Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Kitendo hiki kimepingwa vikali na China, na pia kimesababisha mvutano ndani ya Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na ukosoaji kutoka Ujerumani, Hungary na nchi nyingine, na upinzani kutoka kwa sekta husika za kiviwanda. Pande nyingi zinaamini kwamba vitendo vya kujilinda kibiashara haviwezi kuleta faida kwa upande wowote, na ushirikiano unanufaisha pande zote.
Katika kura za maoni kuhusu mswada huo, nchi wanachama 10 wa Umoja wa Ulaya zilipiga kura 10 za kuunga mkono, 5 za hapana, na nyingine 12 hazikupiga kura. Ujerumani ndiyo nchi mwanachama mkuu wa Umoja wa Ulaya inayopinga mswada huo. Hapo awali, Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz alielezea matumaini yake ya kusuluhisha mvutano na China kupitia mazungumzo, na kusema mswada huo hautaleta faida kwa sekta ya magari barani Ulaya.
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ushawishi wa Marekani, Umoja wa Ulaya umeiweka China kama “mshirika, mshindani na mpinzani”. Baadhi ya wataalam wa Umoja huo wanaona kuwa, kuegemea Marekani kupita kiasi kutaathiri uhuru wa Ulaya katika masuala ya kimataifa, na badala ya kuleta manufaa kwa Ulaya, kutaharibu taswira yake ya kimataifa.
Awali, watu wengi wa Umoja wa Ulaya walionya kuwa vitendo vya kujilinda kibiashara vitadhuru maslahi ya Ulaya. Tarehe 9 mwezi Septemba, ripoti ya “Matarajio ya Ushindani wa Umoja wa Ulaya” iliyotolewa na Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mario Draghi kwa idhini ya Rais wa Tume ya Ulaya Ursulla Von der Leyen, ilifuatiliwa na nyanja zote barani Ulaya.
Ripoti hiyo ilitaja umuhimu wa ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya Umoja wa Ulaya na China, na kupendekeza Umoja huo kuchukua sera zinazofaa zaidi, ili kuepuka mzozo na China kutokana na vitendo vya kujilinda kibiashara. Katika nyanja za teknolojia mpya kama vile nishati safi, bidhaa za China zina ubora wa juu na bei nafuu, na zinaweza kusaidia Umoja wa Ulaya kufikia malengo yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Soma Pia: China yailaani Tume ye Umoja wa Ulaya kwa kutaka siri za kibiashara katika uchunguzi wa magari ya umeme
Draghi alisisitiza katika kongamano lililofanyika nchini Ubelgiji kuwa, Ulaya ni tofauti na Marekani, na bara hilo haliwezi kujenga ukuta wa kujilinda kibiashara. Alisema ili kuepuka kuanguka katika mtego wa kujilinda kibiashara, utungaji wa sera za kibiashara za Umoja wa Ulaya unapaswa kulingana na hali halisi, na kuendana na lengo la jumla la ukuaji wa Umoja wa Ulaya.