Mukuu123
JF-Expert Member
- May 7, 2019
- 319
- 1,223
Nakumbuka ilikua mwaka 2012 nikiwa niko chuo tulipanga nyumba nzima maeneo ya Buguruni mimi na vijana wengine kama wanne, sasa ikatokea laptop kuibwa katika mazingira ambayo mimi ndio nilikua suspect so ikabidi maamuzi kwamba twende kwa mganga ili kujua nani kachukua, wakati huo kuna jirani yetu naye aliibiwa akaenda kwa mganga na akaipata simu yake, akatushauri twende kwa uyo mganga wake, tulikubaliana.
Tukipofika kwa yule mganga yule jamaa angu aliyeibiwa akapakwa dawa flani machoni na mbele kukawekwa kitambaa Cheupe kama tv, baada ya muda yule jamaa aliyeibiwa akaanza kuona picha ya nyumbani kule namna wizi ulivyotekea, sasa ile dawa ilikua kama inamuumiza sana ilitakiwa akaze macho na kuvumilia maumivu ili ile picha isipotee, alikua anakaza sana macho huku akiwa anatuambia nini anachokiona kwenye lile tambala jeupe lililoko mbele yake lakini hakufanikiwa kuona tukio lote kutokana na maumivu anayoyapata. Finally ikabidi awekwe dawa mtu mwingine ambaye alikua dem wangu lakini pia hakufanikisha kutoka na maumivu aliyokua anayapata.
Tukaamua kuondoka sasa yule mwanamke wangu wakati tuko njiani akaanza kupiga kelele kwamba anaona mambo ya ajabu barabarani alikua anapiga kelele mnoo yani HITIMISHO LANGU ni kua hii dunia kuna mambo mengi ya kiroho ambayo hayawezi kuonekana kwa macho ya kawaida, kuna watu wanasema kwamba uchawi Na Mungu ni vitu vya kufikirika lakini si kweli ni vitu ambavyo vipo katika ulimwengu wa kiroho zaidi ndio maaana Yesu anasema onjeni muoni yesu ni mwema.