Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,599
Hamjambo wadau wapenda maendeleo,
katika pita pita zangu za kuongeza ujuzi wa maisha, niliwahi kusoma kitabu cha RICH DAD POOR DAD kilichoandikwa na ROBERT KIYOSAKI, jambo mojawapo nililojifunza ni jinsi RICH DAD alivyowafundisha kazi Kiyosaki na rafiki yake ilhali wakiwa watoto wa umri mdogo kabisa (walipokuwa wanafunzi wa darasa la 4). Mwanzoni walidhani alikuwa akiwanyanyasa kumbe alifanya vyema kuwafunza kazi na jinsi ya kutengeneza pesa, leo hii wako vizuri kiuchumi kwasababu walipewa msingi mzuri wa elimu ya pesa.
Turudi kwenye mada, jirani na ninapoishi kuna familia ya kichaga imejenga mji wa kuishi na fremu za maduka, juzi nikaenda kwa duka lao kununua mahitaji kadhaa ila nilipofika sikumkuta muuzaji mtu mzima kama nilivyozoea badala yake nikamkuta mtoto mdogo wa kike mwenye umri usiozidi miaka minane.
Akanikaribisha vizuri nami nikamsihi amfate mama yake kuja kunihudumia dukani lakini cha ajabu yule mtoto wa kike akaniuliza kwani wataka nini nikuuzie? Nikamjibu kwa swali, utajua kunirudishia chenji? Mtoto akakubali 'ndiyo nitaweza' .
Bhasi nikampatia elfu 2 nikamwambia anipe vocha ya elfu moja na soda moja ya chupa, yule mtoto akanihudumia kwa usahihi kabisa na chenji akanirudishia vyema.
Nikabaki kushangaa jinsi alivyofunzwa vyema yule mtoto mdogo, ila nikajifunza kuwa ukitaka mwanao apende biashara na kujishughulisha mfunze mapema kabisa, ukitaka mwanao awe na mafanikio ya kifedha baadae bhasi mfunze maana ya pesa na jinsi pesa inavyofanya kazi bado angali mdogo.
Funza mwanao aijue pesa angali mdogo.