Ushindi wa Simba Nyumbani kuipatia Tiketi ya Nane Bora

Ushindi wa Simba Nyumbani kuipatia Tiketi ya Nane Bora

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Simba ya Tanzania inajivunia ushindi wa nyumbani wa asilimia 100 ya Caf Champions League na inaweza kuandikisha record ya kuingia robo fainali kwa kuwafunga wageni As vita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mchezo utakafanyika Jumamosi hii.

Mabingwa wa mara nane Al Ahly wa Misri na JS Saoura wa Algeria wanafukuzia pia nafasi ya kuingia robo fainali katika mchezo wao wa kundi D wa mashindano haya ya CAF yenye hadhi kubwa sana katika Afika

Saoura ipo juu kwa pointi nane ambapo Ahly na As Vita Club wana point saba wakati Simba wana pinti sita, hata hivyo mpangilio huu unaweza kuwa tofauti kabisa baada ya michezo miwili ya mwishoni mwa wiki.

Ahly, klabu nyingine iliyo na rekodi ya asilimia 100 katika mechi za nyumbani inatarajiwa kuishinda Saoura huko Alexandria na kumaliza ya kwanza katika kundi D. Simba inaweza kutoka nafasi ya mwisho hadi ya pili kama itaifunga As vita na kulipiza kisasi kipigo cha bao tano ilichokipata huko Kinshasa miezi miwili iliyopita.

Tunapitia sasa mechi hizi za sita (siku ya sita) zinazojuisha vilabu 11 vinavyotarajiwa kujiunga na mabingwa Esperance wa Tunisia na Mamelodi Sundowns wa Afrika Kusini ambao tayari wameshaingia nane bora

Kikundi A

Wakati Sundowns wameshafulu robo fainali, nani atayemaliza wa kwanza katika hili kundi na kama Wydad Casablanca ya Morocco au ASEC Mimosas ya Ivory Coast nazo pia zitaendelea robo fainali ni suala litakaloamuliwa na mechi za mwishoni mwa wiki

Waafrika Kusini wanahitaji sare tu dhidi ya Wydad kubaki mshindi wa kwanza wa kundi hili wakati ASEC wanacheza ugenini na Lobi Stars ya Nigeria wanaopaswa kupata matokeo yaliyo bora ili kupata nafasi ya ushindi pili wa kundi hili

Sundowns na ASEC wanajivunia wachezaji wao walio katika kiwango bora Themba Zwane na Amed Toure wanapotafuta ushindi ushindi wao wa kwanza wa ugenini wa mashindano haya.

Kikundi B

Esperance imeshajipatia tiketi ya robo fainali shukrani kwa ushindi wao wa mara tatu wa nyumbani na sare mbili walizozipata ugenini wanawaacha Horoya wa Guinea na Orlando Pirates ya Afrika Kusini kuipigania nafasi moja iliyobakia katika kundi hili.

Kocha wa Milutin Sredojevic wa Serbia amekuwa akiwakumbusha wachezaji wake juu ya walichokifanya mwaka wa 1995, wakati klabu hiyo ilipoishinda ASEC huko Abidjan kushinda kikombe kilichokuwa kikiutwa wakati huo Kila bingwa za Afrika

Lakini Horoya ya Guinea iliyo na wachezaji kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Mghana Ocansey Mandela ipo juu ya Pirates kwa pointi moja na kwa vile wanachezea nyumbani mechi yao ya mwisho, wana nafasi bora zaidi ya kusonga mbele.

Kikundi C

Mabingwa wa mara tano TP Mazembe kutoka DR Congo ambao kama Simba na Ahly wana rekodi ya ushindi wa nyumbani wa asilimia 100 ukiwapo ushindi wao wa kihistoria wa goli 8-0 dhidi Club Africain kutoka Tunisia; wanajiandaa kuwashinda CS Constantine ambao wamefanikiwakupata pointi nne tu katika michezo mitatu tangu waifunge TP Mazembe goti 3:0 huko kaskazini mwa Afrika.

Constantine wanaweza kuwa washindi wa pili wa kundi hili ikizingatiwa wana pointi tatu na wastani bora wa magoli dhidi ya Club African inayocheza na Ismailia ya Misri iliyo katika nafasi ya mwisho.

Kikundi D

Ahly wana tatizo la kipa baada ya kuripotiwa kuumia kwa kipa wa chaguo la kwanza Mohamed el Shenawy na kipa chao la pili akihifadhi Sherif Ekramy, hivyo kubakiwa kipa moja tu Ali Lotfy atakayecheza mechi dhidi ya Saoura.

Klabu hii ya Misri ambao wamekuwa washindi wa pili wa mashindano haya kwa miaka miwili mfululizo, wana rekodi nzuri ya michezo ya nyumbani ambapo wameshinda michezo yao mitatu ya awali ya makundi huku wakiwa mamefunga magoli tisa bila nyavu zao kuguswa.

Simba wanatumaini muunganiko wao wa washambuliaji kutoka mataifa mbalimbali yaani Meddie Kagere wa Rwanda, Clatous Chama wa Zambia, John Bocco wa Tanzania na Emmanuel Okwi wa Uganda unaweza kuwapatia ushindi dhidi ya waliokuwa mabingwa huko nyuma As Vita ya Kongo.

Source : Home win will lift Simba into Caf CL last-eight
 
Mungu awe pamoja nanyi as vital mtakapoingia uwanjani awape wepes wa kushinda mechi hii!!! Kila la heri as vital.
 
Back
Top Bottom