Ushawahi kwenda kwa mganga?

Mukuu123

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2019
Posts
319
Reaction score
1,223
Nakumbuka ilikua mwaka 2012 nikiwa niko chuo tulipanga nyumba nzima maeneo ya Buguruni mimi na vijana wengine kama wanne, sasa ikatokea laptop kuibwa katika mazingira ambayo mimi ndio nilikua suspect so ikabidi maamuzi kwamba twende kwa mganga ili kujua nani kachukua, wakati huo kuna jirani yetu naye aliibiwa akaenda kwa mganga na akaipata simu yake, akatushauri twende kwa uyo mganga wake, tulikubaliana.

Tukipofika kwa yule mganga yule jamaa angu aliyeibiwa akapakwa dawa flani machoni na mbele kukawekwa kitambaa Cheupe kama tv, baada ya muda yule jamaa aliyeibiwa akaanza kuona picha ya nyumbani kule namna wizi ulivyotekea, sasa ile dawa ilikua kama inamuumiza sana ilitakiwa akaze macho na kuvumilia maumivu ili ile picha isipotee, alikua anakaza sana macho huku akiwa anatuambia nini anachokiona kwenye lile tambala jeupe lililoko mbele yake lakini hakufanikiwa kuona tukio lote kutokana na maumivu anayoyapata. Finally ikabidi awekwe dawa mtu mwingine ambaye alikua dem wangu lakini pia hakufanikisha kutoka na maumivu aliyokua anayapata.

Tukaamua kuondoka sasa yule mwanamke wangu wakati tuko njiani akaanza kupiga kelele kwamba anaona mambo ya ajabu barabarani alikua anapiga kelele mnoo yani HITIMISHO LANGU ni kua hii dunia kuna mambo mengi ya kiroho ambayo hayawezi kuonekana kwa macho ya kawaida, kuna watu wanasema kwamba uchawi Na Mungu ni vitu vya kufikirika lakini si kweli ni vitu ambavyo vipo katika ulimwengu wa kiroho zaidi ndio maaana Yesu anasema onjeni muoni yesu ni mwema.
 
Ni ww tu kuchagua lakini vitu vipo siyo kwamba ni story za kufikirika just imagine mtu anauwezo wa kurudisha matukio ya nyuma Na ukayaona
Mahakama za nn kutafuta ushahidi, dunia nzima hakuna serikali inawaamini hawa watu.
 
Max mwambie alipie tangazo uyu jamaa siyo anakuja jitangaza bure bure.
 
Pakitokea wizi siwezi kukubali upumbavu wa kuleta mganga eti atumie madawa yake kujua mwizi, hichi kitu hakipo katika imani yangu.

Hayo madawa wanayokupaka saa nyingine yanakuja kukuletea matatizo makubwa zaidi (kukuroga)

Hao watu sio wa kuamini,
 
Hizi story natamani niwe shuhuda siku moja ili niziamini..
 
Nilikunywa damu mbichi ya kuku glass nzima,

Nilikunywa uji ulipikwa na kuchanganywa na Yale majani ya baharini Yale mawimbi yakija unaona yanakuja.yako kama nyavunyavu ya kiijani.bado nikayaoga

Nilichanjwa chale mwili mzima,nilinyilewa nywele zangu ndefu nkabaki uoara

Nilfukizwa kwenye mijungu,

Nashukuru si kwenda kwa hiyari yangu Bali shida za dunia na wakunisaidia walikua wa naamini huko

Siku nkakata shauri nikawaambia enough is enough huu ushenzi sitaki tena na ukome.kama kunitenga mnitenge.wakanitishia ntakufa.nkawaambia sifi kwa jina Yesu

Kumrudia Yesu wangu na kula kiapo sitarudi nyuma nikatengwa,sisaidiwi,napuuzwa,changamoto zikazidi but sikuruhusu imani yangu iyumbe.nikasimama imara.
 
Sitasahau Mganga alichotufanyia

Jamaa zangu waliibiwa simu na PC enzi tuko chuo[...] Mganga alitupaa Masharti " Moja ya Sharti lilikuwa ni kwenda kulala saa 11 Jioni mpaka asubuhi" πŸ˜‚

Kesho yake kumtafuta Mganga Hapatikani πŸ˜‚πŸ˜‚ aiiisee tulichoka simu na PC hatukupata na pesa zimeliwaa 🀣🀣🀣

Kila nikikumbuka huwa nacheka sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

NB Mganga sio wa kuamini
 

[emoji3][emoji3] Kuna dada aliibiwa simu akaenda kwa mganga wa tv akamwona mwizi wake na akarudishiwa simu.
 
Mambo ya kwenda kwa waganga hayana suluhu ya kudumu hakuna cha maana huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…