Pre GE2025 Ushindi wa Lissu unamaanisha nini kwa Watanzania? Tunapata picha gani Uchaguzi Mkuu 2025? Samia atapumua? Ukabila kuisha?

Pre GE2025 Ushindi wa Lissu unamaanisha nini kwa Watanzania? Tunapata picha gani Uchaguzi Mkuu 2025? Samia atapumua? Ukabila kuisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Safi sana. Umma umeshinda na sasa tukijenge chama kwa moyo safi
 
Wakuu,

Lissu amekuwa akiongelewa kama mtu mwenye misimamo, aliyenyooka, na siyo rahisi kuyumbishwa. Yeye na Heche imekuwa pea moja ambayo inaendana kwa kwenye misamamo na njia zao za kuongoza wote wakiongelea mabadiliko makubwa ndani ya chama na maeguzi kwenye siasa za Tanzania.

Baada ya ushindi wa Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti CHADEMA na Heche kama Makamu wake, inamaanisha upinzani utazidi kuimarika na kuongeza siasa safi nchini? CCM itaacha kuzembea na kuongeza nguvu kwenye kuongeza ubora wa huduma ili kuendelea kubaki madarakani?

Mchuano wa Uchaguzi Mkuu utakuwa moto na Samia kuhenyeshwa kwelikweli? Vipi ubande wa ubunge, unawaona upinzani wakipata viti vingi na kuwa na bunge lenye uwakilishi mkubwa pamoja na mchuano mkali hoja zitakapokuwa zinaletwa mezani?

Vipi ushiriki wa Watanzania kwenye masuala ya siasa? Tutegemee ushiriki mkubwa wa wananchi kwenye siasa na uchaguzi Mkuu?

Wazee wa kitengo usema TAL ni shida sana
 
Bila kupepesa macho kama uchaguzi mkuu utakuwa wazi na huru kama huu wa chadema Samia ndio basi tena atastaafishwa. Mifumo ya nchi ijiandae tu kisaikolojia kupokea mabadiliko ya kisiasa
 
Back
Top Bottom