Pre GE2025 Ushindi wa Lissu na Uchumi wa Tanzania

Pre GE2025 Ushindi wa Lissu na Uchumi wa Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

noisi

New Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Natanguliza pongezi za dhati kwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu kwa kuaminiwa na kukabidhiwa Kijiti kuongoza chama kutoka kwa Freeman Mbowe.

Lissu anafahamika kwa harakati zake za kitambo katika kupigania lile analoliamini na kulisimamia.

Katika kampeni zake za kugombea uenyekiti wa chama alijinasibu kama mpinga rushwa na ufisadi.

Sikumbuki kama Mwenyekiti mpya alishawahi kuainisha “roadmap” ya ukombozi wa kiuchumi kwa nchi kama jinsi ambavyo anapigania “Haki”.

Waswahili wanasema mkono mtupu haulambwi, ukishashiba kwanza ndio utaanza kuwaza mambo mengine.

Kuna kundi kubwa la vijana halina ajira, kuna kundi kubwa la watoto linalokuwa kwa kasi ambao soon watakuwa nguvu kazi.Hawa, hata wakizipata hizo “Haki” ila wasipopata “Mlo wa uhakika” nchi haitatulia.

Hawa ukiwapa wachague option ya kwanza kati ya “ Haki na usawa” au “ Mlo kwanza” nina uhakika watachagua “Mlo kwanza”.

Hivyo jambo la kwanza na la muhimu kwa Mwenyekiti ni kutoa suluhisho la kiuchumi kwanza sababu ni jambo la msingi na la muhimu sana.

Democarcy sio chakula, haitafuta matatizo ya kiuchumi na ya umasikini wa Tanzania automatically.Kwa maneno mengine Democracy sio muarobaini wa uchumi wa nchi hata kama kama itakuwa practiced in the highest order.

Tunahitaji kuzifahamu sera mbadala za kiuchumi kutoka upande wa pili (Upinzani) ili tupime tujue mrengo wao utaweza kutatua matatizo ya kiuchumi kwa kiasi gani.

Naungana mkono upiganiaji wa haki na siudunishi kwa namna yoyote ila upinzania nahisi wamejisahau kuelezea “sera” mbadala wamebakia kuwa wakosoaji zaidi tena kwa mambo ya kisiasa bila kutoa suluhisho la mambo ya kiuchumi.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom