Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Mkuu utamaliza maandiko ni lini wapenda sifa za kidunia waliwahi kuwa na hofu ya Mungu nafsini mwao?
 
Watanzania wanalalamika ati mashindano ya haki, yaani JPM ndio aliyebadilisha mfumo wa uchaguzi? Je, hiyo tume iwe na kina nani? Nani wasimamie uchaguzi Tanzania? Je, tutafute wageni waje kusimamia chaguzi zetu? Labda wengi hawaelewi mfumo wetu wa uchaguzi ni kama wa UK. Yaani tulichukua mambo mengi kutoka kwa wakoloni wetu, wasimamizi wa uchaguzi UK ni Halmashauri za wilaya yaani Borough Councils zilizo mijini na County Councils hao ndio wamepewa dhamana. Wanaofanya kazi siku za uchaguzi wengi wao ni wafanyakazi wa Halmashauri hizo pamoja na raia yoyote atakayeomba kuwa moja ya wafanyakazi kwenye uchaguzi kupitia halmashauri hizo kwa malipo ya ile siku.

Vyama vya upinzani hawana nia nzuri na hii nchi kwa sababu, mfano Chadema hawana uwazi jinsi wanavyotumia ruzuku wanayopata kila mwezi ya 350 million, yaani ni kugombea ruzuku, nawahakikishia next round kwa jinsi JPM anavyotenda kazi ruzuku yao itapungua kutokana na kutokupata kura nyingi kwenye urais. Vyama vya upinzani kama kweli wanataka kuing'oa CCM lazima wawe na demokrasia ya kweli kwenye vyama vyao kwanza.

Mambo ya kashfa kwenye mitandao hayataweza kuing'oa CCM madarakani uwazi na demokrasia ya kweli kwenye hivi vyama vitaweza kuiondoa CCM ni ushauri wa bure tu, vile vile waache kuwakumbatia mabeberu kwa sababu hakuna hata mzungu moja anayependa kuona ngozi nyeusi inafanikiwa kuwazidi weupe.
 
...na jafo anaweza kurudishwa kisarawe kulima mihogo ili jiwe aaminike na watz wengi walivyo mabegwe watamshangilia mzalendo
Huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza tatizo na kulitatua ili apate umaarufu zaidi. Sitashangaa nikisika Dr Abasi akisema “Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli amewasamehe wote waliojaza fomu kimakosa”.
 
Ki ukweli kabisa ccm bila wakurugenzi,vyombo vya dola na tume ya uchaguzi hawawezi kabisa kushinda pamoja na wewe kushabikia madege reli na vingine ulivyovitaja watanzania wamechoka na utawala wa manyanyaso wa ccm,watu sasa hivi hawana uhuru kila mmoja kabanwa mpaka mbavu wananchi hawana pa kupumlia wasimamizi wa uchaguzi inavyoonekana wamepewa maelekezo kuvuruga uchaguzi ili tu ccm yao ishinde kwa kishindo kitu ambacho kimenyima wananchi wengi haki ya kuchagua au kuchaguliwa na wananchi wao.Mpaka kufikia hapo ccm imekosa haki ya kutawala kwa kufuata katiba na sheria.
 
Kama Magufuli angekubali democrasia ishamiri TZ, he would have been the best president in Africa history.
 
Upo sahihi mkuu,,,

Imani imetoweka[emoji16]
 
"Law of probability," inakataa kuwa katika makundi mawili mathalan yanajaza form zilizo sawa na wajazaji wa makundi hayo wawili wanafanana kwa kila hali katika sifa zao pakawa makosa yawe yanafanywa na kundi moja tu.
Umesema vyema sana, ni hujuma za wazi zenye nia ovu.
 
Pascal umesema vizuri lakini unajaribu kusifia ili tu kufikirisha watu. Hii mizengwe si bure inatokana na hofu na tamaa. Kwa mujibu wa wewe una maana waliofanya mizengwe ni vipofu wasioona ukweli uliosema? Yaani hayo mavitu mareli, midege ... Kwa nini mkimbiaji anafika mwisho na washindani wake wako mbali lakini anamwaga miiba ili wapinzani wakwame huku yeye anamalizia mbio na tayari ushindi anauona.
 
Naona Mkuu unataka kuwaingiza force king kimtindo, busara nyiiiiingi[emoji23][emoji23][emoji23] hawawezi kukubali ushindani huru na wa haki ng'ooo manake wanajua hilo ndo litakuwa anguko lao.
 
Mawazo ya wasaka tonge yanajulikana kwa kutetea kwa kila hali dhuluma inayofanywa,Kuna uwezekano mkubwa wanaotete ubinywaji huu wana maslahi yao binafsi ili tu waendelee kushibisha matumbo yao na kuyaweka pembeni maslahi ya wananchi wengi.
 
Binafsi swali nililonalo kichwani kwangu siku nyingi halijawahi kupata majibu. Nalo ni hili: Hivi ni kwa nini CCM huwa inaogopa sana sanduku la kura? Maana kila unapoitishwa uchaguzi wowote CCM inakosa raha kabisa! Itaomba kuhakikishiwa ushindi toka mamlaka mbalimbali kama vile NEC, jeshi la polisi, n.k. Tatizo ni nini? Wakiwa majukwaani wana CCM wanaimba mafanikio makubwa ya utawala wao, lakini wananchi hao hao wanaoambiwa hayo mafanikio hawaaminiki kama wataichagua CCM. Tatizo ni nini? Je,kwani hayo mafanikio wananchi hawayaoni?

Binafsi nilifikiri CCM wangetamani kuwe na uchaguzi kila siku ili waudhihirishie umma kukubalika kwao kwa wananchi.
 
Paskali! wewe mwenyewe unaandika kwa tahadhali kubwa sana, kuwaogopa watu wasiojulikana! Nani atathubutu kuichagua CCM na Serekali yake yenye vitisho vilivyomfanya kila MTZ kuishi kwa hofu Kuu? Hata wewe mwenyewe Paskali ukiwa kwenye chumba cha kupigia kura huwezi kuthubutu kuichagua CCM. Paskali ukiichagua CCM, akili ya kuku itakuwa imeizidi akili yako kwani kuku akili yake imekuwa imekuwa ikimsaidia kuchukua tahadhali dhidi ya Mwewe.
 
MBunge Sanga anautaka ukuu japo hata wa wilaya
 
Pascal wakati mwingine huwa unanishangaza, unasema Magufuli aingilie kati suala hili wakati ndo mastermind wa tatizo? wale watendaji walipoitwa ikulu hukusikia au ulikuwa nje ya nchi? hata kama ulikuwa nje ya nchi mitandao ipo definitely habari uliipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…