Ushenzi wa vikwazo wanaoumia ni wananchi

Ushenzi wa vikwazo wanaoumia ni wananchi

Natty Bongoman

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2008
Posts
403
Reaction score
191
Vikwazo vya kiuchumi na kufungia pesa imekuwa ni silaha ambayo imetumiwa mara kadhaa na mmarekani na wenzake. Hii silaha ilianza miaka ya 1950 hivi na Korea kaskazini.

Wakaja Iraq, Iran, Venezuela…hata Zimbabwe wamo. Nchi wenza wa mmarekani hazijawahi kuwekewa vikwazo hata zikitenda madhambi yanayofanana na waliowekewa vikwazo.

Kila wakati, sababu ya vikwazo tunaambiwa ni kuhamasisha wananchi mapinduzi ya yule kiongozi wasiempenda wao wamarekani (hata kama wananchi wanampenda).

Tunaimbiwa walivo wema na wala hawana nia ya kuumiza wananchi – mara nyingine wakitamka ‘wananchi si maadui zetu ni viongozi’. Cha kushangaza miaka yote hii, kama sote tunavoona, nao lazima wanaliona, ni kwamba hata mara moja vikwazo havijafanikisha lengo lao la mapinduzi kupitia wananchi.

Tumeshatambua (wengi wetu) kwamba wanawekea vikwazo nchi zenye viongozi, aidha ni wababe ama wanakubalika na wananchi wao. Hili swala nao si wajinga wanalitambua.

Kwa hilo naona ni silaha ya kibaguzi pia, kwa maana wanajua wananchi watafyata mkia ila wacha wateseke – hatuwajali. Data za wazi zinaonyesha kwa kila mtu namna vile vikwazo vinaathiri huduma za umma hadi za kiafya, kipato na Maisha ya mwananchi kiujumla.

Kwanini linaendelea kurudiwa kama si ubaguzi? Imefika mahali vikwazo vinachanganya kichwa – kwa mfano, “umekomboa” Iraq, umeweka viongozi wako… afu bado unawawekea vikwazo, aumie nani? Ndo kujengaje nchi ivo ama uliikomboa kwa nini??

Hii video hapo chini ni taarifa ya Habari kutokea uturuki. Kwa kweli unaona wazi vikwazo vinavofeli lengo na kuumiza wananchi hadi Watoto wachanga kupona kabla ya miaka 5.



Kama umeangalia video – jamani muafghanistan nae ni binadamu… Huyu mmarekani wengine mnasifia mambo yake kuhusiana na vita vya Ukraine, vile anavolipia gharama kibao kumuokoa muUkraine… ndie yule yule leo hii anamemfanyia muafghanistan, yafuatayo:

  • Kamkuta mwananchi asiehusika na Taliban anavumilia fujo anajifanyia vibarua vyake anadunduliza hela zake ndani ya benki (NMB zao). Benki za Afghan zikiamini sheria za kimataifa za biashara, zinatunza hizi hela za wananchi kule marekani (labda kwa amri manake mmarekani alikuwa anakalia nchi). Sasa kaamua kutelekeza ama kashindwa vita anaondoka. Anafika kwao anaamua na anatamka Hela za wananchi zimefungiwa. Hawana ruksa kupata hela zao!!!
  • Vikwazo vinambana muafghan - wakati wanakufa njaa, wanakufa magonjwa hakuna madawa, huduma za umma hazipatikani, hakuna kipato cha msingi… wanahitaji hela zao lakini bado wananyimwa, na mashirika ya “misaada” yako busy kwa miezi kadhaa wanajadili eti watoeje msaada ili Taliban asiguse hela… wananchi wanaendelea kuumia na kufa na kuomba hela zao
  • Mara sasa wanaambiwa kuna uamuzi mpya - nusu ya hela zao zilizofungiwa zitatumika kuwalipa wahanga wa 911 wamarekani waliomshtaki Taliban. Sijui wenzangu, mimi sikujua kulikuwa na kesi hii. Jamani kwani hela ya wataliban hiyo? Ubaguzi huu, ingekuwa hela ya waingereza lisingekubalika swala hili…
Hii pointi ya mwisho imenifanya nipekue kidogo nipate orodha ya wahusika wa majanga ya 911 niangalie walihusika… kutoka link hapo chini

September 11 Hijackers Fast Facts

Hijackers by Nationality

Egypt
Mohamed Atta

Lebanon
Ziad Jarrah

Saudi Arabia
Ahmed al Ghamdi
Hamza al Ghamdi
Saeed al Ghamdi
Hani Hanjour
Nawaf al Hazmi
Salem al Hazmi
Ahmad al Haznawi
Ahmed al Nami
Khalid al Mihdhar
Majed Moqed
Abdul Aziz al Omari
Mohand al Shehri
Wail al Shehri
Waleed al Shehri
Satam al Suqami

United Arab Emirates
Fayez Banihammad
Marwan al Shehhi
 
Back
Top Bottom