Ushuhuda kutoka kwa Shehe Omari Mnyeshani

Wachawi hawana akili...Yaani MUNGU akadirie jambo lake halafu kiumbe awe na uwezo wa kulitengua?

Ukiona mkapa aliupata urais jua kuwa Qadar ya MUNGU ilishatangulia....Toka ulimwengu haujaumbwa tayari alishakadiria kuwa Mkapa atazaliwa na kuja kuwa rais wa Ardhi ya Tanzania mwaka 1995-2005.
 
Hii ni mpya isee na kituko cha mwaka si ajabu tz kuendelea kuwa masikini kwa ujinga huu mmh!

Yaani wachawi wakikutana wanajadili siasa za hii nchi tena..basi kuna wengine pia wakikutana wanajadili mpira wa simba na yanga..🤣🤣🤣😅
 
Labda uingie YouTube umsikilize mwenyewe, na ukipenda, unaweza kumpigia simu kumhoji. Kaweka namba zake za simu.
 
Nadhani la Mwenge ndio hilo la Bagamoyo
Kwa mujibu wa Omari Mnyeshani, Forojo Ganze alipoingia pangoni kuwasilisha kwa Shetdni maombi yao, ilionekana kama kulitokea ubishani kati yake na "mungu" wao. Ni kama vile "master" wake hakuwa ameridhia jambo fulani kuhusiana na ombi lake juu ya Tanganyika.

Alipotoka pangoni, ililazimu kubebwa na wenzake kutoka Bagamoyo hadi Dar Es Salaam. Mara tu baada ya kumaliza kuelekeza juu ya mbio za
mwenge, alikata roho. Wenzake hawakuweza kufahamu kilichomsibu alipokuwa pangoni kuwasilisha kwa Shetani maombi yao kuhusu Tanganyika.
 
Mimi naweza kukupinga nikiwa hoja hakuna anayeweza kupinga Kusudi la Mungu hii ndio maana ya Propaganda za kisiasa
Siyo kweli mkuu. Ili Mungu afanye jambo duniani, anahitaji mtu wa kushirikiana naye. Kadhalika na Shetani. Hawezi kufanya jambo duniani bila kushirikiana na binadamu.

Kama ayasemayo Mnyeshani ni ya kweli, inamaanisha kuwa katika hilo suala, Shetani alipata ushirikiano toka kwa mawakala wake waliopo Tanzania wakati huo mawakala wa Mungu wakiwa "usingizini".

Kama mawakala wa Mungu wangesimama katika nafasi zao, mpango wa Shetani usingefanikiwa.
 
...Ni KUZINDIKA Sio KUSINDIKA...Mengine yote ni Stupidity ! [emoji57][emoji57]
 
Japo masimulizi yake hayawezi kuthibitishwa Kisayansi, unafikiri nguvu za giza zina nafasi kwenye utawala wa Tanzania?[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmmh ngoja wazee wakongwe wenyewe ila niliwahi kusikia Kuhusu Lindi humu humu JF...kuhusu Makweta kipindi kile aliongelewa sana ktk nafasi tajwa...

NB : Tambiko Bagamoyo
Tambiko Lindi
Tambiko Kigoma
Hii nchi imerogwa na kufanyiwa makafara makubwa mno na kafara kubwa kuliko yote ni lile la bagamoyo la kukimbiza moto, likifuatiwa na la Tanganyika maji ya kina kirefu kisha la Lindi maji mapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmmh ngoja wazee wakongwe wenyewe ila niliwahi kusikia Kuhusu Lindi humu humu JF...kuhusu Makweta kipindi kile aliongelewa sana ktk nafasi tajwa...

NB : Tambiko Bagamoyo
Tambiko Lindi
Tambiko Kigoma
Hii nchi imerogwa na kufanyiwa makafara makubwa mno na kafara kubwa kuliko yote ni lile la bagamoyo la kukimbiza moto, likifuatiwa na la Tanganyika maji ya kina kirefu kisha la Lindi maji mapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…