USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Kuku Chotara Wapo Tegeta Nyuki, Aina Ya Sasso, Croiler Na Malawi, Bei Ni 1500 Kwa Kifaranga Cha Siku 1, Tuwasiliane Kwa 0715488421 Nikupe Uzoefu, Mimi Nimechukua 200 Siku 3 Zilizopita
 
Kumekuwa na upotoshaji kwa baadhi wa watu wanaojiita wataalamu wa ujasiriamali, hasa wanaofanya shughuli za ufugaji kwa maandiko ya whatsapp bila kuwa na hata kuku mmoja bandani. Nimesukumwa kuandika bandiko hili hapa kutokana na jumbe mbali mbali za uufugaji wa kimtandao unaoshawishi vijana kuwa watatajirika mapema kwa shughuli za ufugaji kwa kuanza na kuku wa kienyeji kumi na moja na kuweza kupata Zaidi ya kuku miatatu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji. Hoja yao inaweza kuwa sahihi, ila ningependa kusisitiza mafanikio katika ufugaji hayapo katika idadi ya kuku unayomiki, bali ni namna ulivyoweza kumanage biashara ya ufugaji.

Hoja yangu leo hapa ni kwamba, Biashara ya kuku wa kienyeji hailipi na nikupoteza muda wako. Na nitatetea hoja yangu kwa mifano hai na uzoefu wangu katika ufugaji.

Biashara ya Mayai. (idadi isiyo na tija kibiashara)
Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.

Changamoto kwenye soko la mayai ya kienyeji. (Uhifadhi wa mayai).

Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.

Kwa uzoefu wangu binafsi, nilianza kusambaza mayai ya kienyeji kwenye supermarkets miaka mitatu iliyopita. Nilipata changamoto kubwa sana ya kubadilisha mayai mara kwa mara kwani mteja akichukua yai viza ni kumpoteza kabisa. Hii ni changamoto ya kwanza ambayo mpaka sasa bado inasumbua wafugaji wengi.

Bei juu kwa mayai ya kienyeji

Gharama za mayai husika, bei ya mayai ya kienyeji iko juu ukilinganisha na gharama za mayai ya kuku wa kisasa. Soko kubwa la mayai ni pamoja na vibanda vya chips, migahawa na hoteli. hawa wanauhitaji mkubwa sana wa mayai na soko liko juu muda wote wa mwaka. Soko la mayai ya kienyeji lipo Zaidi kwenye households. (soko la familia) hasa kwa vigezo vya kuzingatia afya zaidi. Soko hili la familia sio kubwa, ni soko dogo na mara nyingi hutumia tray moja kwa kipindi cha wiki mbili au Zaidi. kwa mzalishaji mkubwa wa mayai ya kienyeji ni lazma awe na soko la familia pana Zaidi kuweza kupata faida ndogo, nasema faida ndogo maana ili kuzalisha mayai tray kumi (mayai 300) kwa siku, utahitaji Zaidi ya matetea 700 mpaka 1000 ya kienyeji pure. idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya mayai yanayopatikana.

Biashara ya Nyama.
Na declare interest, mimi pia ni msambazaji wa nyama ya kuku wa kienyeji, hivyo naongea kwa uzoefu, na niko tayari kukosolewa. Pamoja na kufugwa katika misingi ya kijani (organic rearing), iyo pekee haitoshi kumpa thamani inayostahili huyu kuku sokoni. Thamani ya kuku sokoni ni uzito alio nao, organic component ni jambo la ziada lililo muhimu pia. tunavyo jadili bei ya soko ya kuku huyu ni lazma tumliganishe na gharama za bidhaa pinzani zilizoko sokoni. Haitawezekana kumuuza kuku mwenye kilo moja au pungufu kwa bei ambayo tunashawishiana humu ya 15000-20000 wakati bidhaa pinzani (nyama nyeupe) kama samaki sato toka mwanza wanauzwakwa 7500 kwa kilo, au kitimoto, nyama ya ngombe ambazo nazo kilo ni 7500-8000. Hivyo basi. hoja yangu hapa ni uzito wa kuku husika. Ukiachana na jamii chache za kuku wa kienyeji (kuchi etc) wenye uzito mzuri, majority ya kuku pure wa asili/kienyeji kwa majogoo huwa na pungufu ya kilo moja na nusu. Kumbuka uzito wa kuku hawa sio kwasababu ya malisho duni, laah hasha, bali ni kutokana na vinasaba (genes) vyao kuwafanya kuwa na maumbo madogo madogo. kwa kuku wa aina hii, sitegemei mfugaji kama atafanikiwa kuwapeleka sokoni na kuweza kupata bei nzuri toka kwa mlaji wa mwisho.

