USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Kumekuwa na upotoshaji kwa baadhi wa watu wanaojiita wataalamu wa ujasiriamali, hasa wanaofanya shughuli za ufugaji kwa maandiko ya whatsapp bila kuwa na hata kuku mmoja bandani. Nimesukumwa kuandika bandiko hili hapa kutokana na jumbe mbali mbali za uufugaji wa kimtandao unaoshawishi vijana kuwa watatajirika mapema kwa shughuli za ufugaji kwa kuanza na kuku wa kienyeji kumi na moja na kuweza kupata Zaidi ya kuku miatatu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji. Hoja yao inaweza kuwa sahihi, ila ningependa kusisitiza mafanikio katika ufugaji hayapo katika idadi ya kuku unayomiki, bali ni namna ulivyoweza kumanage biashara ya ufugaji.


Hoja yangu leo hapa ni kwamba, Biashara ya kuku wa kienyeji hailipi na nikupoteza muda wako. Na nitatetea hoja yangu kwa mifano hai na uzoefu wangu katika ufugaji.

Biashara ya Mayai. (idadi isiyo na tija kibiashara)
Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.

Changamoto kwenye soko la mayai ya kienyeji. (Uhifadhi wa mayai).

Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.

Kwa uzoefu wangu binafsi, nilianza kusambaza mayai ya kienyeji kwenye supermarkets miaka mitatu iliyopita. Nilipata changamoto kubwa sana ya kubadilisha mayai mara kwa mara kwani mteja akichukua yai viza ni kumpoteza kabisa. Hii ni changamoto ya kwanza ambayo mpaka sasa bado inasumbua wafugaji wengi.


Bei juu kwa mayai ya kienyeji

Gharama za mayai husika, bei ya mayai ya kienyeji iko juu ukilinganisha na gharama za mayai ya kuku wa kisasa. Soko kubwa la mayai ni pamoja na vibanda vya chips, migahawa na hoteli. hawa wanauhitaji mkubwa sana wa mayai na soko liko juu muda wote wa mwaka. Soko la mayai ya kienyeji lipo Zaidi kwenye households. (soko la familia) hasa kwa vigezo vya kuzingatia afya zaidi. Soko hili la familia sio kubwa, ni soko dogo na mara nyingi hutumia tray moja kwa kipindi cha wiki mbili au Zaidi. kwa mzalishaji mkubwa wa mayai ya kienyeji ni lazma awe na soko la familia pana Zaidi kuweza kupata faida ndogo, nasema faida ndogo maana ili kuzalisha mayai tray kumi (mayai 300) kwa siku, utahitaji Zaidi ya matetea 700 mpaka 1000 ya kienyeji pure. idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya mayai yanayopatikana.

Biashara ya Nyama.
Na declare interest, mimi pia ni msambazaji wa nyama ya kuku wa kienyeji, hivyo naongea kwa uzoefu, na niko tayari kukosolewa. Pamoja na kufugwa katika misingi ya kijani (organic rearing), iyo pekee haitoshi kumpa thamani inayostahili huyu kuku sokoni. Thamani ya kuku sokoni ni uzito alio nao, organic component ni jambo la ziada lililo muhimu pia. tunavyo jadili bei ya soko ya kuku huyu ni lazma tumliganishe na gharama za bidhaa pinzani zilizoko sokoni. Haitawezekana kumuuza kuku mwenye kilo moja au pungufu kwa bei ambayo tunashawishiana humu ya 15000-20000 wakati bidhaa pinzani (nyama nyeupe) kama samaki sato toka mwanza wanauzwakwa 7500 kwa kilo, au kitimoto, nyama ya ngombe ambazo nazo kilo ni 7500-8000. Hivyo basi. hoja yangu hapa ni uzito wa kuku husika. Ukiachana na jamii chache za kuku wa kienyeji (kuchi etc) wenye uzito mzuri, majority ya kuku pure wa asili/kienyeji kwa majogoo huwa na pungufu ya kilo moja na nusu. Kumbuka uzito wa kuku hawa sio kwasababu ya malisho duni, laah hasha, bali ni kutokana na vinasaba (genes) vyao kuwafanya kuwa na maumbo madogo madogo. kwa kuku wa aina hii, sitegemei mfugaji kama atafanikiwa kuwapeleka sokoni na kuweza kupata bei nzuri toka kwa mlaji wa mwisho.

