Ushawahi panda gari za kusafirisha magazeti ?

Ushawahi panda gari za kusafirisha magazeti ?

Kwan huwa wanatumia gari za aina gan?
Ist, kluger, hiace, au? Maana licha ya mwendo mkali Ila sijawah kusikia ajali zinazohusu izo gari za magazeti.
Zipo za aina nyingi, hiace, pickup nk
 
Aiseee zile gari acha kabisa

Yani kabla hujakaa tayari upo Kibaha mana Dar - Moro ni lisaa tu 😂😂😂😂

Kupanda zile gari inahitaji uwe na roho ya paka 😆😆😆

Sishauri kabisa wanawake kupanda zile gari mana sisi wanaume tu tunapanda kwa dharura

Embu tupe uzoefu wako mara ya kwanza kupanda zile gari ulijiskiaje
Wenye uzoefu mkubwa wa hayo.magari, muda huu wapo.makaburini wamechill.

Sipandagi hizo gari maana ni kama jeneza zinazotembea
 
My dear,
Siku yako ikifika hakuna kitakachozuia, unaweza hata usitoke nje lakini ukafia kitandani kwako..!!
Nadhani ndo maana tunakwama, Mungu katutia akili tujishughulikie, sisi tunajitoa akili kusubiri afanye miujiza.

Ajali zinaweza epukika mpaka kuleta maana halisi ya ajali.

Barabara za ovyo, mwendo wa ovyo, unachokimbiza ni cha ovyo...Dar-Moro tu, taa za kuangaza barabara ziko maeneo gani labda?

Ukila buyu ukalamba mchanga, waseme ni siku imefika?

Kuna nchi life span ni 80yrs, sisi sijui tumefikia ngapi sasa ila mara mwisho naona ilikuwa 49, sababu za kutofautiana huko ndo hizo sisi tunazoita SIKU IKIFIKA.
 
Hili mbona liko wazi na nimesema hapo, hata uishije my dear you'll never walk out of this world alive...!!
Hata lifespan ikiwa 500 kufa ni lazima ufe tu..!
 
Kuna watu speed kwao sio issue and they feel normal kabisa ila kuna kina sisi Nyota za Punda speed kali ni adui kwetu.
 
Zile gari zisikie tu nilipanda kuwahi miadi na mganga wa Jadi Moshi.. aisee nilijitoe kbs ufahamu nililala nikasema liwalo na liwe. Tukafika Mkata Trafiki akatuuliza eti gari linakimbia tukamjibu hapana. Manina yule dereva alivaa kofia kama Ndumilakuwili hana story na mtu bati bati Moshi nadhani tuliingia saa 10. Asubuhi nikawahi kwenye ulozi wangu. Saa 11 jioni mganga akanisindikiza njia panda. Ile nafika tu pale nakutana na chombo ile ile inageuka dereva akanijua maana sikubadili nguo. Nikazama pale Makanya na ule upepo yule chizi alipita na 120. Saa 5 ama 6 hivi akatushusha Ubungo. Uwa nawaza sana ule ujinga niliofanya. Mganga kala kuku na deal nikakosa halafu nusu kibarua kiote nyasi. ONYO USIPANDE GARI LA GAZETI hasa yale maroli ya Posta na simu yenye bodi nyekundu. Kuna mzee nadhani alijikojolea hiyo Dar Mbeya.
 
Kwan huwa wanatumia gari za aina gan?
Ist, kluger, hiace, au? Maana licha ya mwendo mkali Ila sijawah kusikia ajali zinazohusu izo gari za magazeti.
Ajali ni chache. Iringa ilichinja 9,
images (2).jpeg
images (3).jpeg
images (1).jpeg
 
Aiseee zile gari acha kabisa

Yani kabla hujakaa tayari upo Kibaha mana Dar - Moro ni lisaa tu 😂😂😂😂

Kupanda zile gari inahitaji uwe na roho ya paka 😆😆😆

Sishauri kabisa wanawake kupanda zile gari mana sisi wanaume tu tunapanda kwa dharura

Embu tupe uzoefu wako mara ya kwanza kupanda zile gari ulijiskiaje
Balaa lingine ni zile gari zinabeba mirungi hapo Kenya 🇰🇪. Zile pickup na probox zinatembea balaa, zigo isije sinyaa maana inapakiwa alfajiri kutoka Meru saa 3 asubuhi nchi nzima iwe imefikishiwa. Zipo makala za NTV Kenya juu ya miraa drivers.
Miraaaa
Miraa cle drivers
 
Kwan huwa wanatumia gari za aina gan?
Ist, kluger, hiace, au? Maana licha ya mwendo mkali Ila sijawah kusikia ajali zinazohusu izo gari za magazeti.
Ni miezi sasa ilitokea ajali hakuna aliyepona nafikiri ni watu 11 walipotea
Ilikuwa inaenda mbeya au iringa

Kupanda hizo gari ni jambo moja na kucheza na shilingi chooni lolote linaweza kutokea mda wowote
 
Nadhani ndo maana tunakwama, Mungu katutia akili tujishughulikie, sisi tunajitoa akili kusubiri afanye miujiza.

Ajali zinaweza epukika mpaka kuleta maana halisi ya ajali.

Barabara za ovyo, mwendo wa ovyo, unachokimbiza ni cha ovyo...Dar-Moro tu, taa za kuangaza barabara ziko maeneo gani labda?

Ukila buyu ukalamba mchanga, waseme ni siku imefika?

Kuna nchi life span ni 80yrs, sisi sijui tumefikia ngapi sasa ila mara mwisho naona ilikuwa 49, sababu za kutofautiana huko ndo hizo sisi tunazoita SIKU IKIFIKA.

Nadhani Traffic wanajua, Wana siasa wanajua.

Hivi haya tunayofanya hata wenzetu wanafanya hivyo? Hivi hakuna namna ya kufanya printing huko huko bila kupeleka kwa gari, au ndo tuko comfortable na hii

Anyway, mtoa mada kataka mwenye experience na kupanda gari hizo.
 
nikipanda segera saa 11 jion, saa mbili kasoro nilikuwa ubungo mataa shel zilipokuwa zinapak
 
Mleta mada acha chai ww mwenyewe umeskia stori tu huna lolote unajua usidanganye jamii
 
Nilipanda la mwananchi nilikua nawai interview arusha, dar tuliondoka saa 6 usiku arusha saa 12
Sasa zina tofauti gani na bus kipindi ambapo hakukua na tochi na usimamizi mkali barabarani maana ulikua ukipanda ngorika au buffalo kipindi hicho cha ligi unatoka dar 12 kamili saa sita kasoro unakula mtori arusha
 
Nakumbuka 2011 niko Makambako..nikaenda sehem flani karubu na Mizani kuna ka stendi ka gari za private wale madalali wkananambia midaa hii ya saa 7 mchana tutakusimamishia Gari ya Gazeti...[emoji17]ninachokumbuka tu ni kwamba tulitoka pale Makambako saa 8 kasoro mchana

Ile gari nakumbuka ilikuwa ni Isuzu Pick up Suka alikuwa anaongelea kuiwahi mechi ya Barca na Man U fainali ya UEFA .Tulipiga sana Story za Mpira kuhusu hiyo Kechi mapaka kufikia saa 1 usiku tulikuwa tushafika maeneo ya Kibamba Dar

Njiani Matrafiki walikuwa wanarushiwa Bundle ya Magazeti chuma inapita

N.B: Usipande zile gari kwa usalama wa Maisha yako na kama unajipenda
 
Back
Top Bottom