Nini kifanyike.
Ili ufugaji uwe wenye tija kibiashara ufanyike, ni lazma wafugaji tuamke na kuachana na ufugaji wa kuku hawa asilia kwani hawana tija. Nikisema hivi simaanishi watu waache kufuga, hapana, ila wafuge aina /breeds za kuku zenye tija kibiashara. Kuku pekee unaoweza kuwafuga kwa mbinu za kienyeji na bado wakakuletea mfugaji faida nzuri kibiashara, ni kuku aina ya chotara (cross breeds). hii ni aina ya kuku wenye sifa zote za ukienyeji kwa misingi ya mbinu zao za kuwafuga pamoja na namna walivyo nauwezo wa kuhimili mazingira hasa ya vijijini. Kuna aina mbalimbali ya kuku hawa ikiwamo Black/ white australorps, kroiller, Rhodes island red, red hamshire, Sussex etc. Hawa ni kuku ambao wanaserve purpose zote za mayai na za nyama. Mfano kuku aina ya black/white australorps wao wanauwezo wa kutaga mpaka mayai 250 kwa mwaka, tofauti na wa kienyeji, mayai ya kuku hawa huwa makubwa na yenye kasha jeupe na kiini cha njano kama utawafuga kwenye mazingira na mbinu asilia (za kienyeji). Ukilinganisha uwezo wa utagaji wa kuku hawa utagundua utagaji wao ni Zaidi ya asilimia 500% ukilinganisha na ule wa kienyeji pure. Idadi hii ya mayai toka kwa kuku mmoja kwa mwaka, anaweza kumwezesha mfugaji kuzalisha mayai kwa wingi na kushusha Zaidi bei ya mazao yake (mayai) kuwa chini kuweza kuliteka soko kwa urahisi Zaidi. Kumbuka, bei ya juu ya mayai ya kienyeji ni kwaajili ya kulipia gharama kubwa za utunzaji wa kuku huyu ilihali utagaji wake ni hafifu.

Pili, kuku hawa wana nyama nyingi Zaidi kuliko hawa wa kienyeji kwa majogoo hufikia mpaka uzito wa kilo 3-3.5. huku matetea hufikia kilo 2-2.5 na huwa na nyama nzuri, iliyokomaa vyema na yenye ladha. kwa uzito huu kwa majogoo, kuku hawa uuzwa kwa bei ya 20,000 - 25,000 wakiwa hai. bei ambayoni kwa mujibu wa bei ya soko kwa makadirio ya shilingi 8,000 kwa kilo kwa nyama nyeupe.

Mapungufu.
Pamoja na ubora wa kuku hawa katika ufugaji wa kibiashara, kuku hawa pia wanachangamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na uwezo wa kutamia. Pamoja na hii kuwa changamoto pia ni fursa kwani kwa yeye kutotamia kunamwongezea nafasi ya yeye kuendelea kutaga mara nyingi Zaidi bila kupumzika. hivyo changamoto hii ni faida kwa mfugaji anaelenga kufuga kwa tija. kwa vile mayai haya huwa yamerutubishwa na majogoo, nirahisi kwa mfugaji kuongeza idadi ya kuku kwa kupitia kutotolesha kwa mshine za kuangulia vifaranga au kumpa kuku mwingine ayatamie kwa niaba.

Neno la kufungia.

