Ushuhuda: Hasara inauma asikwambie mtu

Ushuhuda: Hasara inauma asikwambie mtu

GoPPiii.

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
1,792
Reaction score
3,075
Kilio cha watu wengi kukosa ajira kilipokuwa kikubwa tuliambiwa tukajiajiri,mzee nikasema isiwe shida ngoja nijiajiri yawezekana huko ndiko utajiri ulipojificha.
Nikawaza nifanye nini,nikakumbuka Jembe halimtupi mtu tena washairi walisema kama mnataka mali mtaipata shambani. Nikajipanga nikaitafute mali shambani.
Sikuwa na mtaji hapo mwanzo,nikajibana nikapata sh kama milioni kasoro elfu 25 yaan nilikuwa na sh 975000/=. Nikashawishiwa kuingia kwenye tikiti.
Mambo yalienda vizuri,mwezi wa kwanza mazao yako vizuri,wa pili katikati ulikuja ugonjwa gani jamani daaahhhh. Ule ugonjwa Kama ulitumwa vile kumaliza hata ule mtaji mdogo niliokuwa nao tena niliojibana kwa mda mrefu.
Sikuamini ndani ya wiki moja ugonjwa ulikula mazao yote,yaani mpaka majani. Dawa zote zilidunda. Asikwambie mtu,pale ndipo nilipojua hasara inauma mazeee. Niliumia kupita maelezo ukizingatia sikuwa na pesa nyingine.
Niliyumba sio siri,nimeishi maisha ya shida sana hapo kati. Sasa hivi nina madeni kama laki tatu hivi.
Nimegundua wanaosema tukajiajiri ni wale wasiokuwa na uelewa ni jinsi gani huku kuna changamoto. Kuna kufirisika huku tena ule mtaji kidgo nao hupotea.
Asikwambie mtu hasara inauma jamani,ni noma.
Sijafa moyo,nikijipanga nitatafuta mishe nyingine.
 
Pole Sana mkuu, baada ya hapo ndo utafanikiwa Sana, ili ufanikiwe mara moja ni lazima ushindwe mara mia "By Silvester Stallone, Rambo ".
 
katka maisha yangu niliwah kukata tamaa mara moja tu. Siku niliyotaka kujinyonga halaf kamb ikakatka, nikaenda dukan kununua nyingne nikakosa mwenye duka akaniambia kama hutojali nikupe nyororo(hakujua lengo langu ila nilimuona kama asie na upendo), kuniambia hvyo na kuoa ile nyoro ilivyo nikaona isiwe tabu nikaghaili. Hio ndo mwanzo na mwisho sikat tamaa tena
 
Pole Sana mkuu, baada ya hapo ndo utafanikiwa Sana, ili ufanikiwe mara moja ni lazima ushindwe mara mia "By Silvester Stallone, Rambo ".
Nashukuru mkuu,nina imani nitafanikiwa pia hapo baadae...
 
katka maisha yangu niliwah kukata tamaa mara moja tu. Siku niliyotaka kujinyonga halaf kamb ikakatka, nikaenda dukan kununua nyingne nikakosa mwenye duka akaniambia kama hutojali nikupe nyororo, kuniambia hvyo ndo nikaona isiwe tabu nikaghaili. Hio ndo mwanzo na mwisho sikat tamaa tena
Hahahaha pole jamaa.
 
we acha tuu mkuu hasara haziko katika kilimo pekeyake...ni kote....wengine tunanyamaza tuu...kama vipi angalia mishe nyingine, kilimo kinalipa ila ukiwa na mtaji mdogo kina majaribu mengi
Mwanzo mgumu nilijuq huku kuna afadhali kidg.
 
Back
Top Bottom