tu alitosha kunipa kichapo cha tatu bila...shingoni,kisogoni na kwenye mkono ndani ya sekunde
 
Hatari, kabla ya kung'ata anakuachia wenge kwa ule mngurumo wake kama engine ya Jet.
 
Ndio Rwanda wakaipa timu yao ya taifa ya soka jina la Manyigu (Amavubi).

Ni wadudu wakali kweli kweli
 
Kuna Yale meusi yanatotoboa mbao!

Kuna ng'ombe aligongwa na ng'onda alikimbia hapa na doksi
 
Back
Top Bottom