Ushawahi kupata pesa nyingi sana kwa wakati mmoja bila kutegema? Ulijisikiaje?

Ushawahi kupata pesa nyingi sana kwa wakati mmoja bila kutegema? Ulijisikiaje?

daxy Jr

Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
88
Reaction score
307
Kwema wadau? Leo kwenye pitapita zangu mtandaoni nilikutana na picha hii chini ya huyo mwamba aliyeshinda Milioni 10 kwenye kampuni moja ya kubetti mtandaoni, Sokabet.

Nilibaki najiuliza tu huyo mwamba anajiskiaje? Furaha sana maana inawezekana hajawahi kushika pesa nyingi hivyo? Au anajiskia uoga pia akifikiria kuitumia vibaya? Vipi akifikiria kuombwa na kila mtu wake wa karibu? Nawaza ila sipati majibu kwasababu haijawahi kunitokea!

JACCCCCCCCKPOO.jpg
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Wazee wa kubeti
 
umenikumbusha 1m yangu nilivyoitia kwenye chipsi😢😢😢
 
Pesa yangu nyingi kushika kwa mara ya kwanza ilikua 5.7mil...nilishinda mbet 2014...

Nilihama hostel za chuo nikapanga hotelini,wiki 3 tu nikabaki na 100k nikarudi hostel...

Ule mkeka niliscreenshoot nikaubackup gugodrive
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] masihara hayo ,,,, ukamahama na makazi
 
Pesa za haraka hivi hazina baraka sometimes niliwahi pata mil 8 lakini mpaka leo sijui nimefanya kitu gani cha maana nilikuwa nafanya kazi sehemu waka terminate contract by mutual agreement ilikuwa imebaki miezi michache wakanipa hela za kuvunja mkataba na hela nyingine nikaenda kuchukua NSSF jumla zikawa million 8 aisee ziliyeyuka hata sijui ziliishaje.
 
Pesa yangu nyingi kushika kwa mara ya kwanza ilikua 5.7mil...nilishinda mbet 2014...

Nilihama hostel za chuo nikapanga hotelini,wiki 3 tu nikabaki na 100k nikarudi hostel...

Ule mkeka niliscreenshoot nikaubackup gugodrive
Hahahaha waafrika bhana ni watu wasiopenda taabu kabisa, Wakipata lazima wale raha

... kongole mzee
 
Back
Top Bottom