Nini kifanyike.
Ili ufugaji uwe wenye tija kibiashara ufanyike, ni lazma wafugaji tuamke na kuachana na ufugaji wa kuku hawa asilia kwani hawana tija. Nikisema hivi simaanishi watu waache kufuga, hapana, ila wafuge aina /breeds za kuku zenye tija kibiashara. Kuku pekee unaoweza kuwafuga kwa mbinu za kienyeji na bado wakakuletea mfugaji faida nzuri kibiashara, ni kuku aina ya chotara (cross breeds). hii ni aina ya kuku wenye sifa zote za ukienyeji kwa misingi ya mbinu zao za kuwafuga pamoja na namna walivyo nauwezo wa kuhimili mazingira hasa ya vijijini. Kuna aina mbalimbali ya kuku hawa ikiwamo Black/ white australorps, kroiller, Rhodes island red, red hamshire, Sussex etc. Hawa ni kuku ambao wanaserve purpose zote za mayai na za nyama. Mfano kuku aina ya black/white australorps wao wanauwezo wa kutaga mpaka mayai 250 kwa mwaka, tofauti na wa kienyeji, mayai ya kuku hawa huwa makubwa na yenye kasha jeupe na kiini cha njano kama utawafuga kwenye mazingira na mbinu asilia (za kienyeji). Ukilinganisha uwezo wa utagaji wa kuku hawa utagundua utagaji wao ni Zaidi ya asilimia 500% ukilinganisha na ule wa kienyeji pure. Idadi hii ya mayai toka kwa kuku mmoja kwa mwaka, anaweza kumwezesha mfugaji kuzalisha mayai kwa wingi na kushusha Zaidi bei ya mazao yake (mayai) kuwa chini kuweza kuliteka soko kwa urahisi Zaidi. Kumbuka, bei ya juu ya mayai ya kienyeji ni kwaajili ya kulipia gharama kubwa za utunzaji wa kuku huyu ilihali utagaji wake ni hafifu.

Pili, kuku hawa wana nyama nyingi Zaidi kuliko hawa wa kienyeji kwa majogoo hufikia mpaka uzito wa kilo 3-3.5. huku matetea hufikia kilo 2-2.5 na huwa na nyama nzuri, iliyokomaa vyema na yenye ladha. kwa uzito huu kwa majogoo, kuku hawa uuzwa kwa bei ya 20,000 - 25,000 wakiwa hai. bei ambayoni kwa mujibu wa bei ya soko kwa makadirio ya shilingi 8,000 kwa kilo kwa nyama nyeupe.

Mapungufu.
Pamoja na ubora wa kuku hawa katika ufugaji wa kibiashara, kuku hawa pia wanachangamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na uwezo wa kutamia. Pamoja na hii kuwa changamoto pia ni fursa kwani kwa yeye kutotamia kunamwongezea nafasi ya yeye kuendelea kutaga mara nyingi Zaidi bila kupumzika. hivyo changamoto hii ni faida kwa mfugaji anaelenga kufuga kwa tija. kwa vile mayai haya huwa yamerutubishwa na majogoo, nirahisi kwa mfugaji kuongeza idadi ya kuku kwa kupitia kutotolesha kwa mshine za kuangulia vifaranga au kumpa kuku mwingine ayatamie kwa niaba.



Neno la kufungia.

“ I think I touched a raw nerve when I said farming is NOT cool! I believe farming takes a lot of HARD work and dedication. Lets not lie to the youth that they'll become instant millionaires when they get into farming. It becomes "cool" once you master the trade......” caleb

Ufugaji unalipa ukiweza kuibudu biashara ya ufugaji,


Kwa ushauri Zaidi kuhusu shughuli za ufugaji, tuwasiliane kwa namba 0755815174. pia pata fursa kusoma ya Makala mbali na utaalamu kutoka kwenye mtandao wetu www.backyard.co.tz

Nimejaribu kuattach picha za baadhi ya kuku bora wanaofaakufugwa kienyeji na wakaleta tija kibiashara hapa chini. Neno langu si sharia, nakaribisha Michango

View attachment 385750 View attachment 385751 View attachment 385752 View attachment 385753 View attachment 385754

Umeongea point na umekuwa wazi na wengi wanafanya ufugaji kwa maandishi wakati ukija practical ni changamoto kubwa.
All in all wel said

I agree with you [emoji817] %
 
Umeongea point na umekuwa wazi na wengi wanafanya ufugaji kwa maandishi wakati ukija practical ni changamoto kubwa.
All in all wel said

I agree with you [emoji817] %
Mkuu ni kweli ufugaji wa kuku wa kienyeji una changamoto but lakini ukiwa na nia ya dhati INSHAALLAH unafNikiwa. Yatupasa kutambua kila kitu kina changamoto zake ila ukiwa mfuatliaji unaweza kuzitatua hizo changamoto.
 