“ I think I touched a raw nerve when I said farming is NOT cool! I believe farming takes a lot of HARD work and dedication. Lets not lie to the youth that they'll become instant millionaires when they get into farming. It becomes "cool" once you master the trade......” caleb

Ufugaji unalipa ukiweza kuibudu biashara ya ufugaji,

Kwa ushauri Zaidi kuhusu shughuli za ufugaji, tuwasiliane kwa namba 0755815174. pia pata fursa kusoma ya Makala mbali na utaalamu kutoka kwenye mtandao wetu www.backyard.co.tz

Nimejaribu kuattach picha za baadhi ya kuku bora wanaofaakufugwa kienyeji na wakaleta tija kibiashara hapa chini. Neno langu si sharia, nakaribisha Michango

View attachment 385750 View attachment 385751 View attachment 385752 View attachment 385753 View attachment 385754
Elimu elimu elimu. Thanks kaka
 
Ah me vifaranga vyangu vinakufa kufa ovyo yaan unaweza kuta kwny vifaranga 15 ni wawili tu ndo wanakuwa wengine wote wanakufa vikiwa vidogo cjui kwann
 
Ah me vifaranga vyangu vinakufa kufa ovyo yaan unaweza kuta kwny vifaranga 15 ni wawili tu ndo wanakuwa wengine wote wanakufa vikiwa vidogo cjui kwann
Pole xana mkuu.mm vifaranga wangu hua wanakua ila tatizo ni mwewe na kipanga ndo wanasumbua na hasa nirudipo kazini au jmosi na jpil ninapokuwa naviacha.
Ww wavifugaje ???
 
Pole xana mkuu.mm vifaranga wangu hua wanakua ila tatizo ni mwewe na kipanga ndo wanasumbua na hasa nirudipo kazini au jmosi na jpil ninapokuwa naviacha.
Ww wavifugaje ???
Me nimewategenezea banda uwa siwatoi nje hadi wakishakukua kufika stage hata kunguru hawata weza kuwabeba ndo uwa naanza kuwachia nje so chakula maji kila kitu nawawekea ndan kwny banda lao
 
Ah me vifaranga vyangu vinakufa kufa ovyo yaan unaweza kuta kwny vifaranga 15 ni wawili tu ndo wanakuwa wengine wote wanakufa vikiwa vidogo cjui kwann
Usafi, chakula kizuri na eneo la kutosha ndio kila kitu kwa vifaranga.
Pole sana ila usikate tamaa
 
@ Ginner
Naweza nikakukosoa kwa asilimia 95 na naweza nikakupongeza kwa asilimia chache kwa ufugaji wa kuku wa kisasa

Kwa machache tu faida ya kuku wa kienyeji ukifuga kwa faida wana faida kubwa sana. But ukifuga kiholela hawana faida

Kuku wa kisasa kwangu sijawahi ona faida yake

Usiwavunje moyo wafugaji.
 
Mkuu kama umesoma mada, nimezungumzia ufugaji wa kuku (pure) wa kienyeji..hasa wale wanaopatikana mikoani hasa singida, dodoma, tabora etc... Sitabadili msimamo, ufugaji wa hawa hauna faida na ni wagumu sana kuwafuga kibiashara...

Pia kama umeifatilia mada vyema, nimependekeza aina ambazo ni bora ziaidi kufuga kibiashara, kuku hawa ni kwa kiasi kikubwa..hawa ni kuku chotara (cross breeds). Hawa unaweza kuwafuga kienyeji na bado wakapata uzito mkubwa na uwezo wa juu wa utagaji
 
@ Ginner
Naweza nikakukosoa kwa asilimia 95 na naweza nikakupongeza kwa asilimia chache kwa ufugaji wa kuku wa kisasa

Kwa machache tu faida ya kuku wa kienyeji ukifuga kwa faida wana faida kubwa sana. But ukifuga kiholela hawana faida

