Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Asilimia 99.95 ya wakazi wa Zanzibar wanasubiri siku ya kuapishwa kwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Raisi kiongozi wa Zanzibar mpya(New Zanzibar).Habari za ndani zinasema kuwa uhakika wa ushindi kwa mgombea huo hauna utata.
Ni wazi kabisa tunasubiri siku ya kuapishwa kwa Raisi huyo mpya ,alisikika mkazi mmoja wa Baraste kipande huku akiendelea kusema kuwa ..unaona hata kampeni safari hii tumeziweka pembeni kwani hazihitajiki na tutazifanya kama kuondoa jiwe kwenye njia lakini si kitu cha ulazima,maana Raisi tumeshamjua sasa kampeni za nini ? Alihoji.
Huku wakazi wengi wakisema mwaka huu dunia itashuhudia kuanguka kwa CCM huko Zanzibar na huo ndio utakuwa muendelezo wa kuanguka kwa CCM Tanzania nzima ,kwani mengi huanzia Zanzibar na kuishia Tanganyika.Mkazi mmoja wa Nyarugusu alidai kuwa uchaguzi huu utaweka historia kwa kuanguka kwa CCM katika nafasi zote akimaanisha kuanzia Uraisi ubunge uwakilishi na nyenginezo(Udiwani) kuna wasiwasi mkubwa kuwa ccm hawataambulia kitu chochote maana hawapo.