Ushirikinai wa mwenge ni uongo?

Ushirikinai wa mwenge ni uongo?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Mengi yameshasrmwa juu yake, kuwa ni uchawi wa Serikali wenye lengo la kuwafanya Watanzania watawalike!

Dini za Ukristo na Uislamu zinapinga uchawi. Hutarajii viongozi wake kujishikamanisha na shughuli za mbio za mwenge.

Kuna clip moja mtandaoni inayoonesha ufunguzibwa mbio za mwenge mkoani Kilimanjaro mwezi April mwaka huu. Katika sherehe hiyo, viongozi kadhaa wa dini waliongoza sala, wawakilishi toka BAKWATA, CCT na TEC.

MASWALI:
2. Hao viongozi hawajui kuwa mwenge ni ushirikinai au wameamua kujifanya hawajui?

2. Yanayosemwa juu ya mwenge kuwa ni ushirikina ni uongo?
 
Huo ndio utaratibu wa nchi yetu mkuu tokea awamu ya kwanza mpaka ya sita . Mganga wa rais ana hadhi kubwa kuliko sheikh mkuu ama kardinali. Japo kuwa huwa hatambulishwi hadharani
 
Iwe uchawi au sio uchawi ila binafsi sioni umuhimu wake.
Hamna impact huko unakopita, hauachi athari chanya zaidi ya athari hasi tupu.
Uuzwaji holela wa pombe chafu, ngono zembe, umalaya, kamali haramu ndio vinakua vimejaa sehemu mwenge utalala.

Kuzindua miradi si inaweza kuzinduliwa hata na mkuu wa wilaya au mkoa.
 
Hata Afisa Mtendaji wa Kata anaweza kuzindua!
 
Huo ndio utaratibu wa nchi yetu mkuu tokea awamu ya kwanza mpaka ya sita . Mganga wa rais ana hadhi kubwa kuliko sheikh mkuu ama kardinali. Japo kuwa huwa hatambulishwi hadharani
Ana hadhi kwa rais mshirikina, ila hakuna taasisi inayomtambua.
 
Back
Top Bottom