Ushiriki wetu michezo ya Olympic

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Tumepeleka wanamichezo 7 tu mashindano ya Olympic zanu hii, yawezekana ukosefu wa fedha, lakini pia, ni kushindwa kuandaa washiriki katika michezo kadhaa. Ninawaza michezo ambayo makabila mengi ni maarufu kama:

1) Kuogelea - makabila yanayojihusisha na uvuvi kama kwenye maziwa (Victoria, Tanganyika, Nyasa, nk) mito (Mara, Rufiji, Kilombero, Ruvu, Ruvuma, nk), bahari ya hindi.
2) Mikuki na mishale - makabila yanayojihusisha na ufugaji na uwindaji, kama Wasandawe, Wagogo, Wanyaturu, Wamasai, Wabarbaig, nk.
3) Mbio ndefu - makabila yaishio milimani km Wapare, Wachagga, Wameru, Wanyakyusa, nk.

Kinachohitajika ni kukuza vipaji vya vijana huko kwa mipango mikakati badala ya urembo, sanaa, nk kama ilivyo kwa sasa.
 
Baiskel - Wasukuma, tanga
Mieleka, Ngumi- wasukuma, wanyamwezi, wakulya
 
Wanyakyusa walivyo mabonge hivyo wataweza kukimbia?
 
Mbeya kuna Rungwe, Chunya na Tukuyu, huko je mbio ndefu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…