Ushindi wa Mayweather utata

Kwa wale wasiojua ngumi......kurusha ngumi
nyingi sio ndio wingi wa point....je ngumi zako
zinafikia target zenye kukuwezesha kupata
point....??


PACMAN ni kama alitumia style ya kurusha
mangumi kama njia ya kujilinda lakini si kwa
lengo la kushambulia lakini mzee wa misifa
alikuwa anashambulia...kwa maana ya kwamba
kila ngumi yake ilikuwa ina hit the target......kwa
wale wanaojua mchezo wa ngumi teknikale
watakuwa wameshanielewa....


defence skills ya PACMAN haiko makini ndio
maana huwa anatumia muda mwingi kutupa
makonde...akiwa na malengo mawili kushambulia
huku akimfanya adui asimkaribie....

lakini pia ana
udhaifu katika kurusha ngumi za aina ya
hook....na uppercut.......anatumia muda mwingi
kurusha jab ambazo kwa bondia makini kama
Mayweather haziwezi kuwa na madhara......

kitu
kilicho mnyima ushindi PAC MAN ni kurusha
ngumi nyingi zisizo na muelekeo huku akikosa
umakini katika kuimarisha ulinzi ,hali iliyofanya
Mayweather kushambulia huku akiwa na uhakika
wa kulenga target kila apatapo
nafasi.....

kushambulia muda mwingi kwa kutumia
jab pekee kumemfanya Mayweather kuwa huru
mchezoni.....na kufanya counter attack zenye
mafanikio..........
 

Waambie mkuu...

wengine ndo wameangalia ngumi kwa Mara ya kwanza Leo baada ya kusikia " THE FIGTH OF THE CENTURY"

Manny kapigwa...mayweather katumia staili ya Mourinho tuu hahaaa..
 
hivi nyinyi mnaolalama humu mnajua masumbwi kweli? mnaiijua 10 point must scoring system? maana kuna watu wanadhani.swinging wildly wins you the fight!! hamjui tu
 

Hamna asiejua kwamba ukirusha ngumi nyingi haina maana ya kupata point nyingi ,umeona takwimu zilizotolewa kwamba Mayweather ndio aliyerusha ngumi nyingi
Hili ni kweli ???????????? Kama ulifuatilia pambano vizuri round ya 1-6 ilitosha kuonyesha Man PAC ndie karusha ngumi nyingi kuliko Mayweather achalia mbali hizo round sita zilizobaki
Anyway jamaa ashashinda hata tukikesha hatutaweza badili historia
Man PAC lost the match but he won so many hearts if you know what I mean
 

Maneno yako ni ya kweli,ila si kwa pambano lao!

Namkubali maney, kabla ya mchezo nilijua ana sifa za kushinda game!

Ila kilichotokea sicho,
Ni kweli may ni fundi wa kukwepa na kulenga target.
Ila kwa leo..

Bila mapenzi binafsi,utaifa,ubabe wa wamerekani,kamari/ubaguzi!

Weather alipoteana.

Na matokeo yamenifanya ghafla,nimpuuze japo namkubali.maana siwezi simama upande wa dhurma,japo pia cwezi badilisha matokeo!
Hata angepewa ndroo angekuwa kapendelewa!

Ila ni wazi WENYE NGUVU WALIUNGANA KUMKABILI MNYONGE!

Kila mtu na mtazamo wake.

Umesema kitaalamu na kiuzoefu!

Ila kiuhalisia weather leo kachemka na ndio bingwa,hakuna tunachoweza badilisha katika hili!
 
Mambo ya ki freemason tu..maywether yupo kwenye kingdom hakutakiwa aangushwe this tyme ila muda ukifika man pac akikubali kuwa raia wa us naye atapewa hiyo kingdom..secret behind the scene and mission was planned
Hawezi kukubali huo ujinga ManPac. Bora aache ngumi
 
Sasa ndio umemwaga utorojo gani huu. Si umejaza server za jf bure wewe?
 
mayweather hajarusha ata panch tano kwa pac
Soma chini hapa uone record ilivyo

Pacquiao wasn't aggressive enough. Mayweather actually threw more punches - 435 to 429 - and landed with 39% of them, compared to 19% for his opponent. But because Mayweather was throwing on the back foot, people were fooled into believing he sucked the life out of the fight.
 
Mchezo Wa ngumi una sheria zake sio kutupa ngumi nyingi bila mpango zitakupa ushindi kumbuka unaweza kutupa ngumi chache ukazipance kiufundi ngumi za mpinzani ukapata ushindi ndicho alichokifanya may weather leo
 

Kama hujui kitu ni busara sana kuuliza mkuu!
In short wewe mchezo wa boxing inaelekea hujui. Pole.
 
Moneyman kashinda kwa point ingawa watu wengie wanaonekana kutokuridhishwa na ushindi huo. Katika mapambano ya ngumi point hupimwa na idadi ya ngumi zinazotua usoni na kichwani. Ngumi zote zinazoangukia kwenye glovu, tumboni na sehemu nyinginze za mwili huwa hazihesabiwi. Ingawa Pacman alitupa ngumi nyingi sana zikiwemo combinations kadhaa, sehemu kubwa ya ngumi hizo ilikuwa inaangukia kwenye glovu za Moneyman, wakati ngumi za Moneyman nyingi sana ziliangukia usoni mwa Pacman.
 
