Prof Sankara
Member
- Sep 17, 2021
- 6
- 10
Utangulizi
Ushindani ni namna ya kupima uwezo, uzuri, uimara, umaridadi, au ubora baina ya pande mbili kwa kutumia vigezo takikana.
Ili kupata mshidi husika vigezo huzingatiwa kupima pande zote mbili. Kupima uwezo wa akili kwa mtu, ujuzi, wake katika Nyanja Fulani lazima akidhi na kudhihirisha uhalisia wa ujuzi wake au uwezo wake katika kitu husika kwa kufanya kwa vitendo.
Ushindani na hamasa
Katika Nyanja ya elimu uwezo wa kiufahamu, ujuzi, kumbukumbu hupimwa kwa kutumia mtihani. Ambapo mwanafunzi anayepata majibu sahihi kwa kwenye mtihani husika ndiye huwa mshindi dhidi ya wengine.
Wanafunzi darasani hukaa na kujifunza pamoja kwa muda Fulani kisha mwalimu huwapima kama wameelewa somo husika kwa kuwapa mtihani. Nia ya mwalimu ni kuona kama wanafunzi wameelewa somo na wanaweza kutumia maarifa hayo katika maisha yao ya kila siku.
Mwanafunzi anayefeli somo husika hupewa adhabu kama njia ya kumfanya aogope adhabu kwa kujibidisha kusoma zaidi ili asije akafeli tena wakati ujao.
Adhabu inaweza kumfanya kumchukia mwalimu na somo husika, wakati mwingine kuwa na uvivu wa kuhudhuria vipindi kwa kuogopa adhabu iwapo atafeli somo la mwalimu huyo.
Tofauti ipo kwa mwanafunzi aliyefaulu ambapo huyo atapewa pongezi na zawadi za kutosha. Mwanafunzi huyo atajisikia vizuri na kuhamasika kuendelea kujibidisha kusoma ili awe anapata pongezi na zawadi kutoka kwa watu wanaomzunguka kama walimu, wazazi, walezi, ndugu na marafiki.
Kwa maelezo haya tunapta hoja mbili tofauti ambazo ni hamasa na ushindani. Mwanafunzi aliyefaulu mtihani hupata hamasa ya moja kwa moja kutokana na zawadi na pongezi kutoka kwa watu wanaomzunguka. Ambapo hamasa hiyo humfanya kuwa na bidii kwa kufahamu kuwa akishinda tena atapata zawadi pengine zaidi ya wakati huu. Huwa na hamasa ya ushindani kwa sababu tayari anatambua na ameshaonja uzuri wa kushinda mtihani.
Mwanafunzi aliyeshindwa hukosa hamasa ya moja kwa moja ikiwa kushindwa kwake kutaambana na adhabu kadha wa kadha kutoka kwa wazazi au walimu wake. Watoto wanapokuwa shuleni kujifunza mambo mbalimbali hujengwa katika mtazamo wa kushindanishwa hasa katika ufaulu wa mitihani darasani kuliko nyanja zingine za maarifa kama vile michezo, uchongaji, kucheza densi, kuzungumza, kuchora, kukimbia, kulenga shabaha, na bunifu mbalimbali.
Wajibu wa mwalimu na mzazi/mlezi katika hamasa na kukuza kipaji kwa mtoto.
Mwalimu anawajibika kuhakikisha kwamba mtoto anafurahia shule bila kujali kama anafaulu au hafanyi vizuri katika masomo. Wajibu wa mwalimu ni kumwelekeza na kumwongoza mtoto katika njia ziwazo zozote za kitaaluma ili kumfanya mwanafunzi ajione ana kitu cha tofauti na cha maana ndani yake.
Hivi karibuni kuna mwalimu wa shule ya msingi huko mkoani Mara Yusuf Pangoma ambaye amejidhihirisha kwa mbinu zake za kufundisha watoto.
Hucheza na watoto katika michezo ya kitoto, huwapa zawadi na kuwanunulia sare za shule baadhi yao, huwapa vifaa vya kujifunzia wanapokuwa hawana, zaidi ya hayo huwatia moyo na kuwahamasisha kuwa wanatakiwa kufanya vizuri mitihani yao.
Kwa mfano huu mwalimu ana nafasi kubwa sana ya kugundua kipaji cha mtoto na hivyo itarahisha kumfunza mtoto katika eneo lake la asili la hamasiko la ndani, yaani kitu ambacho mtoto anakionesha kukifurahia anapokuwa shuleni au nyumbani.
Mzazi hali kadhalika, anapaswa kumfanya mtoto afurahie shule kwa kumpa zawadi na hamasa za namna tofauti bila kujali anafanya vizuri au la katika mitihani yake.
Kinachokubalika na wengi wetu ni kwamba zawadi na hamasa huongeza juhudi katika kufanya kitu kile ambacho zawadi au hamasa imetolewa kwayo. Na adhabu inaweza kumkosesha mtu hamasa au kumfanya kuwa na hamasa kwa kuiogopa adhabu. Adhabu kwa mtoto hasa shuleni inaweza isiwe njia sahihi ya kumfanya mtoto kufurahia masomo na shule.
Hitimisho
Upo mpango wa serikali unaoitwa Communinity rehabilitation program (CRP) ambao ni mpango maalumu wa kurekebisha watoto wanaokinzana na sheria na walio kwenye hataari ya kikinzana na sheria. Njia za marekebisho kwa mtoto zinazoelekezwa na mpango huo siyo adhabu wa jela bali ni kumpatia mtoto elimu maarifa ambayo inaweza inampa ujuzi kamilifu. Kama vile ufundi nguo, umeme, bomba, uashi, na stadi mbalimbali za maisha ambapo akitoka katika hatua hiyo hawezi tena kuwa na tabia za kihalifu au za kikinzana na sheria badala yake anakuwa na mwenendo mwema kwa jamii yake.
Hapa mtoto anarekebishika pasipo kutumia adhabu yeyote na anakuwa mtu mwenye maadili. Njia kama hizi zikitumika kumfunza mtoto shuleni zinamfanya kuwa huru sana kuweza kupata maarifa stahiki kuliko kutumia adhabu kama njia ya kumpa hamasa kwa kuogopa adhabu.
Vipaji kwa watoto ni rasilimali kubwa ambayo lazima itambuliwe na kulelewa vizuri ili kuwafanya wathamini vipawa na uwezo walio nao katika hali ya utoto na kamwe hataacha bali ataendelea kujionesha na kukifanyia kazi katika maisha yake.
Wazazi na walezi, walimu wanatakiwa kuwatia moyo watoto katika chochote wanachokionesha na kukifanya vizuri iwe katika masomo au vitu vingine tofauti. Kama vile michezo na sanaa. Na inapobainika kuwa hicho ndicho apendacho mtoto, inatakiwa kuanza kuoneshwa taswira nzima na faida ya hicho, jinsi kinavyoweza kusababisha mtoto kuwa mtu wa namna Fulani katika jamii yake na kumletea mafanikio.

Attachments
Upvote
1