Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Malawi wazidi kung'ara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
IMG_20201007_170344_578.jpg
IMG_20201007_170344_576.jpg
✍🏽

TUKIWA tunaelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 28 Oktoba, 2020, Leo Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli amempokea Mhe Rais Lazarus Chakwera wa Malawi pamoja na ujumbe wake aliyekuja Tanzania kwa lengo la kufanya mazungumzo kuhusu kuimarisha mahusiano baina nchi hizi mbili hususan katika biashara na uchumi. Katika hotuba yake Rais Magufuli amesema;

Biashara kati ya nchi zote hizi mbili zimekuwepo na hivi karibuni biashara zimeanza kupanda ambapo mwaka 2015 zilikuwa zinakadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 60 hadi mwaka 2019/2020 ambapo zimeongezeka na kufikia Dola za Kimarekani Milioni 80 - 81.

Hadi sasa Kituo Cha Uwekezaji nchini Tanzania, kimesajili miradi 8 kutoka Malawi ambayo imeajiri watanzania wapatao 390, pia kuna makampuni ya Tanzania ambayo yamekwenda kuwekeza katika nchi ya Malawi yakiwemo ya Azam group, Mohamed Interprises na Mount Meru.

Mpaka sasa, Bandari ya Mtwara inafanyiwa ukarabati mkubwa ambapo kwa sasa expansion yake ina uwezo wa kubeba takribani tani 400 elfu na itakapofika mwezi Disemba mwaka huu itakuwa na uwezo wa kubeba tani milioni moja hivyo kupelekea kurahisiha biashara baina ya nchi hizi mbili.

Katika kuhakikisha mawasiliano na usafiri wa kuwezesha nchi ya Malawi, amesema, sehemu zote zilizokuwa zinasumbua kwa upande wa Malawi zenye takribani km 52 sasa zinajengwa kwa lami, na lami imekamilika aslimia 95. Barabara hii ina jumla ya km 82.7 kutokea Songwe - Ileje hadi kwenye mpaka wa Malawi, ambapo kukamilika kwakwe kutaleta fursa ya kutumika kama njia mojawapo ya kawaida kwenda Malawi.

Nchi hizi mbili zinapanga kushirikiana katika uzalishaji na mgawanyo wa Megawatt za umeme kwa kuzingatia kuwa nchi ya Malawi inakabiliwa na tatizo kubwa la Power, yaani kuwa na mahitaji makubwa ya umeme kuliko Megawatt zinazozalishwa.

_”Tanzania kwa sababu hivi karibuni tutakuwa na Megawat zaidi ya 5,000 tumezungumza na Mhe Chakwera kwamba zingine tunaweza kuwapatia Malawi wakati tunasubiri Megawat za Development ya Songwe Basin ambayo itatoa Megawat 180 ambazo zitagawanywa katika nchi hizi mbili”_alisema.

Aidha Rais Magufuli ametilia mkazo suala la mshikamano baina ya nchi za Afrika, kwa kusisitiza kuwa tunapaswa kusimama imara na kujikita zaidi katika kukuza uchumi wetu kama waafrika ili tuweze kujiimarisha sisi wenyewe kwa sababu hatuna ndugu wengine wa kuwategemea.

_”Ndugu zangu Watanzania na Wana Malawi, this is the special opportunity God has given us, we are supposed to move together, we are supposed to consider the best issue of economic development, we have no brothers, we have no fathers, we are supposed to move as Africans”_alisema.

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo yamehusisha pia kuimarisha mahusiano katika masuala ya Madini, Uvuvi, Biashara, Uhamiaji, Utalii, ukusanyaji wa mapato pamoja na ushirikiano katika uzalishaji wa mazao mbalimbali likiwemo zao la korosho.

#ChaguaMagufuli2020
#T2020JPM
 
Malawi ni masikini mno wana GDP kama ya 7 Billion, hiyo ni ndogo mno kuliko turnover ya kampuni kama Monsanto
 
Cha ajabu kwacha moja ya malawi ni sawa na tshs 3,hivi ni kwanini?
 
Kenya watanuna
 
Nimemuona Kabudi nikakumbuka ile dawa ya madagascar iliyofuatwa na ndege
 
Back
Top Bottom