Ushuhuda: Kuajiriwa ni bora kuliko kujiajiri

Weka namba nigga ili tujue tunakupata vipi in case tu_ nahitaji kitu kariakoo
 
Mleta mada nataka nikusahihishe kidogo..

Labda ulitakiwa kusema kuajiriwa ni rahisi kuliko kujiajiri, hapo ndio ungeeleweka.
Lakini ukisema ni bora, unaleta kizungumkuti kwa sababu haieleweki unasema bora kivipi?

Kwamba ukiajiriwa unaishi maisha mazuri kuliko waliojiajiri?! Au ukiajiriwa unaingiza kipato kikubwa kuliko kujiajiri?! Au unamaanisha nini? Haieleweki!
 
Hakuna mwanasiasa anaetaka ufanikiwe wewe graduate......tupambane wakuu mpaka tone la mwisho....tukifa tufe tukiwa kwenye mapambano...
 
Haieleweki nini..wacha kukuza mambo kama akina mama wa kiswahili wauza vitumbua....
 
Mkuu kwanini hukuanza biashara wakati bado upo kwenye ajira ukizingatia umesema hukua na kazi kubwa kiivo huenda ulikua na kamuda ka kufanya research mkuu.
Biashara si lelemama aisee.
 
Kuajiriwa sio kikwazo cha wewe kufanya biashara

Unapowaza kufanya biashara usiwaze kuacha ajira

Ajira yako endelea na pia anzisha biashara yoyote isiwe mvivu tena ukizingatia ndio kwanza unaanza kutafuta maisha
 
Hatuwezi kufanana mkuu, wapo watakaoshindwa na wapo watakaofanikiwa.
Pia wapo walioshindwa na wapo waliofanikiwa. Ila cha muhimu ni kwamba business sio lelemama na ni kitu kinachohitaji Strong strategy, commitment, nguvu, muda na akili ya kutosha.

Hiyo kazi usingeiacha bali ungekuwa unafanya business na kazi pia means hata business ikifail basi una sehemu ya kushikia.
Then unatulia kidogo alafu unasimama tena mpaka kieleweke. Hii ndio maana ya Strategy. naweza sema ulikurupuka na hukujipanga kwa consequences za maamuzi yako, lakini cha muhimu ni kwamba umejiunza.

Alafu kama ulikuwa unapenda business kwanini usingesoma courses ambazo zinaegemea business moja kwa moja kama Economics na MBA?

Maamuzi ni yako na chochote kinaweza kutokea.
Wanasema if you're tired of starting over then stop giving up.
 
Optimists

Persistence is not always the answer, sometimes you need to change direction. Kama unaona mambo hayaendi rudi kwenye kuajiriwa.

Ujasiriamali unawaponza sana watu, mtu anaona bora awe fukara kuliko kuwa muajiriwa.

Hukupaswa kuacha kazi haraka hivyo. 2 sources of income is better than one.

800k is nothing kwenye biashara yeyote labda uwe mchuuzi tu kama ulivyosema. Lazima ujipange unapotaka kuanza on your own kimtaji na uwe na line of credit pale utapohitaji kuinject more capital into your business. Line of credit inaweza kuwa bank loans, your friends and family (Your network. Your networth).

Mwisho ukitaka kuwa maskini nchi hii ingia kwenye kilimo na mtaji wa mbuzi.
 
Mkuu kwanini hukuanza biashara wakati bado upo kwenye ajira ukizingatia umesema hukua na kazi kubwa kiivo huenda ulikua na kamuda ka kufanya research mkuu.
Biashara si lelemama aisee.
Kwa mazingira niliokuepo ilikua kijijini sana fursa pekee ilikua ni kilimo na mtaji huo sikua nao kwa kipindi hicho
 
Kwa mazingira niliokuepo ilikua kijijini sana fursa pekee ilikua ni kilimo na mtaji huo sikua nao kwa kipindi hicho
Kwa kijiini ni sawa lakini mkuu next time ukipata nafasi research ni muhimu.
Acha uonekane ni muoga lakini kuweka pesa mingi sehemu ambayo huna uhakika nayo na ni pesa unayoitegemea ni too risk aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…