Kuku wa kisasa kwangu sijawahi ona faida yake

Usiwavunje moyo wafugaji.
Unakosoa kwa maneno mkuu toa hoja tupime
 
Ginner
Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji pure. Nimeanza miaka mi3 iliyo pita na nimepata faida sana hata kuku wa kizungu sitamani
1 wana soko hasa katika mahoteli makubwa
2 kuku wa kienyeji anafundishika tabia. Na ukitaka faida usisubiri kuku akulele vifaranga
3 kuku wa kienyeji ni wavumilivu na hawahitaji mlolongo saana wa chakula ( kila siku madini n.k)

Mimi naweza nikakukosoa saaaana na kukuomba uombe radhi kwa wana jamvi
Kiwango cha kuku nilicho nacho. Kila mwezi lazima nipate zaidi ya 90( trey 3 hizo). Soko langu liko kwenye mahoteli na mayai yanakaa wiki 2 hadi kuharibika na kuharibika kwakwe si kwamba ushindwe kula.
 
Umefuga kuku kwa miaka mitatu sasa, na kwa mwezi unapata mayai 90 (tray 3) na bado unasema biashara inakulipa!..nadharia ya ufugaji wa kibiashara bado iko chini chana miongoni mwa wafugaji. Kufuga kwa miaka mitatu, na production ya mayai iko chini ya tray 3 kwa mwezi basi uzalishaji wako ni wa matumizi ya nyumban tu na si wa kibiashara.

Hongera sana pia kwa kupata soko kwenye mahoteli, ila ungetufafanulia zaidi, matumizi ya kawaida ya mayai kwenyebmahotel ni pamoja na kutengeneza chips za mayai, cakes, chapati na kwa kiasi flani ni vitafunwa vya breakfast...costwise, ulimconvice vipi mteja wako, (hotel) kutumia mayai ya kienyeji yenye bei juu zaidi kwaajili ya matumizi yao na kuacha kutumia ya kisasa yenye bei nafuu zaidi.
Wana jamii mnaweza mkajipimia wenyewe.
 
Tanzania ya viwanda
Mi nadhani ktk hili hakuna kuwa watanzania tuliojijazia akili za kikejeli! Tufanye kazi kwa bidii kwa kila mmoja! Nakumbuka kauli ya baba wa taifa inayosema hivi; usiseme Tanzania itakufanyia nini sema nitaifanyia nini! Anzisha kiwanda chako cha kusindika nyama za kuku ajili watu hii ndio Tanzania ya viwanda tunayoitaka na usitegemee kuwa serikali itajenga kiwanda; kazi yake ni kuweka mazingira mazuri ili wewe mwekezaji wa ndani na nje muwekeze!! Acha hizo kijana;
 
Nimeipenda hii heshima kwako[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
apo tuna changanyanyana cjui nani mkweli nan ana potosha
 
Umefuga kuku kwa miaka mitatu sasa, na kwa mwezi unapata mayai 90 (tray 3) na bado unasema biashara inakulipa!..nadharia ya ufugaji wa kibiashara bado iko chini chana miongoni mwa wafugaji. Kufuga kwa miaka mitatu, na production ya mayai iko chini ya tray 3 kwa mwezi basi uzalishaji wako ni wa matumizi ya nyumban tu na si wa kibiashara.

Hongera sana pia kwa kupata soko kwenye mahoteli, ila ungetufafanulia zaidi, matumizi ya kawaida ya mayai kwenyebmahotel ni pamoja na kutengeneza chips za mayai, cakes, chapati na kwa kiasi flani ni vitafunwa vya breakfast...costwise, ulimconvice vipi mteja wako, (hotel) kutumia mayai ya kienyeji yenye bei juu zaidi kwaajili ya matumizi yao na kuacha kutumia ya kisasa yenye bei nafuu zaidi.
Wana jamii mnaweza mkajipimia wenyewe.
Hapana sikuwa na maana ya kwamba idadi ya kuku wote. Nina kuku specially nimewatenga kupata hayo mayai. Kuku wangu mmoja ana uwezo wa kutaga mayai hadi 18. Na wako ambao wanataga mayai hawalalii

Hizo tray 3 ni kwa ajiri ya kupata kuku tu ( vifaranga) na
 
Back
Top Bottom