USHUHUDA: Nikishalewa nafanyaga maamuzi mazuri sana

USHUHUDA: Nikishalewa nafanyaga maamuzi mazuri sana

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
1. Nilipata ajira kupitia ulevi na mlevi mwenzangu

2. Nilifanya maamuzi ya kuoa nikiwa nimelewa, na sasa nina familia

3. Nilinunua viwanja viwili mjini Dsm na nikajenga kupitia mlevi mwenzangu anayefanya kazi halmashauri idara ya ardhi

4. Niliamua ninunue gari nikiwa bar nimelewa na nikalinunua kwa mlevi mwenzangu

5. Nilipata tenda ya kusupply vyakula gereza fulan kupitia bar tukinywa na maafisa fulani

6. Nilianza kula kitimoto nikiwa bar,na sasa mm n mdau muhimu wa mnyama huyu

7. Projects nyingi za hela nilipata mawazo nikiwa bar nalewa na walevi wenzangu

8. Maamuzi magumu yote ya "lazima na mm niwe na kitu kile" nayafanyaga nikiwa nimelewa

9. Asilimia 95 ya jamaa zangu ninaosaidiana nao mjini niliwapata nikiwa nalewa

10. Niliamua niwe na paasport ya kusafiria nikiwa nimelewa. A na mlevi mwenzangu aliiprocess ndani ya siku 1 ikawa mkononi,na aliniletea bar

Informations zote za watu, nchi, dunia, fursa zinapatikana bar watu wakishalewa.

Maamuzi magumu mazuri huanziaga mtu ukilewa.

Connections zote bar.

DRINK BEER TO SAVE WATER..Lets meet at Deluxe Bar Rumba ~ Sinza Kijiweni, Dsm
images.jpeg
images-1.jpeg
 
Tabia ya walevi wote duniani ni moja KURAHISISHA MAMBO wakisha lewa kila kitu wanaona rahisi tu,
Kwa kijana unae angaika na kimshahara chako akifiki ata laki 6 usijidanganye kunywa pombe ata ile ya bia 1 au mbili utokaa uone faida ya kazi yako ata malaika washuke!!
 
Kwa shuhuda hizi mkuu ...unamaanisha

unategeemea pombe ndo kila kitu katika maisha yako !!!
si ndio?!
 
Kama kweli ni mlevi basi ni halali kabisa ule mshahara unaopata Wa 435,000 usikutoshe, na ndio maana ukaja hapa kuomba ushauri ufanyaje kwa mshahara huo Punguza pombe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hata siku yako yakufa utakuwa unatamka bar au pombe
 
Niko upande wa mtoa mada.....

Pombe msiifananishe na vitu vya kijinga tafadhali...Pombe inasaidia sana hata kwenye bajeti ya nchi, kodi yake inachangia mapato mengi sana.... Hahahaha (jokes)
 
Back
Top Bottom