Ushirikina,Unafiki wa Matajiri wa Afrika na Maisha halisi

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Matajiri wa Afrika wengi wametajirika kwa njia kuu tatu.
1. Ushirikina
2. Ushiriki Siasa
3. Ushiriki Dhulma

Na ndo maana utakuta kwa kiasi kikubwa hujaribu kuosha kikombe kwa nje ilhali ndani kunanuka uvundo.

1. Yusufu Manji - alikuwa anatumia mamilioni ya pesa kuwapeleka yanga nje na kusajili kwa gharama huku akiwalipa wafanya kazi wake pesa kidogo sana. HASA WATANZANIA.

2. Reginald Mengi alikuwa akionekana akito misaada sehemu mbalimbali huku wafanyakazi wake kwa baadhi ya Makampuni wana miezi hawajalipwa salaries.

3. Bakhresa - analipa mishahara kidogo ( ingawa tunashukuru kazini kwake anazingatia kigezo cha kutuajiri kwanza sisi) ila mishahara yake ni aibu huku akisajili na kuweka pesa nyingi azam team ambayo haina msaada mkubwa wa kiuchumi kwake.

4. Mo Dewji- angalia mishahara wanayolipwa wafanyakazi wake hasa watanzania weusi. Utasikitika.lakini anatumia mamilioni ya pesa kuwekeza simba.

Na wengine wengi wengi. Wazungu wanasema "Charity begins at home" unawezaje saidia wa nje ilhali wa ndani hali zao kiuchumi ni hali jojo?

Ndo unafiki na Ushirikina wa matajiri wengi wa nchi za afrika. Machoni kama watu.moyoni hawana utu.

Wanapenda kupita kwenye makutano makubwa ya watu na njia na kuonekana wakitenda mema na kusifiwa. Hawa ni matajiri wanafiki ambao wanaosha kikombe kwa nje wakati ndani kuna uvundo.
 
Nimesoma heading tu nikagundua hii si siasa.
 
Dada umepaniki sana. Na wewe ni mmoja ya matajiri? Ungekuwa na hoja ungemjibu tu mleta uzi. Ingekuwa vizuri .usipaniki hivyo dada yangu. 😁😁😁

Toka hapa na umbea wako
 
GuDume, Kuna tajiri mmoja anaitwa Ali Kiba, eti ni tajiri Mkubwa lakini hataki hata kujulikana wala investment zake zisijulikane. Huu kama sio ushirikina ni mbinu za ukwepaji kodi.
Sasa sijui maprodyuza wake anawalipa kiasi gani?
Bila shaka nae wimbo mmoja analipa shilling laki kadhaa .....
 
Matajiri wa Afrika wengi wametajirika kwa njia kuu tatu.
1. Ushirikina
2. Ushiriki Siasa
3. Ushiriki Dhulma

Na ndo maana utakuta kwa kiasi kikubwa hujaribu kuosha kikombe kwa nje ilhali ndani kunanuka uvundo.

1. Yusufu Manji - alikuwa anatumia mamilioni ya pesa kuwapeleka yanga nje na kusajili kwa gharama huku akiwalipa wafanya kazi wake pesa kidogo sana. HASA WATANZANIA.

2. Reginald Mengi alikuwa akionekana akito misaada sehemu mbalimbali huku wafanyakazi wake kwa baadhi ya Makampuni wana miezi hawajalipwa salaries.

3. Bakhresa - analipa mishahara kidogo ( ingawa tunashukuru kazini kwake anazingatia kigezo cha kutuajiri kwanza sisi) ila mishahara yake ni aibu huku akisajili na kuweka pesa nyingi azam team ambayo haina msaada mkubwa wa kiuchumi kwake.

4. Mo Dewji- angalia mishahara wanayolipwa wafanyakazi wake hasa watanzania weusi. Utasikitika.lakini anatumia mamilioni ya pesa kuwekeza simba.

Na wengine wengi wengi. Wazungu wanasema "Charity begins at home" unawezaje saidia wa nje ilhali wa ndani hali zao kiuchumi ni hali jojo?

