Ushuhuda mwanaume mwenzenu: Nilioa Single Mother yalioyonikuta ni haya. Nilichukua uamuzi huu.


We mpumbavu!!!

Nakuuta tena
We mpumbavu!

Kwa dakika moja nione kama baba yako

Acha na usijaribu mkuu
Yaan usihoji na usitake jua kwanini
Ila sepa!
Narudia tena
Sepa

Shauri yako
 
Tulishakubaliana kwenye vikao vyetu hakuna kuoa single mother hadi uone kaburi la baba wa mtoto.
 
Pole Mkuu... Hakika saiv roho ishakomaa.... Sema fanya kama unalipa kisasi hivi... Mtafute Mke wA jamaa alafu mpangie bajeti nzuri. Unahakikisha mpaka jamaa na yeye anajuaa
Naunga hoja ahakikishe anampa mimba


Naomba namba ya mchango
 
Daaa haya maisha so poa binadamu tunapitia mengi sana
 
Single mothers hawaolewi, usithubutu. Kwanza wana Visirani na kila akikaa ni kutaja mwanae tu, kitu kidogo kanuna alooh achana na hawa viunbe
Hii ni kweli..niliwahi kuwa na single mother nikawa namsaidia kusomesha na mtoto wake...alikuwa na kisirani, wakati nakuwa na kazi Mimi ndiye nilikuwa namsomesha hiyo mtoto baada ya kudai Baba mtoto alimsusa

Ila alianza mtafuta Baba mtoto kisiri wakati Ada nilikuwa nalipia bila shida..ndio maana humu ndani watu wanasema uhakikishe kaburi la Baba unalijua

Sasa kama huyu wangu nilikuwa nampa kila kitu .nalipia mtoto wake Ada ..Ila alimtafuta Baba mtoto tena baadaye ndio akaanza kisirani..nikitoka kazin nakuta amenuna, nikimwongeresha anaongea kama bubu..nikimpa kama laki5 mfano..week moja tunakaa kwa upendo..baada ya hela kuisha..sijui alikuwa anaifanyia nini,(hela)maana kila kitu ndani nilikuwa nanunua..hela uliisha ataanza tena kununa na kujibu kwa mkato...mwezi wa 9nilipata kibalance flani ndio akachukua akakimbia mkoani zaidi ya milion 4 alichota akasema anaenda anzisha maisha mapya..U can imagine baadhi ya akili za single mothers
 

Oa mkuu hakuna mwanadamu mkamilifu hata wewe unamapungufu yako.
 
Jamani eeeeee... Mkilala mkiamka single mother, mkitembea, mkikaa single mother. Ebu wapumzisheni nao ni binadamu. Kusingekuwa na hao single mama kama sio ninyi wanaume. Hata huyu anaesemwa hapa amekuwa single mama sababu ya wanaume. Aliyemzalisha mwanzo angemuoa, yasingetokea.
Ila wanawake na sisi hatujitambui jamani. Yaani hadi unaweza pata hasira. Limtu limekupa mimba likakuacha, ukae unawasiliana nalo kisa mtoto. Kwani kulea kuna kazi gani kulea pekeako. Huyo mwanaume angekufa usingelea?
Aiseeee, nimeolewa na Allah aninusuru, itokee tumeachana, siji kufanya ufirauni wa kubembelezana na limtu kisa mtoto. Mtoto nabaki nae, kama kukutana watakutana paradiso kwenye makazi ya bwana.

MUHIMU. Ushauri wangu *
1. Tuwaheshimu wanawake. Hakuna ufahari kukaa nyuma ya keyboard na kuwasema na kudharirisha wengine. Nao ni binadamu. Tuwajenge kwa kuwaongoza, na kuwashauri yaliyo kheri, na kuwaombea yasiwapate yaliyo Shari.
2.kama huna malengo nae, usimuharibie maisha kwa kumzalisha na kumuacha.
3. Wazee wetu waliishi miaka 40 au zaidi pamoja, sio kwamba walipendana saaaana. HAPANA, lengo lilikuwa kutupa malezi ya pamoja, SO, kama mmeamua kuachana kwa kushindwa vumuliana na kuwapa watoto malezi mkiwa pamoja ACHENI UNAFIKI wa kujidai mnawajali hao watoto. Kila mtu ashike 50 zake.
4. Wanawake jitambueni. Ukiachwa achika. Kuendelea kugandana na mtu na ukoo wake kisa mtoto ni UZUZU uliopitiliza na kuvuka mipaka. Kama utaamua kuolewa tena, heshimu ndoa yako mpya.
5. JAMIIFORUM, ibaki kuwa sehemu salama na sahihi watu kupata maarifa, habari na ushauri. Tuelimishane bila chuki na kudharirisha wengine. Ifike kipindi tupunguze kuwadharirisha na kuwadunisha ndugu zetu ambao ni single mama. Hii inawaongezea tabia ya kujichukia, kujiogopa, na hata kujiamini. Wengi wamekuwa wakidanganya na kujificha. Na wengine hufikia hatua kuwachukia hata watoto.

Tusiwanyooshee tu vidole, tujaribu kutafakari chanzo cha tatizo. Wanaume punguzeni ubinafsi kupunguza wimbi la hawa single mama.
Wanandoa tuvumiliane, na tuviombee vizazi vyetu visije pitia haya maisha ya single mama, hakuna anayependa. Tuwape watoto malezi mazuri, mafunzo juu ya dini na maadili ili kupunguza wimbi la kuzaliana kabla ya ndoa.

Mwisho, I am sorry kwa comment ndefu, kwa nitakaowakera kwa maoni yangu pia, am sorry. Mwenye thread am sorry, sijaandika kukushambulia, ila nimepata uchungu maana wimbi la kuwasema hawa single mama vibaya limezidi. Umesema umeoa tena, mpende mkeo, mvumilie pia, ili nae asije kuwa single kwa kumuacha.

Binti yangu. Hakika nitakuombea Siku zote na sitachoka kukufundisha ili usipitie dhariri hii ya kusemangwa.
Na kwa uzao wowote wa kiume utakaotoka katika tumbo langu, nitauombea, nitaulea na kuufundisha ili usiwe chanzo cha kuongeza single mama hapa duniani labda itokee kifo ambacho ni faradhi kwetu.
 
Jiandae kumsamehe na kumpokea maana atarudi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…