Ushuhuda: Hasara inauma asikwambie mtu

Ushuhuda: Hasara inauma asikwambie mtu

Kilio cha watu wengi kukosa ajira kilipokuwa kikubwa tuliambiwa tukajiajiri,mzee nikasema isiwe shida ngoja nijiajiri yawezekana huko ndiko utajiri ulipojificha.
Nikawaza nifanye nini,nikakumbuka Jembe halimtupi mtu tena washairi walisema kama mnataka mali mtaipata shambani. Nikajipanga nikaitafute mali shambani.
Sikuwa na mtaji hapo mwanzo,nikajibana nikapata sh kama milioni kasoro elfu 25 yaan nilikuwa na sh 975000/=. Nikashawishiwa kuingia kwenye tikiti.
Mambo yalienda vizuri,mwezi wa kwanza mazao yako vizuri,wa pili katikati ulikuja ugonjwa gani jamani daaahhhh. Ule ugonjwa Kama ulitumwa vile kumaliza hata ule mtaji mdogo niliokuwa nao tena niliojibana kwa mda mrefu.
Sikuamini ndani ya wiki moja ugonjwa ulikula mazao yote,yaani mpaka majani. Dawa zote zilidunda. Asikwambie mtu,pale ndipo nilipojua hasara inauma mazeee. Niliumia kupita maelezo ukizingatia sikuwa na pesa nyingine.
Niliyumba sio siri,nimeishi maisha ya shida sana hapo kati. Sasa hivi nina madeni kama laki tatu hivi.
Nimegundua wanaosema tukajiajiri ni wale wasiokuwa na uelewa ni jinsi gani huku kuna changamoto. Kuna kufirisika huku tena ule mtaji kidgo nao hupotea.
Asikwambie mtu hasara inauma jamani,ni noma.
Sijafa moyo,nikijipanga nitatafuta mishe nyingine.
Mkuu mwaka 2016 nilifuga kuku kwa mataji wa zaidi ya 1.5 ml.kuku walikwenda poa baada ya miezi kadhaa uliingia ugojwa kuku wote walkufa..yani kuku hata nyama huoni ladha yake.niliumia sana sana..nilitiwa moyo kama hiv na principle yangu flank hv huwa inaniongoza kuwa kufeli ndio njia njia ya kuelekea kufaulu..nilisimama tena watu wa kalibu walisema kila mtu na lake mm sikufa moyo nilianza tena kwa hapa na pale now mkuu nina kuku zaidi ya 400..mungu ni mwema..usikate tamaa mkuu,,ukikata tamaa tu umekwisha.
 
Kuanguka ni kawaida ila ukishindwa kuinuka ndio tatizo usiogope,nafac unayo tena ya kunyanyuka!
 
Mkuu mwaka 2016 nilifuga kuku kwa mataji wa zaidi ya 1.5 ml.kuku walikwenda poa baada ya miezi kadhaa uliingia ugojwa kuku wote walkufa..yani kuku hata nyama huoni ladha yake.niliumia sana sana..nilitiwa moyo kama hiv na principle yangu flank hv huwa inaniongoza kuwa kufeli ndio njia njia ya kuelekea kufaulu..nilisimama tena watu wa kalibu walisema kila mtu na lake mm sikufa moyo nilianza tena kwa hapa na pale now mkuu nina kuku zaidi ya 400..mungu ni mwema..usikate tamaa mkuu,,ukikata tamaa tu umekwisha.
Hongera sana boss.
 
Duh pole sana...."Stake what you can afford to loss"
 
Back
Top Bottom