Kama hujui kitu ni busara sana kuuliza mkuu!
In short wewe mchezo wa boxing inaelekea hujui. Pole.

Mkuu utamaliza nguvu zako kubishana na watu ambao hushabikia ushindi through emotions
Achana nao
Floyd ndo 48-0
 
[21:42, 5/3/2015] Ndupe: Mwandishi mkongwe wa BBC ambaye amewahi kucheza boxing zamani Ndugu Erick David Nampesya ametoa maoni yafuatayo kuhusu pambano la Mayweather na Pacquiao. Akiongea kwa kutumia utaalamu wake wa ndondi amesema;
"Ngumi za sasa ni biashara. Katika kukumbatia kwa yule "mswahili" zaidi ya Mara mbili alipaswa kukatwa point. Jambo la ajabu eti ameshinda round zote, wakati Mimi nimeona kashinda 8,9 na 10.
Anyway ndio matokeo, lakini binafsi nililpoona "mfilipino" ameshindwa kumdondosha jamaa hadi round ya 6, nikajua lazima atamaliza na wakimaliza tu Maywether atatangazwa mshindi (that was planned).
Njia pekee ya kumzuia Myweather kutangazwa mshindi ilikiwa kumpiga KO au kuhakikisha hamalizi raundi zote. Lakini kumaliza raundi zote ni advantage kwake maana points hawezi kupewa mfilipino.
Kama unaijua ndondi lazima utashangaa Mayweather kutangazwa mshindi wakati yeye alikua anajihami zaidi badala ya kushambulia. Na aliposhambulia alitumia zaidi "jab" wakati Mfilipino alikua anatumia the "jab" mara chache ila mara nyingi alitumia "cross", "hook" and "uppercut". Lakini marefarii kama hawakuona vile.
Unajua mchezo wa leo, ulikuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 300. Sasa uchezwe Las Vegas, Majaji wote wa hapo Nevada, Kisha ashinde mfilipino?? Wamarekani wasingekubali.
Wameandaa mazingira ya Re-march iwapo mheshimiwa mbunge Pacqiao atakubali. Lengo ni kumsaidia Mayweather kutunza rekodi yake. Alisema anataka kustaafu akiishavunja rekodi ya Rocky Marciano ya kushinda mapambano 50 bila kupoteza.
Kumbuka leo amefikisha 48-0, yaani bila kupoteza pambano lolote. Kwa hiyo kinachofanyika ni siasa tu za ulingoni ili rekodi hiyo ya 50-0 iweze kufikiwa."
Haya wale waliojiita wataalamu wa ngumi waje kusema Mayweather alicheza "jab" ngapi, "cross" ngapi au "uppercut" ngapi.!
[21:44, 5/3/2015] Ndupe: Watu wanamaneno eti ngumi zingechezwa PTA sabasaba na hakuna kamba za ulingo basi May weather tungemkamatia mbagala kibondemaji.. 🏃🏃🏃
 
Mkuu umeniibia coment yangu...niliipost asubuhi kwenye uzi wa BAK
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Hahahahahahaha lol! wizi wa comments umeanza JF, njemba inachukua mzoo bila hata kubadili hata kidogo au kutoa credit kwa muhusika na hivyo kujionyesha kama yeye ndiye mwandishi. Pole Mkuu KikulachoChako niliisoma hii comment yote na kukupa like.

Mkuu umeniibia coment yangu...niliipost asubuhi kwenye uzi wa BAK
 
Last edited by a moderator:
Statistics hizi zitsaidia kuamua ni nani alistahili.

Yaani hizi takwimu sielewi wamezitoa wapi?
Kama hawakuja nazo kabisa basi wamebadilisha.points za may kapewa pac na za pac kapewa may. Maana ukitoa mapenzi binafsi tu,may kapigwa na ndio mshindi.
Hatuwezi kubadilisha ila ukweli ni kapendelewa.

Mitambo ipo kuchukua picha,ila points wanahesabu watu/majaji.ambao wawili kama sio wote ni wamarekani.na hawatumii mitambo kuangalia poits ,wanatumia macho yao.

M.weather mmarekani.waandaaji wamarekani,pambano limefanyukia marekani.
Majaji wamarekani.

Ndio maana hawaona hata tabu kufanya dhurma!

WENYE NGUVU WAMEUNGANA KUMKABILI MNYONGE.
 
Kama watarudiana mywether ajiandae na kichapo hana uwezo nilijua atashinda kwa ko kumbe jamaa yuko fit balaaa.

Hawezi kukubali marudiano,hili lenyewe kasumbua sana.
Sijui alikua hataki/anaogopa/anadharau? Hata cjui?

Mwisho wa siku chai imeungwa chumvi,na watu wamekubali kuinywa.watafanyaje sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…