USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Nimekusoma, ila kichwa cha habari kinakatisha tamaa kwa wasomaji, yaloandikwa ndani ni mazuri sana na yanafaa kufanyiwa kazi. Umeandika changamoto za ufugaji wa kuku wa kienyeji; zikifanyiwa kazi, ufugaji huo unaleta tija kubwa sana.
Kwanza niwaeleze kitu;
Kuku matahila (wa kizungu) ni majanga kwa jamii yetu, ndo maana utakutana na mtoto miaka 10 mnene hadi unamhurumia; chemicals zinazotumika kwenye ufugaji wa haya makuku ndo hizo zinawaadhili watoto wetu kunenepeana. Nyumbani kwangu ni marufuku kuyaona hayo mayai / manyama ya hao kuku.
 
Duh sitakata tamaa bado maaana mwenzetu pamoja na changamoto alizozitaja hakuwahi kulala njaa.... that means ana instant income, no matter yametoka mayai mangapi au kuku wangapi. Pia suala la marketing ni muhimu sana, huwezi kusema nina kuku na mayai kisha ukakaa ukatulia ukasubiria wateja waje,wenyewe, marketing ni muhimu sana sana. Kwenda kuuza kwenye supermakerket peke yake haiku-guarantee kuwa ndio umepata soko zuri.

Hata hivyo umesema vyema kuwa Vijana waache kuwa na ndoto kuwa mambo yatakua rahisi rahisi tu, sivyo hivyo. Dedication ni muhimu sana
 
Hoja nzuri ya kushawishi wateja kwenye biashara yako kijanja.Kuku wa kienyeji wanalipa na salama zaidi kwa mfugaji anayeanza kuliko kuku wa kisasa.Ni kweli changamoto zipo nyingi ila hakuna biashara isiyo na changamoto.
MASOKO
Kuhusiana na soko kuku wa asili hawawezi kushindanishwa na kuku wa aina nyingine yeyote Tanzania.Ukitaka soko la uhakika kuku wa kienyeji ni 100% labda kama unaongelea soko la Dar kwa watu wa kipato cha chini kabisa na wasio jali afya zao.
UZALISHAJI
Changamoto ni sahihi kwa atakayeamua kuwafuga kuku hao kienyeji.Wapo waliofanikisha ufugaji huu kwa kuzingatia kanuni za kisasa kwa vifaranga.Kuku hanyonyeshi,kama unavyowatunza kuku wa kisasa watunze wa kienyeji kwa kanuni zilezile isipokuwa baada ya kuwa na uwezo wa kujitegemea unawaachia huru ili wathibitishe uasili wake.
Ukiwatunza na kuwalisha kama kuku wa kisasa ladha ya kuku wa asili inapotea na hutawauza kwa bei wanayostahili wala kuwatofautisha na hao tunaowaita wa kisasa.
ATHARI KWA MLAJI
Kizazi kinachokula bila kujali au kuzingatia ubora na usalama wa wanachokula hakitabaki salama na hakitadumu.Kwa walio makini na afya zao wimbi kubwa la walaji linaanza kuondoka taaratibu kutoka kwenye ulaji wa chakula kisichojali afya zao.Kuku wa asili sawasawa na vyakula vyetu vya asili ni salama na vina nafasi kubwa ya kutawala soko.Tatizo hautaki kuvitangaza au kuvitetea.
MTAJI WA KUANZIA
Wakati wa kutetea hoja iliyopo mezani njoo mezani na hesabu inayohitajika kuanza ufugaji wa kisasa hadi kufika gharama za uzalishaji zinapokuwa sawasawa na mauzo(BEP).

Changamoto kubwa kwenye ufugaji wa kuku wa asili kwa walio mijini ni eneo la kufugia na vyakula.Kwa walio na maeneo makubwa nje ya miji kuku wa kisasa kwa hesabu zake hawawezi kushindana na kuku wa asili.

Katika jukwaa hili la JF wakenya walipoleta mayai mkengi Tanzania malalamiko mengi yalitoka kwa wafugaji wa kuku wa kisasa.

Ninaafikiana na mtoa mada kwa 100% kuhusu ufugaji wa kuku chotara kwa aliyepata uzoefu na siyo anayeanza ufugaji na hana chanzo kipya cha kuinua mtaji anapodondoka.Hakuna mstari mnyofu katika biashara yeyote.

Tujadili fedha nyingi na usalama wa mlaji.
 
N
hebu na ww tupe ukweli mkuu!!!!!!!!

Nyongeza ndogo kwenye eneo la uzalishaji.Kuku huatamia mayai kwa siku 21.Fuatilia tarehe ya kwanza ya kuku wako wanapoanza kuatamia,jifunze mbinu za kuwafanya kuku wako waanze kuatamia na kutotoa kwa wakati mmoja.Mfano una kuku 10,unawalazimisha kuku 5 waanze kuatamia kwa pamoja (rejea masomo ya nyuma juu ya ufugaji wa kuku wa asili/kienyeji).

Siku ya 21 alfajiri wanyang'anye kuku waliokuwa wanaatamia vifaranga vyao kabla havijatoa milio,wape mayai mengine.Hawatatoka hapo hadi siku nyingine 21 zifike na watotoe vifaranga vingine.Wanyanyang'anye vifaranga na kuwaachilia wapumzike.Ukiwatunza kwa chakula cha uhakika na kinga za magonjwa majuma mawili/matatu wataanza kutaga tena.Idadi ya vifaranga na mayai atakayokupatia kila kuku haitakuwa ya mazoea.