Yote ulioeleza in sawa kabisa .ila tuje kwenye faida na hasara ya kuku Wa kienyeji na Wa kisasa nyama na mayai katika afya ya binadamu ,ukichambua na hili utaona afya ya binadamu ni zaidi ya fedha ,aijalishi ni aghali kiasi gani.ushauri usiturudishe nyuma kule dunia nzima sasa unapakimbia ,sasa duniani pote mpango mzima ni ( organic food and cosmetics) chakula ,mifugo vya kienyeji na virembesho vya mwili.kuanzia mbolea,dawa,malisho ya mifugo na mifugo yenyewe,ushauri endelea kufuga Wa kienyewe wacha tamaa ya faida kubwa kwa gharama ya maisha ya binadamu mwenzako.pole pole ndio mwendo
Hapa umeongea vizuri sana, hivi vyakula vya kisasa vina athari kubwa sana kwenye jamii yetu
 
sina uhakika n by da way natumai wanao ikiwa hawana ulizia wafugaji ulionao jirani huko ipi kampuni nzuri ya vifaranga...mi nilinunua toka kiwanda cha mkuza ....wale niliowakuta wakati ule walikuwa ni vjogoo 2pu
Shukrani mkuu dezamba ngoja naendelea kukufatilia
 
sina uhakika sana ila nahisi umeuziwa vijogoo vya layers (vijogoo vya kuku wa kisasa wa mayai) na si chotara. Rangi yao huwa weupe na baadhi wanamabaka mekundu au vyenye rangi ya kanga kanga...
Mkuu huo ndo wakati mwafaka wa kutuambia wanakuaje ili na sisi tukienda tuwe tunajua wapo vipi hata picha ukiweza tuma mkuu heshima kwako
 
sina uhakika sana ila nahisi umeuziwa vijogoo vya layers (vijogoo vya kuku wa kisasa wa mayai) na si chotara. Rangi yao huwa weupe na baadhi wanamabaka mekundu au vyenye rangi ya kanga kanga...
hvyo ndivyo ilivyo tokea ila nazani c kama usemavyo wa layers coz layers c warefu kama hawa niliopewa hata vijogoo vya broiler huwa ni wafupi pia,,,hawa wana karibu 80% ya kuku wa kienyeji ktk ustahimilivu wa magonjwa,hewa,chakula pia hata shape yao pia kama c rangi wanapokuwa wamekuwa wakubwa sana,,,even meat taste also almost similar.........
 
inabidi niende hapo kwani bei yenyewe inavutia
ILA KTK KUNUNUA HAWA VIFARANGA NI VYEMA KUCHAGUA KWA UHAKIKA KABISA KUWA NI MACHOTARA SABABU AINA YAHAO NILIOPEWA MM JAPO HAWASUMBUI KTK MAGONJWA WALA CHAKULA NI VYEMA KUJUA JINSI YA KUPATA VIFARANGA HALISI VYA KUKU CHOTARA ALIYETOKA NA JOGOO WA MBEGU ZAKI8SWAZ,,,MAANA HAWA SOKONI NILISIKIA WANASUMBUA KWA KUWA RANGI YAO INA WATAMBULISHA KUWA NI BLOIRELS
 
hvyo ndivyo ilivyo tokea ila nazani c kama usemavyo wa layers coz layers c warefu kama hawa niliopewa hata vijogoo vya broiler huwa ni wafupi pia,,,hawa wana karibu 80% ya kuku wa kienyeji ktk ustahimilivu wa magonjwa,hewa,chakula pia hata shape yao pia kama c rangi wanapokuwa wamekuwa wakubwa sana,,,even meat taste also almost similar.........

mkuu niamini mimi, umeuziwa vijogoo vya layers na si chotara, vijogoo vya layers huuzwa kwa sh 450-600 kwa madalali pale Tazara. kuhusu taste, kinachompa kuku taste asilia si aina ya kuku husika bali ni chakula unachompa, kadri unavyompa kuku majani, anavyokula nyasi, wadudu na madini madin katika udongo ndipo anapopata harufu na taste ya kienyeji.
 
