Elections 2010 Ushindi kwa CUF

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Asilimia 99.95 ya wakazi wa Zanzibar wanasubiri siku ya kuapishwa kwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Raisi kiongozi wa Zanzibar mpya(New Zanzibar).Habari za ndani zinasema kuwa uhakika wa ushindi kwa mgombea huo hauna utata.

Ni wazi kabisa tunasubiri siku ya kuapishwa kwa Raisi huyo mpya ,alisikika mkazi mmoja wa Baraste kipande huku akiendelea kusema kuwa ..unaona hata kampeni safari hii tumeziweka pembeni kwani hazihitajiki na tutazifanya kama kuondoa jiwe kwenye njia lakini si kitu cha ulazima,maana Raisi tumeshamjua sasa kampeni za nini ? Alihoji.

Huku wakazi wengi wakisema mwaka huu dunia itashuhudia kuanguka kwa CCM huko Zanzibar na huo ndio utakuwa muendelezo wa kuanguka kwa CCM Tanzania nzima ,kwani mengi huanzia Zanzibar na kuishia Tanganyika.Mkazi mmoja wa Nyarugusu alidai kuwa uchaguzi huu utaweka historia kwa kuanguka kwa CCM katika nafasi zote akimaanisha kuanzia Uraisi ubunge uwakilishi na nyenginezo(Udiwani) kuna wasiwasi mkubwa kuwa ccm hawataambulia kitu chochote maana hawapo.
 
Hata wale mamluki walioletwa kuja kupiga kura tokea mwaka jana wameshahama na kurudi kwao bara na wale wauza karanga na taulo mitaani hatuwaoni sana siku hizi.
 
acheni hizo, uchaguzi bado na chochote chaweza kutokea.

maana CCM wapo na CUF wapo na wana nguvu zenye kufanana kwa hio si jambo la kulitabiria kirahisi namna hio
 
SASA MUUNGANO VIPI..?!! BARA CHAMA KINGINE VISIWANI CHAMA KINGINE.. PATAMU HAPO..? HEBU SUBIRI TUONE:becky::becky::becky:
 
Much as I wish that to happen, but it is a deal done - Madevu can't make it. Majambazi yamempeleka mjini.
 

HALAFU UNAMALIZIA...."MARA NIKAAMKA KUMBE NI NDOTO"..tehe tehe tehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…