DOKEZO Ushetu Health Center hutoza pesa wajawazito kwa ajili ya kliniki

DOKEZO Ushetu Health Center hutoza pesa wajawazito kwa ajili ya kliniki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari,

Kuna changamoto katika kituo cha afya Ushetu kata ya Ushetu halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga ambapo mama wajawazito hulazimika kulipia gharama kwa ajili ya huduma ya kliniki.

Mama anayeanza kwa mara ya kwanza kliniki ya ujauzito hulipia kuanzia 20000 na zaidi kwa ajili ya huduma, baada ya hapo kila hudhurio analazimika kwenda na kati ya 5000 mpaka 10000 kwa ajili ya huduma ya kliniki kwa mjamzito.

Nimekuwa nikisikia sera na kauli za wizara na serikali kwamba huduma za mama na mtoto ni bure.

Niliwapigia wizara kupitia 199 nikaambiwa huduma hizo ni bure. Je hawa wahudumu wa USHETU HEALTH CENTER utaratibu huo wameelekezwa na nani?

Kama ni utaratibu wa serikali siku hizi basi jamii uambiwe hadharani,isiwe ni mambo ya kukutana nayo eneo la huduma halafu jukwaani tunahubiriwa vinginevyo kama ilivyo kwa REA kumwambia mwananchi umeme ni 27000 vijijini kumbe vijijini kama mjini tu.

Mke wangu ana mimba ya miezi 5 na sijampeleka mpaka angalau ibakie miezi 3 kupunguza gharama. Hii ni kwa sababu kwa miezi 9 kila hudhurio ukilipia ni sawa na gharama ya 40,000-90,000, ambayo ni kubwa kwa wasio na bima.

Siku ya kujifungua napo kuna kununua vifaa vya kujifungulia ambavyo pia zamani vilikuwa vinapatikana bure.

Tupazie sauti, taifa lijue hili si sawa.
 
Mimba Ina miezi 5, mjamzito bado hajaanza kliniki, halafu tunategemea vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka 5 vipungue, yaani tunachekesha.
Mkuu, wewe kwa usalama wa mkeo na mtoto, tafuta hela umpeleke mkeo kliniki, akipata matatizo aje afariki wakati wa kujifungua,hakuna atakaekuja kukusaidia. Weka mambo ya bure pembeni ,uzazi ni suala la kufa na kupona, hakuna cha bure hapa nchini. Ungefahamu hali halisi wanazopitia wahudumu wa afya hasa katika mazingira hayo, usingeuliza kwanini wanatoza hela.
Sasa endelea kusikiliza wanasiasa ambao wake zao wanapelekwa kujifungulia nje ya nchi tena wanalipiwa mamilioni uone kama watakusaidia mkeo au mtoto wakipata matatizo.
 
Habari,

Kuna changamoto katika kituo cha afya Ushetu kata ya Ushetu halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga ambapo mama wajawazito hulazimika kulipia gharama kwa ajili ya huduma ya kliniki.

Mama anayeanza kwa mara ya kwanza kliniki ya ujauzito hulipia kuanzia 20000 na zaidi kwa ajili ya huduma, baada ya hapo kila hudhurio analazimika kwenda na kati ya 5000 mpaka 10000 kwa ajili ya huduma ya kliniki kwa mjamzito.

Nimekuwa nikisikia sera na kauli za wizara na serikali kwamba huduma za mama na mtoto ni bure.

Niliwapigia wizara kupitia 199 nikaambiwa huduma hizo ni bure. Je hawa wahudumu wa USHETU HEALTH CENTER utaratibu huo wameelekezwa na nani?

Kama ni utaratibu wa serikali siku hizi basi jamii uambiwe hadharani,isiwe ni mambo ya kukutana nayo eneo la huduma halafu jukwaani tunahubiriwa vinginevyo kama ilivyo kwa REA kumwambia mwananchi umeme ni 27000 vijijini kumbe vijijini kama mjini tu.

Mke wangu ana mimba ya miezi 5 na sijampeleka mpaka angalau ibakie miezi 3 kupunguza gharama. Hii ni kwa sababu kwa miezi 9 kila hudhurio ukilipia ni sawa na gharama ya 40,000-90,000, ambayo ni kubwa kwa wasio na bima.

Siku ya kujifungua napo kuna kununua vifaa vya kujifungulia ambavyo pia zamani vilikuwa vinapatikana bure.

Tupazie sauti, taifa lijue hili si sawa.
 

Attachments

  • 1000020485.jpg
    1000020485.jpg
    12.1 KB · Views: 8
Mzee baba utazalisha watoto mapooza kwa kuogopa gharama. Siungi mkono hizo tozo za kliniki ila peleka mkeo kliniki.

Wife niliacha kumpeleka clinic private ili kukwepa gharama. Mimba ya mwisho mwezi wa kwanza hosp ya gvt tuliacha elf90. Baada ya hapo ikawa kila mwezi sio chini ya 30k.
 
Huo ndo utaratibu kwa hospital zote Tanzania.
Clinic unapoanza lazima uweke mpunga kwaajili ya vipimo muhimu vya jumla baada ya hapo clinic kila mwezi andaa 7,000 kwa hospital za serikali kwa ajili ya kipimo cha mkojo na damu.
Kinachotolewa bure ni dawa za muhimu za kipindi cha ujauzito, muda mwingine neti pia hutolewa bure.

Dawa upewe bure,
Vipimo bure,
Uzalishwe bure,
Mtoto asome bure.

Tumia uzazi wa mpango kwa kipindi hiki ambacho CCM wapo madarakani
 
Jamani ifikie wakati tujue tunafanya nini!!? sio kukurupuka tu.
Sasa unalalamika gharama za clinic na mtoto ni wako???? hayo mambo ya bure ni mapambo ya wanasiasa lakini huduma haziko bure na hiyo ni hospital zote......
Mimi binafsi sipendi hizo huduma za bure na ni bora ulipie upate huduma stahili kwa mama na mtoto!!!!.

Nasisitiza tuzae/ tupate watoto tunapokuwa na u tayari wa kubeba majukumu ya malezi kuanzia mimba mpaka kiumbe.
 
Kwa nini mnataka mpewe huduma za kliniki bure ??
 
Mkiwapa mimba Muwape Na Hela.. Mwanaume Mzima Unasema Huna Hela ya Kliniki .. Utaweza Kununua Pampas kweli na Maziwa ya Unga Kama Mama Akikosa Maziwa Wew
 
Back
Top Bottom