Ushirikina ni kitu kinachochangia sana watu kuogopa kurudi vijijini kwao kipindi cha likizo

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Muhimu: kufanya mila za tamaduni mfano kuchinja mbuzi na kutumia damu katika shughuli za kienzi tamaduni haya ni mambo ambayo yapo karibu kila kabila, huu sio ushirikina bali ni tamaduni. Hapa tunazungumzia ushirikina kama kupigana vipapai (kurogana), kuamka mwili umepigwa chale, kusumbuliwa usiku, n.k.

Katika kipindi cha likizo huwa inafaa sana mtu kwenda kwao kusalimia ndugu au hata kupeleka watoto ili wajijue na kuwa karibu na asili / chimbuko lake lakini hali imekuwa tofauti sana.

Changamoto kubwa ya kurudi huko inayofanya watu wengi hasa wa mjini kuogopa kurudi makwao ni hofu ua ushirikina / kurogwa.

Mtu anaweza akawa ana nauli kabisa ya kwenda hata kwa ndege kwao lakini hofu ni kubwa sana kiasi kwamba watoro wanaweza wasijue hata wazazi wao wametokea wapi.

Kwa tafiti nlizofanya nmeona kuna makabila ambayo yanahesabika kwa mkono moja ambayo hayanaga mambo ya ushirikina na kiukweli hawa watu hawanaga hofu kurudi makwao muda wowote wanaotaka, Hawa ndio wanafanya mila kama kila kabila lakini mambo ya ushirikina hayana nafasi huko makwao,
 
Kabila gani mkuu ambalo halina hofu ya kurudi kwao?
 
Vijijini uchawi ndio utamaduni mkuu.. mgeni kulishwa 'vyaajabu' ndio hofu kuu. Uchawi pia ndio umefanya maisha ya vijijini yabaki yalivyo toka enzi na enzi, hakuna maendeleo.. anayeibuka kiuchumi wanamuibukia[emoji58]
 
Halafu hao hao wanakuwa wanakupiga majungu kwamba amekataa kwao, hataki kurudi kusalimia nyumbani kisa amesoma au anafanya kazi, biashara....ukijichanganya tu wanalala na wewe, halafu unakuta ni ndugu zako wa karibu, walozi ni shida sana nchi hii....
 
Katika kipindi cha likizo huwa inafaa sana mtu kwenda kwao kusalimia ndugu au hata kupeleka watoto ili wajijue na kuwa karibu na asili / chimbuko lake lakini hali imekuwa tofauti sana.

Changamoto kubwa ya kurudi huko inayofanya watu wengi hasa wa mjini kuridi makwao ni hofu ua ushirikina / kurogwa.

Kwa tafiti nlizofanya nmeona kuna makabila ambayo yanahesabika kabisa kama sio moja kabisa ambalo halinaga mambo ya ushirikina na kiukweli hawa watu hawanaga hofu kurudi makwao muda wowote wanaotaka.
Kweli kabisa kwetu songea toka niende 2015 sijaenda tena natamani niwe naenda lkn naogopa mambo ya kishirikina vijana hawajishughulishi wao kulewa na wengine kurithi mikoba wakiwa wadogo.Nimemic sana home ila nikiwaza niliyokua nikiyaona na kusikia naogopa kurudi
 
Ni wale ambao kila krismas ni lazima warudi kwao.
Wanarudi kwao kufanya matambiko/maagano ..watarogana vipi wakati wanaendeshwa Na mizimu...?!

Ndio maana wengi wako Roman hakunaga kukemea mapepo...hawataki unafiki...

Kimya kimya.. ...

Na wanafanikiwa maana wanafata masharti...kushinja kimburu!!

Siyo mizimu Na uchawi wa kishamba ...wasingekuwa Na maendeleo...

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa kwetu songea toka niende 2015 sijaenda tena natamani niwe naenda lkn naogopa mambo ya kishirikina vijana hawajishughulishi wao kulewa na wengine kurithi mikoba wakiwa wadogo.Nimemic sana home ila nikiwaza niliyokua nikiyaona na kusikia naogopa kurudi
Yaani alafu wakisikia umetoka mjini wao wanajua kwamba ushatoboa maisha na mchawi hapendagi maendeleo, hapo ni kujiandaa kuamka mwili umepigwa vichale ama kusikia watu wanakimbia juu ya dari usiku,
 
Wanarudi kwao kufanya matambiko/maagano ..watarogana vipi wakati wanaendeshwa Na mizimu...?!

Ndio maana wengi wako Roman hakunaga kukemea mapepo...hawataki unafiki...

Kimya kimya.. ...

Na wanafanikiwa maana wanafata masharti...kushinja kimburu!!

Siyo mizimu Na uchawi wa kishamba ...wasingekuwa Na maendeleo...

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
soma vizuri maada neno kwa neno
 
Kweli kabisa kwetu songea toka niende 2015 sijaenda tena natamani niwe naenda lkn naogopa mambo ya kishirikina vijana hawajishughulishi wao kulewa na wengine kurithi mikoba wakiwa wadogo.Nimemic sana home ila nikiwaza niliyokua nikiyaona na kusikia naogopa kurudi
Kweli kbs mkuu, huku kwetu Songea wana mambo ya ajabu sana, sisi tulimzika baba yetu mpendwa 2016, mwaka 2017 tukaenda kujengea kaburi lakini baada ya hapo ndio imekua nitolee yaani. Wao ndio wanawezana ila sisi tuliokulia mjini tunahofia maana afadhali basi hata kama ndugu yako ni mwanga basi wangekuwa wanakulinda lakini wao ndio wanakunyoosha daah!
 
Wanarudi kwao kufanya matambiko/maagano ..watarogana vipi wakati wanaendeshwa Na mizimu...?!

Ndio maana wengi wako Roman hakunaga kukemea mapepo...hawataki unafiki...

Kimya kimya.. ...

Na wanafanikiwa maana wanafata masharti...kushinja kimburu!!

Siyo mizimu Na uchawi wa kishamba ...wasingekuwa Na maendeleo...

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Hu wote ni uchawi sasa umeingia hadi makanisani
 
Kweli kbs mkuu, huku kwetu Songea wana mambo ya ajabu sana, sisi tulimzika baba yetu mpendwa 2016, mwaka 2017 tukaenda kujengea kaburi lakini baada ya hapo ndio imekua nitolee yaani. Wao ndio wanawezana ila sisi tuliokulia mjini tunahofia maana afadhali basi hata kama ndugu yako ni mwanga basi wangekuwa wanakulinda lakini wao ndio wanakunyoosha daah!
Aiseeee hii cjui hua n wivu wa maendeleo
Kwa kilekidogo unapata ama nini maana hawakuachi salama kabsa wachawi sio watu kwakweli
 
Wanarudi kwao kufanya matambiko/maagano ..watarogana vipi wakati wanaendeshwa Na mizimu...?!

Ndio maana wengi wako Roman hakunaga kukemea mapepo...hawataki unafiki...

Kimya kimya.. ...

Na wanafanikiwa maana wanafata masharti...kushinja kimburu!!

Siyo mizimu Na uchawi wa kishamba ...wasingekuwa Na maendeleo...

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Mawazo ya masikini kujifariji
 
Huwa wanarudi kutambikia mizimu ya mababu
hii ni mila ya kila kabila mkuu, tatizo huenda wewe ni mojawapo wa wahanga ambao umezaliwa mjini na wazazi wako waliogopa kukupeleka kijijini kwenu kwa hofu kwamba utarogwa.

hizi ni tamaduni mkuu, hata wahindi, wachina, n.k wanazo
 
Back
Top Bottom