Ushindi mzuri sana kwa Simba SC kutujengea ujasiri Mechi ya Robo Fainali

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Salaam wana Msimbazi,

Niwapongeze wote kwa ushindi mzito na mnene tulioupata leo dhidi ya timu ya Horoya kutoka Guinea.

Muhimu ushindi huu mzito tulioupata nyumbani, tutambue utaamsha ari ya mashabiki na wachezaji wa Simba SC, hasa tukielekea mechi yetu ya robo fainali, wajue kwamba hakuna kisichowezekana chini ya jua, juhudi na nidhamu ya kazi ndio siri ya vyote.

Ushindi huu mzito utawatisha hata wapinzani wetu, sasa watajua Tanzania kuna timu inaitwa Simba SC, ikiwa nyumbani kwake kaa nayo mbali ni kama moto wa gesi.

Hii ni pasipo kujali mpinzani wetu atakuwa nani, Nguvu Moja.
 
Wydad Casablanca, Esperanse Tunisia au Mamelodi Sundowns a.k.a Masandawana.

Hongera kwa ushindi mtani, ila hapo mbele kuna aibu inakusubiri. Sio ajabu ukafanyiwa kama ulivyomfanyia Horoya!
 
Mamelodi huu moto wa simba nadhan hataman kuonana nao..
Moto wa mabua ndio umtishe mamelod? Mkishindaga uwa mnakuwa na maneno meeengiii kama wauza karanga, kwaiyo kumfunga kibonde horoya ndio mmejiona bayern munich mnaanza kujilinganisha na mamelod!
 
Naona ushindi dhidi ya kibonde horoya umewalevya, Subilini majibu yenu mtayapata siku sio nyingi
 
Mamelodi Sundowns wanawasubili, kama nyinyi mna paka wale wana snake.

Habari zao waulize miamba Al Ahaly watakueleza vizuri.
 
Naona kuna vibwengo vimedandia huu uzi ili kuharibu furaha yetu..
Asee bora mshuke wenyewe tu[emoji23][emoji23]uto naona kama wanateseka sana
 
Wydad Casablanca, Esperanse Tunisia au Mamelodi Sundowns a.k.a Masandawana.

Hongera kwa ushindi mtani, ila hapo mbele kuna aibu inakusubiri. Sio ajabu ukafanyiwa kama ulivyomfanyia Horoya!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hawa sisi level zetu na ndo maan tuko wote Robo final.
 
Moto wa mabua ndio umtishe mamelod? Mkishindaga uwa mnakuwa na maneno meeengiii kama wauza karanga, kwaiyo kumfunga kibonde horoya ndio mmejiona bayern munich mnaanza kujilinganisha na mamelod!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nachekaaaa km mwehuuu.
Wee utakufa kwaa pressure. Meza kwan panadol kutuliza maumivu.
 
Simba bado timu mbovu
Najua hizi gori 7 atazilipa kwa Raja Casablanca
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daaaaah sio kwa maumivu hayooo.
Poleeeeeeh
 
Mamelodi Sundowns wanawasubili, kama nyinyi mna paka wale wana snake.

Habari zao waulize miamba Al Ahaly watakueleza vizuri.
Wao Mamelody ndo wakawaulize Al Ahly kuhusu Simba.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…