Ndo unafiki na Ushirikina wa matajiri wengi wa nchi za afrika. Machoni kama watu.moyoni hawana utu.

Wanapenda kupita kwenye makutano makubwa ya watu na njia na kuonekana wakitenda mema na kusifiwa. Hawa ni matajiri wanafiki ambao wanaosha kikombe kwa nje wakati ndani kuna uvundo.
Na wewe ajiri ulipe pesa nyingi wafanyakazi waridhike
 
😂😂😂😂. Yaani matajiri wa Bongo ni kichefu chefu sana. Na alikiba naye Tajiri? Wa nini? Wanawake? Pesa? Followers?au nini?

GuDume, Kuna tajiri mmoja anaitwa Ali Kiba, eti ni tajiri Mkubwa lakini hataki hata kujulikana wala investment zake zisijulikane. Huu kama sio ushirikina ni mbinu za ukwepaji kodi.
Sasa sijui maprodyuza wake anawalipa kiasi gani?
Bila shaka nae wimbo mmoja analipa shilling laki kadhaa .....
 
😂😂😂 investment zake anazificha wapi? Ha ha ha... Hawa Matajiri wetu sometime wanafurahisha sana. Sisi wengine pia ni Matajiri wa Mademu no... i meant Madeni.

Mi naona hela zake ni kama zile hela za wafanya mazingaombwe zamani zile. Walikuwa wanatengeneza noti kutoka kwenye magazines
 
Mshahara mdgo unaanzia shilingi ngapi.?? na kama ni mdgo kwanini wasiende kufanya shughuli zao?
Mkuu uzuri wa kampuni binafsi mshahara ni makubaliano hakuna kulazimishana, na unapata kutokana na unachokizalisha na umuhimu wako kwenye kampuni husika.
 
TRA ni jibwa lisilo na meno, wangekuwa na meno, mabasi yangeambatanisha na fiscal receipt kwenye tiketi, wamiliki wa mabasi ni wakwepa kodi wa waziwazi.
Nadhani huyu mwanamuziki ni taasisi ambayo imewashinda nguvu TRA
Aisee... Hi ndo tanzania. Je serikali inatambua hilo? TRA.
 
Hawajawa na mechanism nzuri za kukusanya kodi kiuhalisia. Matajiri wakubwa ndiyo wakwepa kodi. Wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo wanakamuliwa sana kodi.

TRA ni jibwa lisilo na meno, wangekuwa na meno, mabasi yangeambatanisha na fiscal receipt kwenye tiketi, wamiliki wa mabasi ni wakwepa kodi wa waziwazi.
Nadhani huyu mwanamuziki ni taasisi ambayo imewashinda nguvu TRA
 
TRA ni jibwa lisilo na meno, wangekuwa na meno, mabasi yangeambatanisha na fiscal receipt kwenye tiketi, wamiliki wa mabasi ni wakwepa kodi wa waziwazi.

Tetesi
Mkuu sasa hivi wana mpango wa ticket ziwe za EFD, wameshawapa taarifa wahusika so siku yoyote utalisikia.
 
Hii itakuwa hatua nzuri na pengine itasaidia tatizo la kuuza ticketi mara mbili mbili kama ambavyo wengine hulalamika kutendewa.

Khofu yangu ni kuwa mzigo huo utawaangukia abiria.wenye mabasi watataka ile kodi ilipwe na abiria hivyo kama serikali haitaongilia kuweka kikomo cha bei ya juu kutakuja kuwa na shida kwenye nauli.

Tetesi
Mkuu sasa hivi wana mpango wa ticket ziwe za EFD, wameshawapa taarifa wahusika so siku yoyote utalisikia.
 
Tetesi
Mkuu sasa hivi wana mpango wa ticket ziwe za EFD, wameshawapa taarifa wahusika so siku yoyote utalisikia.
Ugali wa wapiga debe/madali wa kukatisha ticket Ubungo wanaenda kufa njaaa.
 
Back
Top Bottom