Nashukuru kwa kukubali kupokea challenge,
kwa ufupi andiko lako limejaa upotoshaji mkubwa na linalenga kuwakatisha tamaa, wajasiriamali wadogo wadogo ambao wanapendelea kufuga kuku wa kienyeji.
Pia nimegundua mambo makubwa mawili,
1. Bila shaka utakuwa unauza hiyo aina ya kuku amabayo unadai kuwa ni wazuri.
2. Bado hujajua mbinu mbali mbali za ufugaji wenye tija.
Hebu tazama hapa, ulichoandika.
Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.
kuku wa kienyeji wanataga mayai 15 hadi 20 na sio kwa siku za mfululizo kuna siku nyingine huwa hatagi na hii inatokana na kutokushiba vizuri, nakubali kuhusu muda wa kulea kuwa ni siku 50 hadi 60. unachotakiwa kufanya siku tatu baada ya kuku kutotoa vifaranga, mnyang'anye vifaranga na uviweke mbali nae huko vipatie chakula cha kukuzia stater, maji ya kunywa changanya na glucose, pia weka na chanzo cha joto kama ile mtungi wenye mkaa wa moto ndani yake.
ukifanya hivyo itamchukua kuku huyo uliemnyang'anya vifaranga wiki mbili na kuanza tena utagaji.
kwa mwaka atatoa kati ya mayai 100 hadi 160 kwa uhakika.
Tizama na hapa.
'Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.
uhifadhi wa mayai ya kienyeji sio mgumu, yanakaa bila ya kuharibika kwa muda wa mwezi mmoja, unachotakiwa kufanya, hifadhi mayai yako ktk trey ya mayai, pia chunguza kama yai lina ufa hilo usilihifadhi litumie kwa kula mwenyewe na familia, pia weka mayai yako sehemu ya wazi ambayo ina mwangaza wa kutosha, kuyaweka mayai sehemu isiyo na mwangaza kutapelekea mayai kuanza kutunga kifaranga ndani yake (hiyo ni kwa mayai ya kuuza kwa matumizi ya lishe)
kama unahifadhi yai la kutotolesha hilo halitakiwi lizidi siku 14 uwe tayari ushampa kuku kwa ajili ya kuatamia.
kwa faida yako na wengine si lazima kuku wa kienyeji apandwe na jogoo ndio atage, umri wake wa kutaga ukifika tu ataanza kutaga, ambao ni miezi sita hadi saba.
Pia bei ya kuku wa kienyeji zaidi kutokana na ladha yake na wala sio kilo zake.
Mwisho.
Ningefarijika sana kama unge declare interest kuwa wewe ni mfanya biashara wa hao kuku uliowapigia debe, hata ukaweka na picha zao na namba yako, kuliko kuwakatisha tamaa wafugaji waliojikita ktk ufugaji mdogo mdogo wa kuku wa kienyeji.
Pia nawatia moyo wafugaji wote wasikatishwe tamaa na maandiko kama hayo bali yawe chachu ya wao kujua zaidi mbinu mbali mbali za kupata kuku wengi ndani ya muda mfupi na wasichoke kujifunza.
kama utanataka kujua chochote kuhusu kuku wa kienyeji njoo in box nitakusaidia bila ya malipo yoyote, mimi sio mfanya biashara, nami nakaribisha kukosolewa.