Kanuni rahisi ni (1) Jua kitu cha kufanya (2) Jua namna ya kufanya (3) Kifanye.
Mambo haya hatupaswi kuyaweka hadharani kiasi hiki.Tanzania wengi wetu hatua ya kwanza na ya pili tupo vizuri sana ,tatizo lipo kwenye hatua ya tatu.Kenya kwenye hatua ya kwanza na pili wapo dhaifu kuliko sisi ila hatua ya tatu wametuacha mbali ndiyo maana baadhi yetu hatutaki kuweka kila kitu hadharani.

Tunalenga kufundishana wenyewe wanafaidi wapita njia kwa tuliyofundishana kisha wanaanza kutucheka nasi tunashangilia.
 
Asante sana kwa thread hii. Nitakupigia for sure. Ninahamia kwenye nyumba ambayo ina eneo la wazi kama la robo 3 eka na maji ya kutosha. Tutawasiliana ili unielekeze namna ya kufuga kuku mahali hapo.
 
 



IPO NJEMA KIMTAZAMO LAKINI NI LAZIMA KUWEPO MTAZAMO ZAIDI KUKUZA HUU UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KWANI NI CHAKULA MHIMU NA ASILI MWILINI MWETU
 
kuna muda huwasijuti kupotezea muda wangu kwenye JF. Be blessed mengi na makubwa nimejifunza hapa. Shida sisi mazoea ya ufanyaji wa mambo sasa umekua utamaduni wetu. ntakutafuta for more clarification. i wishi kufuga kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa. big up Ginner
 
Wadau nina heka 10 eneo la MKATA njia panda ya handeni naomba ushauri wenu nifanyie nn kwa maeneo haya ili niweze kusonga mbele Kama ni kulima nilime nini Kama ni kufuga nifuge nini msaada tafadhali wadau Asante
 
Wakuu ahsanteni kwa ushauri wote waliochangia uzi huu shida yangu nina vifaranga vya siku tano tu mpaka sasa naona vingine vina kosa nguvu na dakika hii washakufa wawili msaada wenu tafadhali
 
Tunauza kuku wa kienyeji, kwa wakazi wa DSM onja msisimko wa kuku watamu wa kienyeji. Kuku ni wakubwa na wanauzito wa kilo 3-4. Bei nzuri kabisa. Unaweza ukaletewa mpaka ulipo kama utahitaji wengi. DM kama unahitaji
 
Maoni ya mleta mada ni conclusive pasipo kuwa na utafiti, inaonesha yeye ni mhanga wa kufanyabiashara bila kuomba ushauri wa wataalam wa sekta husika:

Angalia vidokezo kadhaa ambavyo amecoclude nje ukweli wa kutaalam:

1. Utagaji, uatamiaji na kuharibika kwa mayai:
Ili kupata mayaimengi yabidi kuku alishwe chakula cha kutosha, hapo kuku anaweza kutaga hata mayai 20 kwa round moja. Kama imterest ni kuuza mayai basi lazima utoe supplementation, kama interest ni vifaranga na mayai Mengi, kuku hunyanganywa vifaranga immediately baada ya kutotoa na ukifanya hivyo research zinaonesha kuwa after WK mbili anaweza kuanza kutaga round nyingine. Siyokweli kuwa mayai ya kienyeji huharibika haraka, kama wewe ni commercial dealer wa mayai unatakiwa kuyaokota immediately after being laid na kuyahifadhi kwenye ubaridi.
1. Uzito wa kuku:
Kama wewe ni commercial dealer wa Nyama unatakiwa kufanya line/breed selection kwani baadhi ya lines huwa na kuku wakubwa kwa muda mfupi, bila kusahau supplementation.
 

Umeeleweka GAMA, tunashukuru kwa ufafanuzi, ila concern ya mtoa mada sio juu ya mbinu za ufugaji wa kuku wa kienyeji bali uko kwenye mbinu bora zaufugaji wa kibiashara. Tunapolenga ufugaji wa kibiashara ni muhimu kuachana na traditional technique za ufugaji bali kuadapt mbinu za kisasa Zaidi. kwenye swala la inbreeding au breeding selection iyo husaidia kupata ,begu nzuri Zaidi ya kuku, ila ikumbukwe breeding selections is not for every one, sio kila mtu anaweza kutengeneza mbegu bora ya kuku kwa kucross waliopo, na wakati mwengine breeding selection hutumia miaka kadhaa kupata mbegu bora. sasa why all that effort wakati kuna breeds nzuri tu zilizofanyiwa tafiti ziko sokoni tayari. kwanini mtu asifuge hao. Kwenye biashara muda nao ni Gharama.
 
Ninaposema breed selection maana yake ni wewe kwenda kitaa kuchagua kuku wa kienyeji wakubwa,mf, kuchi, hii inachukua miaka mingapi?, hawa ukiwasupplement they are always big and heavier comparatively. My take: mleta mada ni copy cat na hajafanya consultation yoyote kwa wataalam, huu ni ugonjwa sugu kwa wajasiliamali wengi.

Addendum: hata kupeleka yai bovu sokoni kwa zama hizi ni aibu kwani kuna candling touch inayokuwezesha kujua kama yai ni bovu ama la, kauli ya mleta mada kuwa yai LA kienyeji (lililorutubishwa) huharibika haraka viz aviz lisilorutubishwa ni ulongo mtupu, the fact is yai lolote ukilitunza kwenye shelf temperature kama ya pwani huharibika haraka.
Kuhusu size ya kuku: kumbuka kuwa hata hawa kuku wa kisasa wanabodysize tofauti so is egg size na egg laying, kwa broiler for instance Ross ni wadogo kuliko arboacres, big dealers huchagua lines wa kufuga na siyo kujifugia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…