mkuu niamini mimi, umeuziwa vijogoo vya layers na si chotara, vijogoo vya layers huuzwa kwa sh 450-600 kwa madalali pale Tazara. kuhusu taste, kinachompa kuku taste asilia si aina ya kuku husika bali ni chakula unachompa, kadri unavyompa kuku majani, anavyokula nyasi, wadudu na madini madin katika udongo ndipo anapopata harufu na taste ya kienyeji.
shukrani kwa elimu hiyo sikufaham kabla so huenda niliwaona na radha nzuri sababu ya chakula walichokuwa wakila
 
mkuu niamini mimi, umeuziwa vijogoo vya layers na si chotara, vijogoo vya layers huuzwa kwa sh 450-600 kwa madalali pale Tazara. kuhusu taste, kinachompa kuku taste asilia si aina ya kuku husika bali ni chakula unachompa, kadri unavyompa kuku majani, anavyokula nyasi, wadudu na madini madin katika udongo ndipo anapopata harufu na taste ya kienyeji.
Mkuu chotara tunapata wapi na gharama yake msaada tu
 
safi umenena vyema ila mie ninao matetea wakienyeji niliowanunua mkoani nianzishe mradi mkubwa na mwanzoni walitaga mayai 15 kwa msimu ila nilipofahamu njia yakuchanganya msosi wao walitaga non stop hadi nibadilishe ndo waweze kuatamia ila lazima uhakikishe hawaumwi na kuhusu majoo nilipataga mbegu ya jogoo chotara na niliwafuga kwa miez 9 wafikisha uzito wa kg 2.5 japo sikumaintain chakula....i think with a formular n well care its not wasteful
Ilíkua unawapa chakula gan mkuu
 
Mbarikiwe wataalam wote Kwa Elimu nzuri mnayo tupa.Msivunjike mioyo Kwa wachache wanao boa.
Halafu kuna watu humu JF wanasema WaTanzania hatupendani.
 
Ilíkua unawapa chakula gan mkuu

12
Utengenezaji wa vyakula vya Kuku
Namba moja hadi nne katika jedwali hili ni michanganyiko wa vyakula aina 4 tofauti
kwa ajili ya kuku wenye umri uliotajwa hapa juu. Ukihitaji kuandaa chakula cha kuku
hao, chagua mchanganyiko mmoja (kwa safu wima) wenye malighafi zinazopatikana
kwenye eneo lako kwa urahisi na utakazozimudu kifedha.
UTAYARISHAJI CHAKULA CHA KUKU WANAOTAGA (MIEZI 5 HADI MIEZI
18) PAMOJA NA KUKU WAZAZI
Aina ya vyakula
Kiasi (kilo)
Chenga za Mahindi
31.5kg
Mtama
15.0kg
Pumba ya mahindi
13.0kg
Mashudu ya Alizeti
20.0kg
Dagaa
12.0kg
Chokaa
3.0kg
Premix
0.25gm
Chumvi
5.0gm
Jumla
100kg
-------------------------------------------------------------------------------

Aina ya vyakula
Kiasi (kilo)
Dagaa kilo
12.0kg
Chenga za mahindi
30.0kg
Mtama
6.75kg
Mashudu
20.0kg
Pumba ya mahindi
23.0kg
Chumvi
0.25gm
Chokaa
3.0kg
Mifupa
5.0kg
Jumla
100kg
AU
Vyakula hivi vyote vinafaa kwa kuku watagaji na kuku wazazi. Tofauti kwenye kuku
wazazi ni kuwa wanalishwa kiasi pungufu ili wasinenepe na kushindwa uzalishaji.
Mwongozo uliotolewa, hapa juu ni kwa ajili ya kuandaa kilo 100 za chakula cha kuku,
endapo unataka kutengeneza kilo 500 itabidi kila kilichopo kwenye mchanganyiko
kizidishwe, mara tano ndipo kupata hizo kilo 500....HAKIKA KINAFANYA KAZI JARIBU HIYO 4MLA END INGATIA HAWAUMWI UTAPATA MATOKEO
 
Msaada tafadhari,kama kutakuwa na mtu anayefahamu dawa ya kutibu ugonjwa uliowapata kuku wangu wakienyeji naomba msaada wa kimatibabu,kuku wanabadilika ghafla macho yao yanakosa nguvu na kuwa kama mtu aliyetingwa na usingizi,baada yapo miguu inakosa nguvu kuku ana simama kama ana taka kubenukia nyuma,wakati mwingine ana kita miguu yake chini kama kalewa,akianza kuonyesha dalili hizo ina maana tayari ana kuwa ameshaisha hachukui hata saa moja ana kuwa ameshakufa,vifaranga ndio hata robo saa haipiti,kuku wameanza kufa isivyo kawaida hata kideri hakifikii kwa siku wanakufa mpaka kuku 10,vifaranga ndio kabisa wanapukutika kama hawana akili nzuri.

Ugonjwa huu ulianza baada ya mafua makali,mafua makali yamepungua kwani mpaka sasa ni kuku mmoja tu ndiye bado hajapona mafua baada ya kuwapa matibabu kwa kutumia dawa ya otc 50%ndipo ugonjwa huu umeibuka na sijui tiba yake nini.
 
Back
Top Bottom