Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenye duka alijua dhamira yako?katka maisha yangu niliwah kukata tamaa mara moja tu. Siku niliyotaka kujinyonga halaf kamb ikakatka, nikaenda dukan kununua nyingne nikakosa mwenye duka akaniambia kama hutojali nikupe nyororo, kuniambia hvyo ndo nikaona isiwe tabu nikaghaili. Hio ndo mwanzo na mwisho sikat tamaa tena
Kilio cha watu wengi kukosa ajira kilipokuwa kikubwa tuliambiwa tukajiajiri,mzee nikasema isiwe shida ngoja nijiajiri yawezekana huko ndiko utajiri ulipojificha.
Nikawaza nifanye nini,nikakumbuka Jembe halimtupi mtu tena washairi walisema kama mnataka mali mtaipata shambani. Nikajipanga nikaitafute mali shambani.
Sikuwa na mtaji hapo mwanzo,nikajibana nikapata sh kama milioni kasoro elfu 25 yaan nilikuwa na sh 975000/=. Nikashawishiwa kuingia kwenye tikiti.
Mambo yalienda vizuri,mwezi wa kwanza mazao yako vizuri,wa pili katikati ulikuja ugonjwa gani jamani daaahhhh. Ule ugonjwa Kama ulitumwa vile kumaliza hata ule mtaji mdogo niliokuwa nao tena niliojibana kwa mda mrefu.
Sikuamini ndani ya wiki moja ugonjwa ulikula mazao yote,yaani mpaka majani. Dawa zote zilidunda. Asikwambie mtu,pale ndipo nilipojua hasara inauma mazeee. Niliumia kupita maelezo ukizingatia sikuwa na pesa nyingine.
Niliyumba sio siri,nimeishi maisha ya shida sana hapo kati. Sasa hivi nina madeni kama laki tatu hivi.
Nimegundua wanaosema tukajiajiri ni wale wasiokuwa na uelewa ni jinsi gani huku kuna changamoto. Kuna kufirisika huku tena ule mtaji kidgo nao hupotea.
Asikwambie mtu hasara inauma jamani,ni noma.
Sijafa moyo,nikijipanga nitatafuta mishe nyingine.
Ha haaaa jamani,ni kweli?katka maisha yangu niliwah kukata tamaa mara moja tu. Siku niliyotaka kujinyonga halaf kamb ikakatka, nikaenda dukan kununua nyingne nikakosa mwenye duka akaniambia kama hutojali nikupe nyororo, kuniambia hvyo ndo nikaona isiwe tabu nikaghaili. Hio ndo mwanzo na mwisho sikat tamaa tena
Nimekupata mkuu king kong,hapo nilifeli pia,siikupata muongozo wa kutosha.Tusijidanganye kwamba lazima afeli mara kwa mara ili aje kuibuka mshindi,kwanini afeli,sikubali hii dhana ya kwamba hata warren buffett naye alifeli hapana,hapa kashasema ugonjwa ndio ulimpiga mweleka,hivi katika kilimo/ufugaji unategemea mazao yatakuwa bila kujipanga kupambana na magonjwa? Hivi unawezaje kulima bila kuweka ulinzi? Kwa wadudu na wanyama wala mazao? Ukitaka kulima lazima ujipange ukitaka kuruka agana na NYONGA...Pole kwa yaliyokukuta ila next time mtafute mtaalamu akupe elimu ya kilimo unachotaka kufanya,hata ukimpa consultation fee ndogo atakupa elimu ya zao unalotaka kulima kuepuka hasara....Lazima ujue pia msimu,Tikiti alitakiwi likianza kukua likutane na maji so usije kulima kipindi ambacho tunda linakutana na masika,hapo tena utasema mvua imeniaribia wakati huu ni uzembe.
Inawezekana pia,kuandaa ulinzi ni nzuri pia.Halafu munavyokuja shambani musije eti kwa kua una mtaji,watu in nuksi ndugu yangu.Ukianza tena jipange kila idara,Mimi nilikiwa mbishi mwanzoni baada ya kupiga hasara kama 2 hivi akili ikakaa sawa.Wanakijiji ninakula nao sahani moja mpaka wanasanda.Swali:ushawahi kulima eka 4 za Mpunga ukapata gunia 4,ambapo ulitumia mbinu zote za kilimo na mvua zilinyesha vizuri ila sikulilinda shamba n walozi.
Hujanielewa bado.sio ilinzi wa kuweka mlinziInawezekana pia,kuandaa ulinzi ni nzuri pia.
Unavyoenda kulima kijijini hakikisha umejipanga kupambana na nguvu za Giza sawaaa.unaweza kuwa na kila kitu kikakuangusha hiko tuuu!hakuna atakayekueleza jambo hili kwa kuwa wabongo wengi wanafikiInawezekana pia,kuandaa ulinzi ni nzuri pia.
Nilikuelewa vzr sana mkuu,hayo mambo yapo vijijini. Unaweza kuwa unalimia kijiji.Hujanielewa bado.sio ilinzi wa kuweka mlinzi
Unavyoenda kulima kijijini hakikisha umejipanga kupambana na nguvu za Giza sawaaa.unaweza kuwa na kila kitu kikakuangusha hiko tuuu!hakuna atakayekueleza jambo hili kwa kuwa wabongo wengi wanafiki
Poa Mkuu kilimo kinahitaji umakini sana,elimu ya mazao husika ni muhimu sana,inahitaji kufanya kiuweledi,haitakiwi kufanya bora liende,lima kisomi ili kupata tija,fuata maelekezo ya wataalamu kamwe hautopata hasara.....Nimekaa na wakulima kila stage wanapiga dawa za wadudu hata kama mazao yapo vizuri lengo ni kujikinga,wanapiga booster kila baada ya stage kwa ukuaji mzuri wa mazao.Nimekupata mkuu king kong,hapo nilifeli pia,siikupata muongozo wa kutosha.