Hii kawaida sana Mkuu.
Wengine mpaka Makondakta wameshatukariri kabisa.. Hata tukisafiri, tukirudi anakwambia Bro hatujakuona siku mbili tatu hizi, vipi ulisafiri nini? Na hata nikimlipa nauli kubwa kama hana chenji anakwambia nenda tu, utanipa siku nyingine..
Nikipanda tu gari yake wala sihangaiki kumwambia anishushe kwenye kituo changu, tukifika anagonga Bodi nashuka.. Kuna siku nilisinzia Konda akasimamisha Gari akamwambia abiria wa pembeni yangu; "Niamshie Braza huyo anashukia hapa".[emoji1][emoji1]