Ushiriki wa Bodi ya Wakurugenzi kwenye Usimamizi wa Mpango Mkakati kwa Kampuni au Shirika

Ushiriki wa Bodi ya Wakurugenzi kwenye Usimamizi wa Mpango Mkakati kwa Kampuni au Shirika

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60
1735724453605.png


Bodi ya Wakurugenzi ni chombo nadi ya kampuni au shirika chenye lengo la kusimamia maslahi ya wanahisa/wanachama kwa kuhakikisha kwamba kampuni au shirika linaendeshwa kwa kufuata misingi na taratibu zilizowekwa, ambapo Bodi ya Wakurugenzi ndio yenye jukumu la kuandaa misingi na taratibu hizo. Bodi ya Wakurugenzi inaundwa na watu wanaotokana na kampuni/shirika yaani “executive directors” pia na watu wanaotoka nje ya kampuni/shirika yaani “non-executive directors”, watu hawa wanaweza kuwa wakurugenzi wa mashirika mengine, wanasheria n.k.

Kwenye usimamizi wa Mpango Mkakati wa kampuni au shirika, Bodi ya Wakurugenzi inapaswa kushiriki kikamilifu ili kuleta matokeo tarajiwa. Majukumu ya Bodi ya Wakurugenzi kwenye eneo hili yamegawanyika katika sehemu kuu tatu, ambazo ni;​
  • Ufuatiliaji (Monitoring): Kupitia kamati zake mbalimbali, Bodi ya Wakurugenzi ina jukumu la kuhakikisha mipango, miradi na sera zitokanazo na Mpango Mkakati zinatekelezwa kama zilivyoapangwa.
  • Kutathmini na Kushawishi (Evaluate and Influence): Bodi ina jukumu la kutathmini mapendekezo ya programu, miradi na hata sera zinazowasilishwa na “Management” na ikibidi kushauri ili kuboresha au kutoa mapungufu yanapoonekana.
  • Kupendekeza Mikakati (Initiate Strategies): Bodi ya Wakurugenzi pia ina jukumu la kupendekeza mikakati kwa “management” ya kampuni au shirika ili kampuni au shirika husika liweze kutimiza malengo yake. Kimsingi mikakati hii inayopendekezwa na Bodi ya Wakurugenzi lazima itokane na dhima au “mission” ya kampuni au shirika.
Kiwango cha ushiriki wa Bodi ya Wakurugenzi kwenye majukumu yote haya matatu niliyoainisha hapo juu yanatofautiana kutoka kampuni/shirika moja na jingine. Ushiriki wa Bodi kwenye majukumu haya unaweza ukawa kwenye hali ya chini kabisa, hali ya kati au hali ya juu kabisa, na hapa ndipo zinapatikana Bodi zenye nguvu na Bodi zisizo na nguvu. Mwandishi Thomas L. Wheelen kwenye kitabu chake cha Strategic Management and Business Policy ameainisha kwamba kiwango cha ushiriki wa Bodi za Wakurugenzi kwenye majukumu haya unaleta aina mbalimbali za Bodi, ambazo ni;
  • Phantom Board of Directors: Hii ni Bodi ambayo haijui lolote linaloendelea ndani ya Kampuni au Shirika, kifupi Bodi ya namna hii haishirikishwi chochote na “Management” ya Kampuni au Shirika.
  • Rubeber Stamp Board of Directors: Hii ni aina ya Bodi ya Wakurugenzi ambayo haina kikwazo kwa maamuzi yoyote yanayofanywa na “Management” na mara nyingi hufanya kile inachoambiwa na “Management”
  • Minimal Reviewing Board of Directors: Hii ni aina ya Bodi ya Wakurugenzi ambayo angalau ina uwezo wa kupitia maamuzi na mapendekezo ya “Management”, ila ni kwa baadhi ya mambo tu yanayohusu kampuni au shirika.
  • Nominal Participating Board of Directors: Hii ni aina ya Bodi ya Wakurugenzi ambayo pia ina uwezo wa kupitia maamuzi na mapendekezo ya “Management”. Utofauti wa Bodi hii na Minimal Reviewing Board ni kiwango cha mambo yanayoletwa mezani na “Management” . Bodi hii inashirikiswa kwenye mambo mengi ukifananisha na Minimal Reviewing Board.
  • Active Participating Board of Directors: Hii ni aina ya Bodi ambayo inapitia mapendekezo na maamuzi ya “Management”, inahoji uhalali wa maamuzi hayo na wakati mwingine inakuja na mapendekezo yake. Bodi hii ina kamati maalum kwa ajili ya ukaguzi wa matumizi fedha ya kampuni au shirika.
  • Catalyst Board of Directors: Hii ni aina ya Bodi yenye nguvu zaidi ukifananisha na Active Participating Board. Bodi hii inashiriki kikamilifu kwenye uandaaji na uboreshaji wa dira, dhima, malengo na mbinu za kampuni au shirika. Kamati zake pia zina nguvu kuzidi kamati za Active Participating Board.
Utafiti uliofanya na McKinsey mwaka 2021 unaeleza kwamba kampuni au mashirika yenye Bodi za Wakurugenzi zenye nguvu yaani “Catalyst Board of Directors” zilifanya vizuri kwa asilimia 30% ukifananisha na kampuni au mashirika yenye Bodi za Wakurugenzi zisizo na nguvu. Pia ripoti ya KPMG ya mwaka 2022 inaonyesha kwamba kampuni au mashirika yenye Bodi za Wakurugenzi zenye nguvu zilipunguza gharama zisizo za msingi kwenye uzalishaji kwa asilimia 25% ukifananisha na Kampuni au mashirika yenye Bodi za Wakurugenzi zisizo na nguvu.​

Takwimu na tafiti zinazoonyesha kwamba kuwa na Bodi ya Wakurugenzi yenye nguvu inapelekea mafanikio makubwa kwa kampuni au shirika ni nyingi. Hivyo basi. Ni wajibu wa makampuni na mashirika kuhakikisha kwamba si tu yanakuwa na Bodi za Wakurugenzi kama sheria zinavyotaka, ila bodi hizi lazima zipewe meno na uhuru wa kufanya maamuzi.

Article By;

OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
For Consultation Service; Call +255 719 518 367 or
Email: msongatheconsultant@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA

"NAPENDA KUKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2025"
 
Back
Top Bottom