Ngoja niwape ishu ya Rombo... Ukweli ni kuwa tofauti na sehemu zingine Rombo imetengwa sana kutoka Tanzania. Kwa taarifa yenu ni kuwa Rombo hakusikiki redio yeyote ya Tanzania kirahisi ukiacha sauti ya injili (moshi). Zaidi ya 90% ya watu kule husikiliza Redio citizen na KBC za Kenya. Miaka michache iliyopita walikuwa wanapata redio one na redio free, lakini siku chache baada ya kuanza kuibuka kwa ishu za ufisadi na Mramba kutajwa, redio free na redio one zikapotea hewani (ukiacha maeneo machache ya Mkuu na Mengwe). Magazeti nayo siku hizi hayauzwi, ukiacha tu sehemu moja pale stendi ya wilayani...
Nimejaribu mara kadhaa ninapokuwa kule kudadisi kwa mfano kwa kiasi gani watu wanafaham kuhusu ufisadi... sana sana watu wahafaham fisadi Kamresh Patney (wa Kenya), na asilimia kubwa neno Rostam, Lowassa, Chenge, Karamagi na wengine kwao ni viongozi wa serikali, ni wachache, tena vijana (ambao hawapigi kura) wanaojua ni kwa nini Lowassa alijiuzulu!!!
Warombo wanaamini kuwa bado wao ni mojawapo ya sehemu zilizoendelea sana Tanzania, na hivyo wamependelewa na serikali, ukiwaambia kumpinga Mramba, hasa baada ya kuwawekea lami, ni jambo zito. Matajiri wote Rombo ni wafuasi wa CCM na mashabiki wa Mramba, ukianzia akina Maulidi Swai, Luka Mchomba, Michael Shirima (mwenye Precision air), Waha, Kanyau, John Marceli, Faida, Oisso, Lasway, Teotim 'mhindi', na wengine kwa mamia. Hii inafanya watu kuhushisha u-CCM na utajiri, hivyo inakuwa ngumu kumwelewesha mtu uhusiano kati ya CCM na umaskini wake. Kila mtu anataka awe tajiri bwana.
Angalau katika siku za karibuni kumekuwa na mwamko kidogo kutokana na watu wengi wanaotoka mijini hasa vijana kusapoti CHADEMA. Ingawa CHADEMA ilikuwa na nguvu kule lakini kitendo cha mbunge wa zamani kwa tiketi ya CHADEMA, Salakana kuhamia CCM hadharani pale Tarakea, na baada ya hapo biashara zake za kampuni ya utalii kuanza tena kufanya vizuri (zilikuwa zimedorora), kwa kiasi kikubwa kiliiua sana CHADEMA Rombo.
Nimepata habari kuwa mwaka huu CHADEMA wameweka mgombea machachari (sijamfahamu ni nani...). Binafsi namtakia kila la heri lakini namtahadharisha ajipange vizuri sana kupambana na wizi wa kura wa Mramba. Yule jamaa anatumia sana nguvu za matajiri wa kule kufanikisha kuchomekewa kwa masanduku bandia ya kura, na wakati fulani (2000), walitumia hata bastola kuescot na kutishia wale wote waliokuwa wanaleta chokochoko. Kwa maana niyo CHADEMA wanapaswa wajipange vizuri pale na wakifanya hivyo watashinda...