Ushuhuda: Mafanikio na vikwazo katika biashara

Ushuhuda: Mafanikio na vikwazo katika biashara

Gulf Streamer

Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
90
Reaction score
40
Dhumuni la post hii ni kutaka kupata ushuhuda wa mafanikio katika biashara na vikwazo mbali mbali tunavyovipitia katika majukumu yetu ya kibiashara.

Mpo waajiriwa mnaojihusisha na biashara kama part time, wengine mliacha kazi ili mjiajiri wenyewe kama wafanyabishara, Mpo ambao maisha yenu ni biashara tu. Tungependa kusikia kutoka kwenu, mafanikio na vikwazo mlivyokumbana navyo.​

Kuna mambo mengi sana jamii ingependa kuyajua kuhusu biashara unayoifanya au uliyowahi ifanya, mpo ambao mnafanya biashara nje ya Tanzania, mpo mliokumbana na dhoruba ya wafanyakazi wenu kukimbia na mitaji yenu, mpo ambao wafanyakazi wenu walianzisha biashara kama zenu baada ya kupata ujuzi toka kwenu, mpo ambao mnakutana na hali ya ushirikina katika uendeshaji wa biashara zenu, Je partners katika biashara yako walikuwa msaada au mzigo kwako? Je ulifanikiwa katika kilimo, au ulikutana na changamoto gani? Mpo mnaofuata bidhaa China na nchi nyingine duniani, toeni uzoefu wenu uwasaidie wengine? Yapo mengi, kama mfanya biashara tungependa sikia toka kwako.

Nimeamua anzisha post hii ili iwe msaada kwa watu wanaopenda kujifunza kabla ya kuingia katika biashara, usije ukajikuta unafanya makosa yale yale yaliyofanywa na watangulizi wako.
 
Dah mimi nilijua unatoa ushuhuda wako kumbe unataka wa wengine? ni vizuri ukaanza na wa kwako
 
Dah mimi nilijua unatoa ushuhuda wako kumbe unataka wa wengine? ni vizuri ukaanza na wa kwako

nipo kwenye late 20s, ni gradute engineer, niliacha kazi mwaka 2012 baada ya ajira ya almost miaka miwili, nkaamua kujiajiri mwenyewe. Mafanikio yapo na changamoto ni nyingi kupita kiasi. Nlishajihusisha na biashara kadhaa kabla ya mimi mwenyewe kuamua kujiajiri. Nliamua kujiajiri kama mkandarasi, nmekutana na changamoto nyingi kwenye hili, kubwa ni mtaji mdogo na kucheleweshewa malipo yangu. Hii inapelekea muda mwingine kuacha kuchukua kazi, kwa kuhofia kufanya kazi chini ya kiwango na kukimbilia mikopo filisi(mikopo yanye riba za kubamiza).
Socially imekuwa ngumu kueleweka, atleast kwa sasa familia inaelewa malengo yangu ni yapi.

Mwaka 2014 nlipanga kufanya kazi za thaman ya dola laki 3, ila nimeishia kufanya kazi za dola elfu 80 tu.
2015 nna aim kufanya kazi za dola laki 5, stratergies kibao, sijui kama zitafanikiwa au laah.
Pia nategemea fungua biashara nyingine tatu kabla ya June 2015, na kusajiri kampuni nyingine 4 zitazoanza kazi kati ya 2016 na 2018.
 
Hakuna biashara isiyokuwa na changamoto mkuu. Kikubwa ni kutokata tamaa
 
Hakuna biashara isiyokuwa na changamoto mkuu. Kikubwa ni kutokata tamaa

Infact si biashara pekee, ajira na jambo jingine lolote ambalo litawahusisha watu wengine changamoto ni kawaida. Imefika mahali mimi ninaamini kuwa njia pekee ya kutokukumbana na changamoto ni kuamua kutokufanya lolote. The moment unapoamua kufanya kitu hata kama ni kidogo kiasi gani unakuwa umekaribisha changamoto. Kushinda au kushindwa kuko kwenye namna ya kuzichukulia hizo changamoto. Je unazichukua kama somo na kurekebisha panapostahili kurekebishwa then unasonga mbele au ndio unaona kuwa mwisho wako umefika? Kuna mtu mmoja alisema ubora wa mpiganaji haupimwi kwa punches anazotupa kwa mpinzani wake bali uwezo wake wa kuzikabili punches za mpinzani wake na bado akaendelea na pambano pasipo kukata tamaaa.
 
Mimi nimefanya biashara ya kilimo cha kibiashara, nilinunua Trekta nikawa nakodi mashamba makubwa. Lakini changamoto kubwa nilizokutana nazo ni hali ya ukame, unakuta unalima shamba kubwa, mazao yanatoka lakini mwisho wa siku upati kitu. Sasa nimeachana na kulima kwa kutegemea mvua, naandaa kisima cha maji

Changamoto nyingine, ukiwa wewe ni muajiriwa na unafanya biashara kuna mambo hayaendi kwa sababu kwa sasa watu wa kazi hawaaminiki

Pia nilikuwa na partiner wangu kwenye kilimo hakuwa mwaminifu, pesa ya kazi alikuwa anaila

Katika upandanji wa mazao kuna changamoto kwa sababu unahitaji planter, lakini pia planter ni expensive sana kuipata
 
Back
Top Bottom